Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

Apewe moyo wa kutubu kwa watanzania kwanza,maana yawezekana ni waziri aliyemwaga damu za watanzania wengi wasio na hatia kuliko yeyote.
 
“Kama Mwenyezi Mungu angeniuliza ni kitu gani anipatie kwa muda huu, ningemuomba anipatie moyo wa upendo na kusamehe,”

Haya ni maneno mazito sana kutamkwa na mwanadamu, ila kwa kiasi fulani yanatupa picha kumtambua ni nani Emmanuel Nchimbi.

Kwa maneno ya kinywa chake anakiri kuwa Mungu ampe moyo wa UPENDO na KUSAMEHE.

Swali dogo tujiulize kwa nini mtu huyu anahitaji hayo mambo mawili, jibu ni moja tu ni kwamba HANA HUO MOYO.

Mwanadamu asiye na moyo wa Upendo na Kusamehe maana yake ana moyo wa Chuki na Kulipiza kisasi, na kwa lugha nyingine Bw Nchimbi alikuwa anajaribu kutueleza kuwa yeye moyoni kwake kumejaa chuki na kisasi.

Nchimbi kaa pembeni, sisi Watanzania hatuhitaji viongozi wa aina yako, wenye kudhani kuwa madaraka ni MALI.

Sisi tunahitaji viongozi wanaotambua kuwa KUWAJIBIKA ni sehemu ya uongozi safi, ulipewa dhamana na sasa imechukuliwa.
 
Na wewe Leo ni wa kusema haya!!, Team Membe utawajua tu kila Mtu wana wasiwasi nae Endelea na chuki zako ukimaliza urudi ukajenge chama

Chama kiko imara na hii ni mishale tu ya kisiasa na ishaanza kuchomolewa na itachomolewa mingine.
 
R.I.P Dr. Mvungi

R.I.P. Watanzania mliopoteza maisha yenu kwa kisingizio cha oparesheni tokomeza ujangili, pamoja na ushahidi wa Meli ya Kinana kukutwa na pembe za Ndovu Nchibi alimtetea Kinana Bungeni. Lakini watz. musio na hatia mmeuwawa nchi hii ina maonezi sana inatutia Uchungu kuiishi.
 
Angemuomba Mungu amsamehe kwa damu za watu wasio na hatia zilizomwagika kwa makusudio yake na watendaji wa wizara yake Arusha, Moro, Iringa, na bla kujali akawapandisha wauaji cheo.
Damu za wstu hao zitamtesa yeye na kizazi chake chote milele amen.

Mzee umekandamiza sana! Watoto naaamini kabisa hawajui baba yao kama huwa anafanya nini awapo kazini, kwa hiyo laana hiyo hawastahili kutoka kwetu. Ni MUNGU tu anayeweza kutoa laana ya namna hiyo, maana asema nawapatiliza wana makosa ya baba zao na hata kizazi cha nne cha wanichukizao!
 
Hana jipya wizara aliyopewa kashindwa kuisimamia itakiwavyo na kinyume chake amekuwa akilihujumu na taifa na serikali ya JK sijui ninani kamtuma? Mungu hatomuacha kila mnafiki salama.

Dunia ina maajabu sana aisee binadamu hawa aminiki hawa watakupenda ukiwa na cheo tu......
 
damu za watu uliowauwa loasti Arusha, soweto,, mwagosi zinakulilia....

Niki kumbuka jamaa nchimbi alicho wafanyia ndugu zangu watu wa mtwara aisee,sema tu nashindwa kumiliki mguu wa kuku.....
 
Duh, jamaa Ana roho ngumu sana badala ya kuomba asamehewe kwa ukatili Mkubwa alioufanya kwa binadamu Na wengine kuuawa kwa amri zake anaomba apewe moyo kwa kusamehe? Kwani yeye ametendewa nini Kibaya, Au kuondolewa uwaziri!
 
SIKU chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kuvuliwa wadhifa wake kwa tuhuma za kushindwa kusimamia wizara yake, kiongozi huyo ametaka apewe moyo wa upendo na kusamehe.

Nchimbi ambaye ni mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya CCM, alisema hayo juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook, wakati akisherehekea kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa.

“Kama Mwenyezi Mungu angeniuliza ni kitu gani anipatie kwa muda huu, ningemuomba anipatie moyo wa upendo na kusamehe,” aliandika.

Mawaziri wengine waliovuliwa nyadhifa zao pamoja na Nchimbi, ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

“Sasa nina miaka 42, namshukuru Mungu kwa kunibariki na kunisaidia kwa kipindi cha mwaka mzima, nawashukuru wazazi wangu, kaka, dada na marafiki zangu, pia ninawashukuru waajiri wangu watu wa Jimbo la Songea na Watanzania wote.

“Ninaukubali upendo wenu na kuniunga mkono…Kama Mungu ataniuliza leo kitu gani anipatie jibu langu litakuwa rahisi, nitamwambia Mungu wangu naomba moyo wa upendo kwa kila mmoja, moyo wa kumsamehe kila mmoja pasipo kujali nini nitarudishiwa, anipe moyo wa kuwatumikia watu kwa saa 24 kwa siku,” alisema Dk. Nchimbi.

Dk. Nchimbi na wenzake wanne walienguliwa madarakani baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao mara baada ya kupewa taarifa za wabunge kuwashinikiza mawaziri hao wajiuzulu kwa sababu ya yaliyojitokeza katika Operesheni Tokomeza Ujangili.

Kuondolewa kwa mawaziri hao kulitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, kuwasilisha taarifa ya kamati yake iliyobainisha unyama mkubwa waliotendewa wananchi katika operesheni hiyo.

Operesheni hiyo ilikuwa ikizihusisha wizara za mawaziri hao waliong’olewa ambapo inadaiwa watendaji waliokuwa wakiiendesha waliua watu, kujeruhi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo mifugo.

Matukio mengine yaliyobainika kwenye operesheni hiyo ni wanawake kubakwa na wengine wakilazimishwa kufanya mapenzi na mama, wakwe au watoto wao.

Source : Tanzania Daima – Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

My Take
Bado nafikiria ni kwanini Nchimbi anaomba apewea Moyo wa Kusamehe , tena kwenye siku yake ya kuzaliwa, ina Maana amekosewa sana huyu Bwana !!!!
ati amekosewa? Mwangosi alivyopigwa bomu hakumbuki anatakiwa kuomba toba kwa vile ni askari wake ndo alifanya ushenzi huo? Aache unafiki!
 
Hahaa nchimbi bana nakumbuka ulivoninyang'anya demu wangu mwanza...yaani uwaziri ulikufanya ukawaweka wanawake wa4 vyumba tofauti pale lakairo unagegeda kika mmoja kwa muda wake bila wao kujuana?hahaa wewe jabali aisee

We! We! We! We!we!!!!! Yaani huku watu wanapigwa; mama zetu wanabakwa; wengine wanasokomezwa vyupa private area zao, na wanaume wanaambiwa waiingilie miti yeye amewapanga wanawake hotelini anatusua tu! Hivi anatumia viagra huyu? Wanne si mchezo inataka moyo wa kujituma na si moyo wa MSAMAHA, Nchimbi we kibogo kweli wanne!!!! Tafadhali ebu jitokeze kujibu tuhuma hizi kiongozi hazifai kupita bila kauli yako, UKWELI UTAKUWEKA HURU KWELI KWELI.
 
SIKU chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kuvuliwa wadhifa wake kwa tuhuma za kushindwa kusimamia wizara yake, kiongozi huyo ametaka apewe moyo wa upendo na kusamehe.

Nchimbi ambaye ni mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya CCM, alisema hayo juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook, wakati akisherehekea kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa.

“Kama Mwenyezi Mungu angeniuliza ni kitu gani anipatie kwa muda huu, ningemuomba anipatie moyo wa upendo na kusamehe,” aliandika.

Mawaziri wengine waliovuliwa nyadhifa zao pamoja na Nchimbi, ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

“Sasa nina miaka 42, namshukuru Mungu kwa kunibariki na kunisaidia kwa kipindi cha mwaka mzima, nawashukuru wazazi wangu, kaka, dada na marafiki zangu, pia ninawashukuru waajiri wangu watu wa Jimbo la Songea na Watanzania wote.

“Ninaukubali upendo wenu na kuniunga mkono…Kama Mungu ataniuliza leo kitu gani anipatie jibu langu litakuwa rahisi, nitamwambia Mungu wangu naomba moyo wa upendo kwa kila mmoja, moyo wa kumsamehe kila mmoja pasipo kujali nini nitarudishiwa, anipe moyo wa kuwatumikia watu kwa saa 24 kwa siku,” alisema Dk. Nchimbi.

Dk. Nchimbi na wenzake wanne walienguliwa madarakani baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao mara baada ya kupewa taarifa za wabunge kuwashinikiza mawaziri hao wajiuzulu kwa sababu ya yaliyojitokeza katika Operesheni Tokomeza Ujangili.

Kuondolewa kwa mawaziri hao kulitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, kuwasilisha taarifa ya kamati yake iliyobainisha unyama mkubwa waliotendewa wananchi katika operesheni hiyo.

Operesheni hiyo ilikuwa ikizihusisha wizara za mawaziri hao waliong’olewa ambapo inadaiwa watendaji waliokuwa wakiiendesha waliua watu, kujeruhi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo mifugo.

Matukio mengine yaliyobainika kwenye operesheni hiyo ni wanawake kubakwa na wengine wakilazimishwa kufanya mapenzi na mama, wakwe au watoto wao.

Source : Tanzania Daima – Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

My Take
Bado nafikiria ni kwanini Nchimbi anaomba apewea Moyo wa Kusamehe , tena kwenye siku yake ya kuzaliwa, ina Maana amekosewa sana huyu Bwana !!!!

Kumbe inauma? Kuachishwa kazi tu unahaha je ungehukumiwa kifo?? Sema yote kwanza ndipo upewe moyo wa kusamehe toba nzuri ni uombe kwa uliowakosea kwanza kaka umeskia??!
 
Kumbe inauma? Kuachishwa kazi tu unahaha je ungehukumiwa kifo?? Sema yote kwanza ndipo upewe moyo wa kusamehe toba nzuri ni uombe kwa uliowakosea kwanza kaka umeskia??!
Nchimbi ndiye huyu huyu aliekuwa anaintelejensi ya mikutano ya Chadematu.
 
Mimi nadhan angeomba apewe moyo wa ujasiri kuweza kuwaomba msamaha watz wote walioguswa na kuathirika na operesheni tokomeza ................
 
Back
Top Bottom