Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Nchi kadhaa za kiarabu zimeanza kuingia akili kwa kukataa kuachia Marekani kutumia ardhi zao kuanzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Houth wa Yemen.Hatua hiyo itaifanya Marekani kushindwa kuwazuia Houth na itakuwa ni msaada wa nchi hizo kwa Palestina.
Nchi hizo ni zile ambazo zimekuwa washirika wakubwa miaka ya nyuma wa Marekani kushambulia Iraq,Afghanistan na Libya.Mshirika wa karibu kufanya hivyo ni UAE aliyeungana na Oman,Qattar na Kuwait.
Kuzuiwa kwa Marekani kutumia ardhi hizo kutafanya hata meli za kivita zilizo kwenye bahari jirani na nchi hizo za bara Arabu kuishiwa na nyenzo za kupiga kwa haraka.Matumizi ya ndege za B1 kutoka Marekani moja kwa moja nayo hayawezi kutegemewa kwa kiasi kikubwa kutokana na masafa ya kulazimika kutudi kujaza makombora mengine yanapoisha.
Katika hatua nyengine ya mabadiliko katika nyoyo za viongozi wa mashariki ya kati kuhusiana na vita vya Gaza,raisi Erdogan wa Uturuki ameitembelea UAE na baadae kukutana na raisi Elsisi wa Misri kutia mkazo wa kuitaka Israel isienendelee kuwaletea madhara wapalestina wa Gaza ambao wameshakimbia sana vita na sasa wamechoka.Hawana tena nguvu na wala pahala salama pa kwenda kutoka Rafah.