Nchi yetu siyo salama, Tujifunze mbinu za kujikinga na watekaji

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Sasa hivi hali nchi siyo salama, ni vizuri tukaelimishana mbinu za kujikinga na kujinusuru dhidi ya watekaji .
Ndugu zangu hawa watekaji ni wauaji, ni makatili na inaonekana serikali ya Tanzania siyo ya kuaminika katika suala hili, Kiufupi imeshindwa kusimamia usalama wa raia. Wananchi wamepiga kelele, wamelaani lakini hii hali inaendelea.

Miezi michache iliyopita, Chama cha mawakili wa TLS walitoa taarifa juu ya idadi ya watu waliotekwa tangu mwaka 2021. Hali inatisha, ni wengi wanakaribia 100.

Sasa kwenye uzi huu, naomba tupeane njia za kujikinga na Watekaji nchini.

Mimi njia ninayoiona
1. Kamwe usikubali kupelekwa katika gari usiyoijua hata ukionyeshwa bunduki. Ukionyeshwa Bunduki na kulazimishwa kupanda gari ujue hiyo bunduki ndo inaenda kukuua huko uendako. Bora upige kelele wakuue hapohapo ulipo ili angalau ndugu zako waokote mwili.

2.Usikubali kutembea mwenyewe kwenda kwenye gari, wewe lala chini, Ukisimama ni rahisi wao kukusukuma lakini ukilala chini watasumbuka kiasi fulani na raia watajaa, angalau watajua kuwa unatekwa

3. Piga kelele za Watekaji, wauaji, wanataka kuniteka ili umma ujue unatekwa

Chnagieni na mbinu nyingine:
 
Tuongeze lishe tunenepe vya kutosha
Screenshot_20241113-114234.jpg
 
Mbinu nzuri kuliko zote unayoikwepa wewe kuiweka hapa na ambayo ni ya uhakika ni kuiondoa ccm madarakani kwa udi na uvumba.

Hii ndio manusura ya mambo yote mabaya unayoyaona Tanzania
 
Sasa hivi hali nchi siyo salama, ni vizuri tukaelimishana mbinu za kujikinga na kujinusuru dhidi ya watekaji .
Ndugu zangu hawa watekaji ni wauaji, ni makatili na inaonekana serikali ya Tanzania siyo ya kuaminika katika suala hili, Kiufupi imeshindwa kusimamia usalama wa raia. Wananchi wamepiga kelele, wamelaani lakini hii hali inaendelea.

Miezi michache iliyopita, Chama cha mawakili wa TLS walitoa taarifa juu ya idadi ya watu waliotekwa tangu mwaka 2021. Hali inatisha, ni wengi wanakaribia 100.

Sasa kwenye uzi huu, naomba tupeane njia za kujikinga na Watekaji nchini.

Mimi njia ninayoiona
1. Kamwe usikubali kupelekwa katika gari usiyoijua hata ukionyeshwa bunduki. Ukionyeshwa Bunduki na kulazimishwa kupanda gari ujue hiyo bunduki ndo inaenda kukuua huko uendako. Bora upige kelele wakuue hapohapo ulipo ili angalau ndugu zako waokote mwili.

2.Usikubali kutembea mwenyewe kwenda kwenye gari, wewe lala chini, Ukisimama ni rahisi wao kukusukuma lakini ukilala chini watasumbuka kiasi fulani na raia watajaa, angalau watajua kuwa unatekwa

3. Piga kelele za Watekaji, wauaji, wanataka kuniteka ili umma ujue unatekwa

Chnagieni na mbinu nyingine:
Kwenye jamii husika tengenezeni utaratibu wa lugha kimya kujinasua na wasiojulikana, (silent language)
 
Tutembee na filimbi shingoni, ukiona huelewi elewi unaipuliza kwa nguvuu,

Wananchi watakaokuwa karibu nao wanaanza kupuliza zao.

Kila mwenye filimbi eneo la tukio akipuliza, watekaji watapagawa na kukimbia.

Gen Zee movement kenya, filimbi zilisaidia sana kuwapagawisha askari ndio maana walipata wakati mgumu sana kukabiliana na waandamanaji.

Hata mauaji ya Rwanda, filimbi zilitumika.
 
  1. kuwa mwangalifu unapopanga kukutana na mtu/watu mahali fulani.
  2. usiopoe wala kuopelewa na usiyemjua... sio unatongoza au unatongozwa unaendaa tuu kama kifurushi
  3. kuwa mwangalifu uitapo tax au boda au bajaji usiyomjua dereva utakayoikuta nje tu nyumbani kwako au popote unapotoka iwe bar au kazini kwako
  4. usizoee mtu uliyekuta barabarani, bar au popote na kuanza kuongozana nae
  5. usipokee wito wowote kizembe
  6. anza kufanya mazoezi angalau uwe na pumzi ya kupiga kelele utakapoanza kukabwa
 
Lazima kuwe na mlio maalum kwenye jamii husika, mazoezi na kula vizuri ni muhimu hawawezi kukuburuta kizembe
 
  1. kuwa mwangalifu unapopanga kukutana na mtu/watu mahali fulani.
  2. usiopoe wala kuopelewa na usiyemjua... sio unatongoza au unatongozwa unaendaa tuu kama kifurushi
  3. kuwa mwangalifu uitapo tax au boda au bajaji usiyomjua dereva utakayoikuta nje tu nyumbani kwako au popote unapotoka iwe bar au kazini kwako
  4. usizoee mtu uliyekuta barabarani, bar au popote na kuanza kuongozana nae
  5. usipokee wito wowote kizembe
  6. anza kufanya mazoezi angalau uwe na pumzi ya kupiga kelele utakapoanza kukabwa
Ukimjua dereva ndiyo hatari zaidi utajisikia uko nyumbani kataa mseleleko, (kikulacho kiko nguoni mwako), vilevile ukitaka kumkamata kuku una mtupia tupia kifuatacho ni..........
 
Back
Top Bottom