Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken hivi karibuni aliahidi kwamba Marekani inapanga kutumia dola bilioni 200 kati ya mpango wa miundombinu wa dola bilioni 600 uliotangazwa hapo awali na G7 kupambana na "nafasi ya uongozi ya China barani Afrika na nchi nyingine maskini." Mwezi uliopita, Umoja wa Ulaya pia ulisema kuwa utawekeza Euro bilioni 150 barani Afrika katika miaka kadhaa ijayo ili kupanua ushawishi wake huku ikidhoofisha nguvu ya China barani Afrika.
Pengine kwa sababu wamekuwa na wivu na maendeleo ya haraka ya uhusiano kati ya China na Afrika katika miongo miwili iliyopita, siku hizi nchi za Magharibi zimeelekeza tena macho yao kwa Afrika, na kujidai wao ni wenzi wa ushirikiano walio muhimu na kuwategemewa katika msingi wa usawa, wakitumia mbinu ya “kutongoza kwa pesa”.
Lakini ukweli ni kwamba, kama nchi hizi za Magharibi hazijatambua matatizo yao halisi, China itaendelea kudumisha ushawishi wake mkubwa barani Afrika.
Kwanza, tofauti na Magharibi, China kamwe haichukulii Afrika kama sehemu yenye njaa na vita, lakini bara lenye fursa. Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC lililoanzishwa mwaka 2000, si tu kwamba lilifungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya China na Afrika, cha muhimu zaidi ni kuwa limefanya "ushirikiano wenye usawa na wa kunufaishana" kuwa kanuni ya nchi za Afrika kukuza uhusiano na nchi zilizo nje ya bara hilo. Licha ya utajiri wake wa maliasili, miundombinu mibovu ni kitu kinachokwamisha zaidi maendeleo ya Afrika.
Kwa miongo kadhaa, China imezifunika nchi za Magharibi katika suala hili. Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyotolewa na taasisi ya washauri mabingwa ya Kenya ya The Inter Region Economic Network (IREN) mwezi Julai mwaka huu, katika miaka 15 iliyopita, miradi ya ushirikiano ya barabara na madaraja iliyotekelezwa na China barani Afrika imebadilisha sura ya Afrika "kwa uhalisi na uwazi ", na kusaidia nchi za Afrika kukuza maingiliano ya usafiri na masoko.
Wakati huo huo, China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 13 mfululizo .
Mwaka 2021, jumla ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa takriban 35% kuliko mwaka uliotangulia, na kufikia dola za Marekani bilioni 254.3. Miongoni mwao, mauzo ya nje kutoka Afrika hadi China yalifikia dola za Marekani bilioni 105.9, na kuweka rekodi mpya kihistoria.
Pili, wakati serikali na kampuni za China zikiiunganisha China na Afrika kwa umoja na urafiki katika msingi wa usawa na kutoingilia mambo ya ndani, kukamilisha miradi na kutekeleza ahadi zao haraka iwezekanavyo, nchi za Magharibi zimejikita katika kuuza maadili yao barani Afrika na kuambatanisha masharti na uwekezaji wao kwa njia ya "uzazi mkali".
Kwa mfano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitamka hadharani katika ziara yake ya nchi tatu za Afrika hivi makaribuni kwamba Marekani iko tayari kufanya biashara na nchi za Afrika, lakini inachukulia masuala ya usalama na haki za binadamu kama masharti ya ushirikiano wao.
Hivyo si vigumu kuona ni kwa nini nchi nyingi za Afrika sasa zinaiona China kama mshirika wao muhimu zaidi, na sio Magharibi.
Kama alivyosema makamu mwenyekiti wa zamani wa kamati ya Umoja wa Afrika Erastus Mwencha, "Katika ushirikiano kati ya China na Afrika, China haisemi kamwe 'tunadai hiki au kile', bali inazipa nchi za Afrika haki ya kuchagua kwanza.
" Nchi za Magharibi zinatakiwa kutafakari sera zao kuhusu Afrika, kwani historia ya miongo kadhaa iliyopita imedhihirisha kwamba nchi za Magharibi haziwezi kuwa na uhusiano mzuri na imara na Afrika kwa “kujitangazia maadili yao”, na kwamba barabara inayofikia vijiji vya pembezoni, nafasi za ajira kwa vijana ni muhimu zaidi.
Nchi za Magharibi zinapaswa kuwa na uhusiano na Afrika unaowaweka sawa na kutoiona tena Afrika kama mwombaji. Katika suala hili, China imetoa mfano bora, lakini hadi sasa nchi za Magharibi hazijafahamu ipasavyo.