Naona unataka kuleta ubishi as if tupo kwenye mihadhara ya uswahilini na unaitafsiri biblia namna unavyotaka wewe na unabishia mpaka neno la Mungu. ok ndo elimu akhera inavyokuongoza hivyo bakia na msimamo wako na tafsiri zako
Mimi sijatafsiri hata aya moja hapo , nimeleta nukuu kanma zilivyo , usinipakazie bure , anayetafsiri ni wewe bila kutuwekea ushahidi wa aya
Jibu haya maswali usikimbie
Aya hii haisemi kuhusu kusamehewa dhambi wayahudi
“Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lenye kuzaa matunda yake. (Kutoka Biblia ya KJV, Mathayo 21:43)”
Sasa tuekee aya bwana yesu anasema kuondolewa ufalme sio kuondolewa upendo , usituletee injili yako
halafu umetuwekea aya ya paulo inayosema
Rum 1:16
Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa
Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
Hapo Bwana Paulo amekusudia injili ipi , kati ya hizi ??
Una mistari inayoonyesha kwamba Paulo alikuwa akihubiri Injili yake mwenyewe...
Warumi 2:16
16 Hili litatukia siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama Injili yangu inavyotangaza.
Warumi 16:25
Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwathibitisha ninyi kwa Injili yangu na uhubiri wa Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyofichwa tangu zamani za kale;
Una mistari inayoonyesha kwamba Paulo alikuwa akihubiri Injili ya Mungu...
Warumi 15:16
16 niwe mhudumu wa Kristo Yesu kwa watu wa mataifa, mwenye wajibu wa ukuhani wa kutangaza Habari Njema ya Mungu, ili watu wa mataifa mengine wawe dhabihu inayokubalika kwa Mungu, iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
2 Wakorintho 11:7
7 Je, ni dhambi kwangu kujishusha ili nipate kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Habari Njema ya Mungu bila malipo?
Una mistari inayoonyesha kwamba Paulo alikuwa akihubiri Injili ya Kristo...
1 Wakorintho 9:13
Lakini hatukutumia haki hii. Badala yake, tunavumilia chochote badala ya kuizuia Injili ya Kristo. 13 Je!
2 Wakorintho 2:12
12 Nilipokwenda Troa kuhubiri Habari Njema ya Kristo, nikaona kwamba Bwana amenifungulia mlango.
2 Wakorintho 9:13
13 Kwa sababu ya utumishi mliojionyesha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utii unaoambatana na kukiri kwenu Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu katika kushiriki pamoja nao na pamoja na watu wengine wote.
2 Wakorintho 10:14
14Hatuendi mbali sana katika kujisifu kwetu, kama ingekuwa hivyo kama hatungekuja kwenu, kwa maana tulifika kwenu kwa Habari Njema ya Kristo.
Warumi 1:9
9 Mungu, ambaye ninamtumikia kwa moyo wangu wote katika kuihubiri Habari Njema ya Mwanawe, ni shahidi wangu jinsi ninavyowakumbuka daima.
Mstari wa mwisho unaonyesha tofauti kati ya Mungu na Mwana wake (ikimaanisha Yesu).
Je, Paulo alikuwa akihubiri injili yake mwenyewe, injili ya Yesu au Injili ya Mungu?