Lazima uwe mjinga kweli kulishangilia hili.
Hujiulizi kwa nini South Africa yenye watu takribani 50 milioni ina GDP zaidi ya dola bilioni 400. Kenya yenye population ya takribani 50 million ina GDP ya karibia dola 120 bilioni, halafu sisi ambao ni zaidi ya milioni 60 tuna GDP dola bilioni 75. Halafu punguani wanashangilia.
Bila kufahamu kuwa hizo nchi nyingine tunazodhani tumezipita ni pamoja na nchi ndogo zenye watu wachache sana kama Burundi, Rwanda, Equatorial Guenea, Botswana, Namibia, ambazo kimsingi zipo juu sana kwenye utajiri halisi, yaani human development.
Ni sawa na jitu liwe na wake 10, watoto 60, halafu kwa mwaka, wote kwa pamoja wanapata milioni 20, halafu linaamini limempita mwenzake mwenye mke mmoja na watoto 3, lakini wamepata milioni 15.