Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Nchi za Afrika zimetajwa kuwa zinaweza kujifunza kutoka kwenye mtindo wa maendeleo wa China kama zikitaka kupata maendeleo ya kasi.
Akiongea kwenye mahojiano maalum na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Profesa Waithaka Niraki wa Chuo Kikuu Cha Nairobi amesema, mbali na kujifunza kutoka kwenye mtindo wa maendeleo wa China, nchi za Afrika pia zinaweza kunufaika na teknolojia na hata kuweza kujiamini, huku akiwa na matumaini kuwa China inaweza kuwa tayari kuzisaidia nchi za Afrika kwa teknolojia na hata kuzipa moyo wa kujiamini kujiletea maendeleo.
Akizungumzia ripoti ya mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Profesa Waithaka amesema ripori hiyo imejikita kwenye uongozi wa jumla, unaongalia nyanja zote za maisha, na sio tu pesa na utajiri.
Amepongeza njia ya kujiendeleza ya China na kuitaja kuwa ni njia muhimu inayotoa mafunzo ya kuleta masikilizano kwenye jamii, kushirikiana na mataifa mengine ya kuzipa uwezo nchi za Afrika.