Nchimbi, Huwezi Kuwa Askari Unayeitelekeza Tanzania Wakati wa Mapambano Kama Sasa

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
22,898
Reaction score
33,309
Ndugu Nchimbi kwanza nikupe pongezi nyingi kwa kuondoka kifungoni.

Awali nilitangaza humu kwamba ningefungua masikio yangu yote nisikilize uliyokuwa ukiyaseama baada ya maneno uliyosema kuhusu waTanzania waidai katiba kwa nguvu zao zote..

Maana yangu ya kufungua masikio, nilitaka niwe na uhakika wa hiayo na mengine ambayo ulishayasema yaliyoonekana kuwa tofauti na wenzio; ambao wengi tuliamini mnawafanyia waTanzania ulaghai na maigizo.

Sasa imebainika kuwa yako hayakuwa maigizo, bali ni msimamo uliokuwa ukiuamini. Wengi tukawa tunashangaa utakuwaje na msimamo kama huo halafu ukaendelea kubaki na kushiriki na watu waovu waliokuzunguka kila mahali. Sasa mashaka hayo tumeyaweka pembeni.

Jambo ninalotaka kulizungumzia hapa, na kama ukipenda ulichukue kama ushauri kwako.

Ulisema kwenye barua yako, kwamba unaachana na siasa (umestaafu) na utumishi wa umma.

Sasa hapa itabidi utakapokuwa umetulia vizuri na kutafakari, ufafanue maana yako ya "kustaafu siasa na utumishi wa umma"

Maana inayoniijia kwa haraka haraka ni kuwa hupendi tena kutegemea siasa na utumishi wa umma kuendesha maisha yako kwa mahitaji ya kila siku ya kibinaadam.

Vinginevyo sifahamu mtu anavyoweza kujiondoa moja kwa moja katika utumishi wa taifa lake katika nafasi na hali mbalimbali. Kwa maoni yangu, anayestaafu maswala ya nchi ni yule ambaye amemaliza maisha yake hapa duniani.

Kwa hiyo sioni jinsi utakavyoweza kustaafu; hasa baada ya kujipambanua wazi kuwa wewe na kundi ulilokuwemo hamkuwa pamoja.

Umri bado unakuruhusu, utawezaje kujifunga minyororo huku ukiangalia taifa ulilolitumikia kwa muda mrefu likiangamia; unaweza kweli ukaishi kwa ustaafu wa amani?

Sikushauri ukimbilie kwenye vyama vya upinzani vilivyopo; na hasa hasa CHADEMA. Kaa utulie kwanza, lakini usijiondoe kwenye maswala ya utetezi wa taifa hili kwa kutumia nyenzo mbalimbali zilizopo kulipigania taifa hili.

Kama kulikuwa na wenzako huko ulikokuwa wakikuamini unachosimamia, endelezeni msimamo huo, muujenge, hata kama hamna chama cha kukitumia kwa sasa.
Waungeni mkono bila ya masharti yoyote CHADEMA katika juhudi zao za kuwaunganisha waTanzania waukatae utwana huu wanaoletewa na kundi uliloliyupa mkono.

Huko mbele ya safari, kama juhudi zenu zinaimarika na kudumu, mambo ya wapi mtaelekeza juhudi hizo yatajipambanua yenyewe.

Naomba nikusisitizie tena, huwezi kustaafu huku ukiwa kwenye mateso

Sasa masikio yapo wazi kabisa kusikiliza unayoweza kusema katika ukombozi wa taifa hili.
 
20260820_233810.png
 
Aisee sionj ni kwa namna gani Nchimbi ataweza kuzungumzia yaliyotokea. Ndio maana naamini ukiondoa shinikizo la damu...EN atatafutiwa ping na wote waliokuwa nyuma yake.
Kuna kuzungumza kusikoelekeza lawama/shutuma..

Tanzania inahitaji kuponywa haraka, bila ya kuelekeza malumbano moja kwa moja na hao wanayoifukia nchi sasa hivi.
Watu watamwelewa tu vizuri.

Kwa mfano swala la uhitaji wa katiba si lazima liwe la kugawa lawama kwa yeyote, hata kama inajulikana ni nani wasiotaka mabadiliko hayo.

Unajuwa, hata hawa waovu wanao ukomo wa kufanya maovu yao kwa watu wasiowataka.

Kwa mfano, unafikiri Tundu Lissu wanapenda sana kumwona anavyowahangaisha hata akiwa jela?
 
Mkuu Kalamu tumwangalie EN kidogo
EN kalelewa CCM kuanzia Chipukizi, UVCCM, NEC, CC, Katibu Mkuu CCM hadi VP.

EN ameona mengi kuanzia Ntyerere hadi SSH. Nchimbi kahudhuria viklao vingi vilitoa maamuzi magumu ya Chama na Serikali. Emma anajua yaliyomkuta Jumbe, Salimin Komandoo, Salim Ahmed, VP Garibu, Maalim Seif, Horace Kolimba, Sophia Simba, Membe, Edo Lowassa, Sitta hadi Ndugai. EN ni ''insider''

Kauli ya ''Katiba na Wananchi wakomae'' in hind sight'' aliijua consequences zake.
Ukisikiliza ile hotuba, EN alikuwa tayari kwa lolote hata 'posture' yake ilionyesha wazi.

Kabla ya hapo, EN alimwambia SSH kwamba kama atataka kubadili VP yupo tayari. Hii maana yake ni kwamba EN aliona asiyokubaliana nayo akajipa moyo kwamba kuwa ndani ya system anaweza kubadilisha hali.

Rudia ile kauli ''komaeni hapo hapo kwa faida ya vizazi vijavyo'' na alizungumzia faida kwa makundi yote ikiwemo Wapinzani etc. Kuna elements za ''haki'' alizozungumzia indirectly Kwahiyo si kauli moja ya Katiba, kuna mengi hakukubaliana nayo na alikuwa tayari kwa consequences zake

Kauli kwamba amestaafu ''siasa na utumishi wa Umma'' zilikuja kwasababu anafahamu system inafanyaje kazi.
EN alijua kauli ile ilipoanza kwa Yuda ni watu waliotumwa kufikisha ujumbe. Yule aliyeitoa anatoka upande gani!!!

EN alimaanisha kwamba anastaafu siasa ili abaki kama Raia. Hii ilikuwa kuwa pre empty CCM watakapomfukuza jambo alilofanikiwa kwasababu tayari alishatangaza kustaafu tofauti na kama asingesema.

Kauli ya utumishi wa Umma alimaanisha hataki teuzi tena akijua hatapata tena kwasababu hizo hizo

Kwamba, ataweza kuwa na platform kama Raia jibu ni YES lakini kuna tofauti kati yake na Wazee kama JS Warioba

EN kaondoka kwa ''inda na indhara' kwa maana ya kuvurugana hadi vikao. Kuna kamba barabarani, akijichanganya anajikwaa. Bado hatujui yupo wapi Mwenezi mstaafu wa CCM!

JokaKuu
 
Ndugu Nchimbi kwanza nikupe pongezi nyingi kwa kuondoka kifungoni.

Awali nilitangaza humu kwamba ningefungua masikio yangu yote nisikilize uliyokuwa ukiyaseama baada ya maneno uliyosema kuhusu waTanzania waidai katiba kwa nguvu zao zote..

Maana yangu ya kufungua masikio, nilitaka niwe na uhakika wa hiayo na mengine ambayo ulishayasema yaliyoonekana kuwa tofauti na wenzio; ambao wengi tuliamini mnawafanyia waTanzania ulaghai na maigizo.

Sasa imebainika kuwa yako hayakuwa maigizo, bali ni msimamo uliokuwa ukiuamini. Wengi tukawa tunashangaa utakuwaje na msimamo kama huo halafu ukaendelea kubaki na kushiriki na watu waovu waliokuzunguka kila mahali. Sasa mashaka hayo tumeyaweka pembeni.

Jambo ninalotaka kulizungumzia hapa, na kama ukipenda ulichukue kama ushauri kwako.

Ulisema kwenye barua yako, kwamba unaachana na siasa (umestaafu) na utumishi wa umma.

Sasa hapa itabidi utakapokuwa umetulia vizuri na kutafakari, ufafanue maana yako ya "kustaafu siasa na utumishi wa umma"

Maana inayoniijia kwa haraka haraka ni kuwa hupendi tena kutegemea siasa na utumishi wa umma kuendesha maisha yako kwa mahitaji ya kila siku ya kibinaadam.

Vinginevyo sifahamu mtu anavyoweza kujiondoa moja kwa moja katika utumishi wa taifa lake katika nafasi na hali mbalimbali. Kwa maoni yangu, anayestaafu maswala ya nchi ni yule ambaye amemaliza maisha yake hapa duniani.

Kwa hiyo sioni jinsi utakavyoweza kustaafu; hasa baada ya kujipambanua wazi kuwa wewe na kundi ulilokuwemo hamkuwa pamoja.

Umri bado unakuruhusu, utawezaje kujifunga minyororo huku ukiangalia taifa ulilolitumikia kwa muda mrefu likiangamia; unaweza kweli ukaishi kwa ustaafu wa amani?

Sikushauri ukimbilie kwenye vyama vya upinzani vilivyopo; na hasa hasa CHADEMA. Kaa utulie kwanza, lakini usijiondoe kwenye maswala ya utetezi wa taifa hili kwa kutumia nyenzo mbalimbali zilizopo kulipigania taifa hili.

Kama kulikuwa na wenzako huko ulikokuwa wakikuamini unachosimamia, endelezeni msimamo huo, muujenge, hata kama hamna chama cha kukitumia kwa sasa.
Waungeni mkono bila ya masharti yoyote CHADEMA katika juhudi zao za kuwaunganisha waTanzania waukatae utwana huu wanaoletewa na kundi uliloliyupa mkono.

Huko mbele ya safari, kama juhudi zenu zinaimarika na kudumu, mambo ya wapi mtaelekeza juhudi hizo yatajipambanua yenyewe.

Naomba nikusisitizie tena, huwezi kustaafu huku ukiwa kwenye mateso

Sasa masikio yapo wazi kabisa kusikiliza unayoweza kusema katika ukombozi wa taifa hili.
Andiko maridhawa
 
Kwa haya ya Nchimbi Nina wasiwasi Lissu anaweza asitoke kabisa. Hata kama Hana hatia.
 
Kwamba, ataweza kuwa na platform kama Raia jibu ni YES lakini kuna tofauti kati yake na Wazee kama JS Warioba
Hii natamani ungenifafanulia zaidi.
Pia kwanini hiyo kamba haijamtega na kumuangusha mzee JS Warioba?
 
Ndugu Nchimbi kwanza nikupe pongezi nyingi kwa kuondoka kifungoni.

Awali nilitangaza humu kwamba ningefungua masikio yangu yote nisikilize uliyokuwa ukiyaseama baada ya maneno uliyosema kuhusu waTanzania waidai katiba kwa nguvu zao zote..

Maana yangu ya kufungua masikio, nilitaka niwe na uhakika wa hiayo na mengine ambayo ulishayasema yaliyoonekana kuwa tofauti na wenzio; ambao wengi tuliamini mnawafanyia waTanzania ulaghai na maigizo.

Sasa imebainika kuwa yako hayakuwa maigizo, bali ni msimamo uliokuwa ukiuamini. Wengi tukawa tunashangaa utakuwaje na msimamo kama huo halafu ukaendelea kubaki na kushiriki na watu waovu waliokuzunguka kila mahali. Sasa mashaka hayo tumeyaweka pembeni.

Jambo ninalotaka kulizungumzia hapa, na kama ukipenda ulichukue kama ushauri kwako.

Ulisema kwenye barua yako, kwamba unaachana na siasa (umestaafu) na utumishi wa umma.

Sasa hapa itabidi utakapokuwa umetulia vizuri na kutafakari, ufafanue maana yako ya "kustaafu siasa na utumishi wa umma"

Maana inayoniijia kwa haraka haraka ni kuwa hupendi tena kutegemea siasa na utumishi wa umma kuendesha maisha yako kwa mahitaji ya kila siku ya kibinaadam.

Vinginevyo sifahamu mtu anavyoweza kujiondoa moja kwa moja katika utumishi wa taifa lake katika nafasi na hali mbalimbali. Kwa maoni yangu, anayestaafu maswala ya nchi ni yule ambaye amemaliza maisha yake hapa duniani.

Kwa hiyo sioni jinsi utakavyoweza kustaafu; hasa baada ya kujipambanua wazi kuwa wewe na kundi ulilokuwemo hamkuwa pamoja.

Umri bado unakuruhusu, utawezaje kujifunga minyororo huku ukiangalia taifa ulilolitumikia kwa muda mrefu likiangamia; unaweza kweli ukaishi kwa ustaafu wa amani?

Sikushauri ukimbilie kwenye vyama vya upinzani vilivyopo; na hasa hasa CHADEMA. Kaa utulie kwanza, lakini usijiondoe kwenye maswala ya utetezi wa taifa hili kwa kutumia nyenzo mbalimbali zilizopo kulipigania taifa hili.

Kama kulikuwa na wenzako huko ulikokuwa wakikuamini unachosimamia, endelezeni msimamo huo, muujenge, hata kama hamna chama cha kukitumia kwa sasa.
Waungeni mkono bila ya masharti yoyote CHADEMA katika juhudi zao za kuwaunganisha waTanzania waukatae utwana huu wanaoletewa na kundi uliloliyupa mkono.

Huko mbele ya safari, kama juhudi zenu zinaimarika na kudumu, mambo ya wapi mtaelekeza juhudi hizo yatajipambanua yenyewe.

Naomba nikusisitizie tena, huwezi kustaafu huku ukiwa kwenye mateso

Sasa masikio yapo wazi kabisa kusikiliza unayoweza kusema katika ukombozi wa taifa hili.
Sasa imebainika kuwa yako hayakuwa maigizo, bali ni msimamo uliokuwa ukiuamini. Wengi tukawa tunashangaa utakuwaje na msimamo kama huo halafu ukaendelea kubaki na kushiriki na watu waovu waliokuzunguka kila mahali. Sasa mashaka hayo tumeyaweka pembeni.✍🏿💪🏿
 
Back
Top Bottom