Nchi za mabeberu wana Ramani zinazoonyesha maliasili ilipo Tanzania na nchi nyingine mbili. Wao wanaamini walitukabidhi tuwatunzie lakini si zetu

Afu ww umezidi matusi sana hapa jamvini, alafu hunaga mambo ya maana ni upumbavu tu na kulobulobu kwenye hoja
Hapana.

Inawezekana pia na wewe huwa unamsoma ukiwa umekwishaweka akili hasi kwa michango yake.

Hebu kwa mfano, katika hayo aliyoandika hapo, ni matusi gani aliyoandika hadi ikabidi umjibu hivyo?

Hebu msome tena vizuri bila hasira naye, utaona kwamba kuna maana sana katika hayo aliyoandika, na wala hakuna "upumbavu tu na kulobulobu..."
 
We jamaa muongo sana eti wanakuanzia mbali sana huko mbali sana ni wapi huko. Nchi inongozwa na wahuni na majizi na mikataba yote wanayoingia ya rasilimali za nchi ni kuwaneemesha wao. Kumbuka mabilioni ya Uswiss na mikataba mingine yote IPTL, Richmond, Dowans, Escrows etc ilijaa wizi na ufisadi wa kutisha na nchi imeporwa trillions kwa sababu ya majizi wanaojifanya Viongozi na kuwa na Bunge DHAIFU.
Hizi nchi hazikupigi wala kukutisha ila hukuanzia mbali sana.
 
Naamini mada yangu imeeleweka kwa alietaka kuelewa.

Wewe kama yakuchanyanga ipotezee.
 
Lakini si kulikuwa na safari nyingi za nje kutafuta wawekezaji?

Au ushasahau?

Na hili la Bunge kuuona mkataba nitajie nchi gani yafanya hivyo kujadili mikataba kama ya kuuziana silaha wapi Wabunge wanapewa wasome?

Maana hata madili kama ya Uingereza au Mmarekani kumuuzia silaha Saudi Arabia au Israel haijawahi kusomwa na Wabunge na ikawa scrutinised.
 
Nimesomaaa,ila nilipofika kwenye hii sentensi "uranium ambavyo ni malighafi muhimu kwa utengenezaji wa betri za magari, simu za mkononi" hapo nikashtuka!nadhani panahitaji tupate ripoti ya CAG!
 
Mkuu! Sisi hatuna uwezo wa kushindana na hao unaowaita mabeberu wakidhamiria kufanya yao! Hatuwezi kuwazuia! Ila tunaweza kukaa nao meza moja tukaweka mambo sawa..
Hakuna Cha mabeberu Wala nini ila ishu ya mabeberu inaletwa na viongozi wetu. Hawataki weka Sera ambazo mwananchi wa kawaida anaweza faidika nazo hawachez na fursa. Tuchukulie kwa upandé wa viwanda tuchukulie utengenezaji wa magari hasa mabasi, Sera zetu mbovu zimeua viwanda vyote vya kuchonga mabasi tumebaki ni wagaizaji lakin ukiwasikiliza viongozi wetu always ni mabeberu.
Tuje kwenye upandé wa kilimo, nchi zote zinazotuzunguka zinauhaba mkubwa wa chakula hasa mchele ila kwa sabab ya Sera mbovu mchele unaozea mashamban hivyo kuwafanya makulima waendelea kuwa maskini.
Africa nzima hakuna nchi inayojitosheleza kwa kilimo Cha ngano na nahitaji ni makubwa Sana lakin Sera zetu mbovu hakuna uzalishaji wq ngano kabisa. Ngano mpaka mwez Jana China inauzwa usd 310 kwa tonne jumla, lakin hakuna mzalishaji kutoka Africa.
Kodi na tozo zetu bado ni chini lakin bado zinaweza tulipa kuliko wenzetu.
Ni Africa tu mkulima anaweza akauza Mahindi kg 350 na ikamlipa tofaut na wenzetu. Ila Sera zetu mbovu Sana .
Wakati wenzetu kupanda eka moja ya mahindi atatumia usd 100 pamoja na mbegu, Africa inaweza fika karibia Mara mbili ya hapo na bado ikalipa. Wakati kuvuna Mahindi kwetu itahitajika tsh40000 ya kuvuna na 40000 kupukuchua Mahind kwa eka wenzetu watahitaji Lita 90 za mafuta kuvuna eka 20 za Mahindi yaliyopukuchuliwa wastani wa 9000 kwa eka lakin bado hawawez uza Bei tunazouza.
Kwa mifano hiyo sisi tuna nafasi nzuri ya kuendelea kuliko hao mnaowaita mabeberu.
Mabeberu ni viongozi wetu wazungu wanalihitaji soko letu
 
Sasa kwani ukienda nje kusaini mikataba inahusiana vipi na kusaini mikataba ya kifisadi? Acha kubadili subject na kutaka kuingiza mambo ya Marekani kuhusu mikataba ya rasilimali za Watanzania.
 
Afu ww umezidi matusi sana hapa jamvini, alafu hunaga mambo ya maana ni upumbavu tu na kulobulobu kwenye hoja

Yaani ww utukanwe na nani, utukanwe ili ujipatie umaarufu? Hapa unapewa ukweli unaokuumiza. Hizi Id za 2020 zilikuja rasmi kulinda siasa Chafu,na kuendekeza propaganda mfu za awamu ya majizi ya Kura, kuelekea uchaguzi mkuu. Na mimi Id hizi za wanafiki nimezipa vitasa vikali, hivyo sishangai huu mrejesho.
 
Kwa bahati mbaya sana sisi watanzania tumejikita kwenye kuangalia maisha ya leo tu, tunatumbua kila kitu kifisadi, anayejaribu kuangalia ya kesho pia anageuzwa adui ,

Itatuchukua muda sana kuja kushtukia mambo kama haya na hata tukifanya hivyo itakua tayari tumechelewa.

Inasikitisha sana lakini ndivyo tulivyo.
 
Kuna kamati za Bunge zinazofanya kazi kama hizo katika nchi nyingi, hasa hizo kubwa kubwa.

Haiwezi ikawa kazi ya waziri pekee, au hata siri ya Rais pekeyake.
 
Umeandika upumbavu mwanzo mwisho.
Hapana mkuu BAK.

Tusiende huko.

Pamoja na ugumu wa mada yake, lakini nadhani haistahiri maneno mazito kama hayo.

Amekwishajieleza kivingine, tena kwa kifupi zaidi, na nadhani anaeleweka.

Tafsiri ya makala aliyoifanya imeongeza ugumu wa makala yenyewe.
 
Beberu asipo yahitaji hayo madini wewe mtu mweusi mwenzangu unaweza kuyafanyia nini?
 
Ndiyo. Hiyo ni tafsiri toka mahali fulani.

Lakini tafsiri yenyewe siyo ya kiustadi hata kidogo.
Mkuu, moja ya masomo niliyopiga kisawasawa ni history.

Kwa kuwa history is about past, present and future basi huwa najikumbusha ingawa si eneo langu ambalo ndio nina utaalam nilio nao.

Hii mada yangu sijaitafsiri kokote ni mtizamo wangu binafsi baada ya kuyaona na kuyasikiliza yanayoendelea chini kwetu, barani Afrika na mtazamo wa nchi ziloendelea juu ya Tanzania.

Pia ni tafakuri yangu juu ya kinachoendelea kule Msumbiji na hatima ya sisi waafrika.

Ningeitafsiri ningeweka chanzo ila nimetumia kitabu kimoja tu.
 
Umeandika upumbavu mwanzo mwisho.
Mkuu, punguza jazba, mwisho wa siku huu mjadala utaisha.

I respect Mr Assad ambae mara mojamoja huwa namsikiliza pale kijiwe cha Mnazimmoja akimwaga madini.

He has had a very distinguished career and he is well respected.

Lakini Prof Assad alisahau kwamba hii ni Tanzania ya CCM na ina namna yake ya kuendesha nchi.

Natarajia Freeman Mbowe kesho atatoa mwelekeo wa siasa za upinzani maana mfumo bado upo pale pale regardless nani ni raisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…