Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Wametumia kigezo gani kuiweka nchi kama Senegal, Liberia, Tunisia, Sierra Leone na kuiacha nchi iliyobarikiwa Amani kutokana na subira na uvumilivu wa watu wake Tanzania?
Nimeishi kwa karibia mwaka mzima Liberia na Senegal. Na mara kadhaa nimetembelea Ghana. Nchi kama Liberia, licha ya kumbukumbu mbaya ya vita vya huko nyuma, kwa sasa katika suala la utawala bora, wapo mbali sana kulinganisha na Tanzania. Kule kukiwa na tatizo dogo tu, hata lililomgusa mtu mmoja tu, na hasa kama tatizo lenyewe Serikali imehusika au kutajwa kuhusika, viongozi, hasa mawaziri watahangaika mpaka wamfikie huyo mtu ili wajue tatizo ni nini, na taarifa itatolewa kwa umma bila ya kuchakachuliwa. Hapa akina Makonda, licha cha kutajwa mara nyingi na watu wengi juu ya kuhusika kwake na utekaji, utesaji na uuaji wa watu wanaowakosoa watawala, lakini hawajawahi kuhojiwa hata siku moja!!
Nakumbuka kuna mkasa mmoja mdogo uliomhusisha mfanyakazi wetu, raia wa Madagaska, kuwa alisumbuliwa na maofisa wa polisi barabarani, habari ikatoka kwenye blog, siku 2 baadaye, mawaziri wawili wa wizara husika wakiambatana na maogisa wao wa chini wanne, walifika kambini kwetu usiku, tulikaa nao kwa masaa 6. Jamaa aliombwa msamaha, na polisi waliotajwa, wakati hayo yanaendelea walikuwa tayari wamesimamishwa kazi kwa uchunguzi. Na taarifa ya tukio lile ilitolewa kwa umma kama ilivyokuwa.
Tena Liberia au Ghana, ukifanya kosa hata la barabarani, omba tu msamaha, usithubutu kutoa chochote kumpa askari, ukitoa tu rushwa, hakika utaenda jela. Ukitoa rushwa, polisi anaona umempa nafasi ya kuthibitisha uaminifu wake. Utakamatwa hapo hapo. Kosa la mwanzo litasahaulika, la kutaka kuhonga polisi ndiyo litakuwa kubwa.