Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

Mipango yote ya kishetani alofanya na mwigulu,mungu akupe upendo upi?ungelikuwa unawapenda wenzako husingeratisha na savimbi wako mauaji ya watanzania
 
Damu ya Ipyana Malecela na watanzania wengine iko juu yako Nchimbi huwezi kukwepa. Wewe ni wa kuhukumiwa na sio kusamehewa, hiyo ya kusamehe labda umsamehe mkeo Tu lakini umeua wengi.

RIP Ally Zona
 
Kwa nini hawaombi aliowakosea wamsamehe?
Huyu sio wa kusamehewa hata akiomba toba, mtoa roho za watu, na majigambo ya kujinga, hivi kwenye kifo cha utata unaweza waanbia Watanzania serikali haitaunda tume kuchunguza kifo???? Yaani walio kufa ni sisimizi wamekanyagwa na kiatu, Nchimbi ni mtu wa hatari sana, asimame tena ujinga wake awaambie wajane na yatima walioachwa na wenzi wao utumbo wake. Na huu ni mwanzo, mengi yatamkuta yeye na kizazi chake.
 
Kama ni gazeti la Tanzania Daima siamini hata kidogo
 
Kama ni gazeti la Tanzania Daima siamini hata kidogo
Ingekuwa gazeti la kufungia vitumbua ( uhuru) ungeamini,???? Sasa hii ni kutoka fb yake, ila issue ya kusema Serikali haitaunda tume kuhusiana na bomu la Soweto aliongea bungeni nami nilimsikia live,
 
Tosabiso abangise mopepe santu nalikolo naipele
botema nangae nono ya Yezu mwana nzambe
CHISTMASE mobili mobimba naitese didii
moningate na losambo ya nkolo nzambe nalobi ya
bon a'nnee'. Motema nayaya tete nangai. Izamote
na mwana Nzambe ya 2014

King Kong III,

Kwanza awali ya yote ningependa unipatie tafsiri ya beti hizi za Kilingala kama sijakosea.

Baada ya kusema hivo sasa naomba nichangie kuhusu thread hii. Emmanuel Nchimbi alistahili hukumu hii ya kuvuliwa wadhifa wa Uwaziri. From the very beggining Nchimbi hakustahili kuwa Waziri kwa vile hana sifa! Nchimbi ni mojawapo ya mawaziri mizigo ndani ya Serikali tangu aanze kuteuliwa kwenye nafasi za Uwaziri. Nakumbuka amewahi kuwa Waziri wa Habari,Michezo na Utamaduni kabla ya kwenda kwenye Uwaziri wa Mambo ya ndani.

Emmanuel Nchimbi alistahili hukumu hii mapema sana. Wengi tunakumbuka jinsi ambavyo alishindwa kusimamia uwajibikaji wa Jeshi lake la Polisi na UWT katika kushughulikia matukio makubwa kabisa yakiwemo ya MABOMU ya Arusha: Olasiti na Soweto. Kwamba mpaka sasa hakuna hata INZI amekamatwa kuhusiana na matukio hayo mabaya ndani ya nchi yetu. Lakini pia kuna matukio ya Kuuawa kwa Mwandishi Daudi Mwangosi, Kutekwa na kuteswa kwa Dr. Ulimboka na Mhariri Absolom Kibanda. Mpaka sasa hakuna hata MENDE aliyefikishwa kwa Pilato kuhusiana na unyama huo! Kuna matukio ya Watu kumwagiwa Tindikali na kuuawa na Polisi kwenye maandamano ya CDM!!!

Kama kweli Nchimbi ni Mkristo wa kweli nasema aache unafiki! Hapo alipo hana cha Moyo wa kusamehe wala lolote! Ni huyu huyu Nchimbi aliyeongea Bungeni kwa KIBRI kabisa kuhusu Bomu la Soweto lililo lipuliwa kwenye Mkutano wa CHADEMA na kuua watu wanne huku likijeruhi kadhaa. Bwana Nchimbi aliwananga CHADEMA kuwa wao ndiyo waliolipua Bomu hilo kwenye Mkutano wao!!!Haya ni matamshi dhaifu na yenye kuudhi kabisa yaliyowahi kutolewa na mtu mwenye dhamana ya Uwaziri!!!

Watu husema malipo ni hapa hapa duniani. Nchimbi asifikiri zile Damu za Watu kwenye Mkutano wa CDM na kule Kanisani Olasiti zilikuwa Damu za kuku! Usicheze na Damu ya Mwanadamu mwenzako hata siku moja. Nchimbi kwa ulevi tu wa madaraka aliweza kutamka ulevi wake huo na kusahahu kabisa kuwa Mungu wa Mbinguni, Jehova tunayemwabudu HAZIHAKIWI hata siku moja. Nchimbi ajue kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuharibikiwa. Zile damu za Watanzania wenzetu zilizomwagwa pasi na hatia kuanzia kwa Mwangosi, Olasiti,Soweto na sasa kwenye Operesheni Komesha Ujangili haziwezi kumwacha salama yeye na hao magaidi wenzake kina Nahodha, Kagasheki, Mathayo, IGP Mwema na CDF Mwamnyange!!

Huwezi ukamwaga damu ya mtu na ukabaki salama. Never. Kama Nchimbi ni msomaji wa Biblia basi asome habari za Kaini ndipo atajua maana ya kumwaga Damu ya mtu asiyeka na hatia.

Wasalaamu.
 
Ana haki ya kusema ya moyoni mwake. Yeye amebeba dhambi za watu wa chini yake ambao hawakuzingatia maadili ya kazi zao. ................................,.,.,, Na pia ana mambo mengi anayoyafahamu ya kitaifa bila kumwita Mungu atashindwa kuendelea kuyameza.
 
King Kong III,

Kwanza awali ya yote ningependa unipatie tafsiri ya beti hizi za Kilingala kama sijakosea.

Baada ya kusema hivo sasa naomba nichangie kuhusu thread hii. Emmanuel Nchimbi alistahili hukumu hii ya kuvuliwa wadhifa wa Uwaziri. From the very beggining Nchimbi hakustahili kuwa Waziri kwa vile hana sifa! Nchimbi ni mojawapo ya mawazir mizigo tangu aanze kuteuliwa kwenye nafasi za Uwaziri. Nakumbuka amewhi kuwa Waziri wa Habari,Michezo na Utamaduni kabla ya kuwa Waziri wa Mambo ya ndani.

Emmanuel Nchimbi alistahili hukumu hii mapema sana. Wengi tunakumbuka jinsi mabavyo alishindwa kusimamia uwajibikaji wa Jeshi la Polisi na UWT katika kushughulikia matukio makubwa kabisa yakiwemo ya MAMBOMU ya Arusha: Olasiti na Soweto. Kwamba mpaka sasa hakuna hata NZI amekamatwa kuhusiana na matukio hayo mabaya katika nchi yetu. lakini pia kuna matukio ya Kuuawa kwa Mwandishi Daudi Mwangosi, Kutekwa na kuteswa kwa Dr. Ulimboka na Mhariri Absolom Kibanda. Mpaka sasa hakuna hata MENDE aliyefikishwa kwa Pilato kuhusiana na unyama huo!

Kama kweli Nchimbi ni Mkristo wa kweli nasema aache unafiki! Hapo alipo hana cha Moyo wa kusamehe wala lolote! Ni huyu huyu Nchimbi aliyeongea Bungeni kwa KIBRI kuhusu Bomu la Soweto lililo lipuliwa kwenye Mkutano wa CHADEMA na kuua watu wanne huku likijeruhi mamia kadhaa. Bwana Nchimbi aliwananga CHADEMA kuwa wao ndiyo waliolipua Bomu hilo kwenye Mkutano wao!!!Haya ni matamshi dhaifu kabisa yaliyowahi kutolewa na mtu mwenye dhamana ya Uwaziri!!!

Watu husema malipo ni hapa hapa duniani. Nchimbi asifikiri zile Damu za Watu kwenye Mkutano wa CDM na Kanisani Olasiti zilikuwa Damu za kuku! Usicheze na Damu ya Mwanadamu mwenzako hata siku moja. Nchimbi kwa ulevi tu wa madaraka aliweza kutamka ulevi wake huo na kusahahu kabisa kuwa Mungu wa Mbinguni, Jehova tunayemwabudu HAZIHAKIWI hata siku moja. Nchimbi ajue kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuharibikiwa. Zile damu za Watanzania wenzetu zilizomwagwa pasi na hatia kuanzia kwa Mwangosi, Olasiti,Soweto na sasa kwenye Operesheni Komesha Ujangili haziwezi kumwacha salama yeye na hao magaidi wenzake kina Nahodha, Kagasheki, Mathayo, IGP Mwema na CDF Mwamnyange!!

Huwezi ukamwaga damu ya mtu na ukabaki salama. Never. Kama Nchimbi ni msomaji wa Biblia basi asome habari za Kaini ndipo atajua maana ya kumwaga Damu ya mtu asiyeka na hatia.

Wasalaamu.

Natamani nikupe LIKE
 
mbona karama ya kusamehe tayari anayo?

si alimpandisha cheo Kamhanda richa ya kumdedisha Mwangosi kule Iringa?

ama??
 
Ana haki ya kusema ya moyoni mwake. Yeye amebeba dhambi za watu wa chini yake ambao hawakuzingatia maadili ya kazi zao. ................................,.,.,, Na pia ana mambo mengi anayoyafahamu ya kitaifa bila kumwita Mungu atashindwa kuendelea kuyameza.

Dada Mamndenyi,

Yeye hajawa Yesu Kristo wa kubeba ati dhambi za watu wa chini yake.

Nini maana ya Kiongozi,nini maana ya kuwa Waziri? Mwl. JK Nyerere alikuwa anasema kuongoza ni kuonyesha njia tena njia iliyo sahihi, maana unaweza kuonyesha njia ya kuwapoteza watu kama wanavofanya Mawaziri wengi wa Serikali ya CCM. Kuna Mbunge mwenzao Kangi Lugola aliwauliza kina Nchimbi na PM wao Pinda kuwa wamepewa magari,ndege na Ving'ora kwa masaa 24 WALIKUWA WAPI WAKATI UOVU HUO UKIFANYWA NA HAO WATU WA CHINI YAO???Walikuwa wapi?? Hivi Uwaziri ni kukaa ofisini na kupulizwa hewa ya kiyoyozi? Je,Uwaziri ni kusaini Vocha na Cheki za Kifisadi?Je,Uwaziri ni Kufungua kuendesha vikao vyenye Posho kila siku? Je, Uwaziri ni kufungua na kufunga semina,Warsha, Makongamano na upuuzi kama huo? Je,Uwaziri ni kuweka mikakati ya kupambana na Wapinzani? Jibu ni BIG NO!

Uwaziri ni zaidi ya hayo.Uwaziri ni Uongozi na siyo Utawala. Tatizo la Tanzania ni kuwa tuna Watawala na siyo Viongozi. Hii ndiyo sababu ya taabu zote hizi. Mawaziri kama viongozi wanatakiwa watoke ofisini waende Mijini,mitaani na Vijijini ili wakaone shida za Watanzania na wazitatue kwa kuwaonyeshe njia za kupita ili kufikia malengo na maendeleo yaliyokusudiwa n yanayotarajiwa.

Nchimbi ni Mtawala na Dikteta ambaye hatakiwi kuwepo kwenye orodha ya viongozi wa nji hii!
 
They say "power corrupts, and absolute power corrupts absolutely". It is after power has been taken away from him that Nchimbi is seeking God's intervention? What a folly, Emmanuel. Repent brother, for all the murders you have committed, may be God will listen.
 
Tosabiso abangise mopepe santu nalikolo naipele
botema nangae nono ya Yezu mwana nzambe
CHISTMASE mobili mobimba naitese didii
moningate na losambo ya nkolo nzambe nalobi ya
bon a'nnee'. Motema nayaya tete nangai. Izamote
na mwana Nzambe ya 2014

Mokili kuku na dhambi!!
 
Mzee umekandamiza sana! Watoto naaamini kabisa hawajui baba yao kama huwa anafanya nini awapo kazini, kwa hiyo laana hiyo hawastahili kutoka kwetu. Ni MUNGU tu anayeweza kutoa laana ya namna hiyo, maana asema nawapatiliza wana makosa ya baba zao na hata kizazi cha nne cha wanichukizao!

Mkuu Biblia ambayo JAHILI Emmanuel Nchimbi aliapa nayo inasema LAANA HUTAFUNA KIZAZI CHA KWANZA HADI CHA NNE cha wamchukizao Mungu..
 
Back
Top Bottom