Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

nchimbi anataka apewe moyo wa kumsamehe pinda au kikwete?

pinda: alitaarifiwa na nchimbi mara 2 kuhusu unyama wa operesheni tokomeza lakini alikaa kimya. pia alimshauri rais amfute kazi nchimbi.

kikwete; alimfuta kazi nchimbi

sasa kati ya hawa wawili ni nani ambaye nchimbi anamuomba Mungu ampe huruma ya kumsamehe?
 
Tatizo alikuwa hajui kujifanyia evaluation. Alikuwa hawezi ile wizara kabisa. Na alipojipa PhD ndio kabisa, alifikiri anafaa kuliko ukweli waliokuwa wanaujua wananchi kuhusu yeye. Aendelee kutafakari akiwa kama observer tu.
 
Siku zote siasa ni mchezo wenye rafu nyingi usipoangalia unapigwa kiatu. Namuomba Mungu ampe moyo wa kuomba msamaha na kusamehewa. Ajue kwamba kuna aliowaumiza ktk utawala wake either direct au indirect kwa sababu yeye ni kiongozi hivyo lawama zote tunamtwisha yeye. Mkuu kumbuka kuna uliowaumiza kupitia kauli mbali mbali ulizokua ukizitoa...........

Umenena vema kabisa!

Nchimbi ni kijana mdogo sana aliyekuwa amemelewa madaraka. Alibarikiwa kupata bahati kupata madaraka ya (Ki ungozi) akiwa na umri mdogo. Nazungumzia toka alipokuwa Mwenyekiti wa UVCCM na hatimaye ujumbe wa vikao vizito kwa maamuzi ya taifa kama ujumbe wa NEC/CC mpaka kwenye ngazi ya U Waziri.

Bahati hii imekuwa ikimfanya ajione mtu muhimu sana na mwenye kudiriki kumvaa mtu yeyote na wakati wowote na kwa jinsi anavyojisikia. Kwa kifupi ni mmoja ya vijana waliolewa viburi vya madaraka. Nakumbuka miaka ya nyuma alipata kumvaa na kumkejeli Askofu Kakobe kwa kufananisha na 'Askofu Kibwetere' wa kule Uganda (Pengine wengie mtakuwa bado mnafahamu hadithi ya Askofu Kibwetere wa Uganda🙂

Anyway! Binafsi sijapata kusikia wala kusoma jema kuhusu Nchimbi. Sifa zake kuu ni kiburi, ubabe na ukomoaji. Na pale itakapotokea mkapishana kauli kama vijana au binadamu basi sifa ya kuu ni ufanyiziaji watu kwa kutumia madaraka yake. Namuona ni kijana mwenye nyota yake (kwa kupata uongozi mfululizo miaka yote hii) lakini asiye na busara wala chembe ya maono. Na hii ina kuonyesha ni mtu ambaye hata huo 'ustawi wa kiroho' anaanza kuutafuta au kuutambua wakati huu wa sasa kwa kuomba Mwenyezi Mungu amjalie kumpa moyo wa upendo na kusamehe

Hivyo Nchimbi hakutarajia katika maisha yake kuwa uongozi kwake unaweza ukakoma ghafla (kama kibatari kilichoishiwa mafuta) na katika staili na namna ya yaliompata. Kwake imekuwa ni mtihani mgumu kuukubali. Ile dhana ya kuwa 'uongozi ni dhamana' haikupata kuwepo akilini mwake. Dhamana ya uongozi kwake ilikuwa ni HAKI yake. Hivyo yaliompata kwake bado ni kama njozi ya jinamizi. Sasa anateseka na kuweweseka kama mtoto mchanga aliyepatwa na homa ya dege dege.
 
Huyu jamaa bhana! Hawa ndo wale wema aliosema Makamba kwamba hawafi?
 
Back
Top Bottom