Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Malipo hapahapa duniani!
Tosabiso abangise mopepe santu nalikolo naipele
botema nangae nono ya Yezu mwana nzambe
CHISTMASE mobili mobimba naitese didii
moningate na losambo ya nkolo nzambe nalobi ya
bon a'nnee'. Motema nayaya tete nangai. Izamote
na mwana Nzambe ya 2014
SIKU chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kuvuliwa wadhifa wake kwa tuhuma za kushindwa kusimamia wizara yake, kiongozi huyo ametaka apewe moyo wa upendo na kusamehe. Nchimbi ambaye ni mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya CCM, alisema hayo juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook, wakati akisherehekea kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa.
Kama Mwenyezi Mungu angeniuliza ni kitu gani anipatie kwa muda huu, ningemuomba anipatie moyo wa upendo na kusamehe, aliandika.
Mawaziri wengine waliovuliwa nyadhifa zao pamoja na Nchimbi, ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
Sasa nina miaka 42, namshukuru Mungu kwa kunibariki na kunisaidia kwa kipindi cha mwaka mzima, nawashukuru wazazi wangu, kaka, dada na marafiki zangu, pia ninawashukuru waajiri wangu watu wa Jimbo la Songea na Watanzania wote.
Ninaukubali upendo wenu na kuniunga mkono Kama Mungu ataniuliza leo kitu gani anipatie jibu langu litakuwa rahisi, nitamwambia Mungu wangu naomba moyo wa upendo kwa kila mmoja, moyo wa kumsamehe kila mmoja pasipo kujali nini nitarudishiwa, anipe moyo wa kuwatumikia watu kwa saa 24 kwa siku, alisema Dk. Nchimbi.
Dk. Nchimbi na wenzake wanne walienguliwa madarakani baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao mara baada ya kupewa taarifa za wabunge kuwashinikiza mawaziri hao wajiuzulu kwa sababu ya yaliyojitokeza katika Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kuondolewa kwa mawaziri hao kulitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, kuwasilisha taarifa ya kamati yake iliyobainisha unyama mkubwa waliotendewa wananchi katika operesheni hiyo.
Operesheni hiyo ilikuwa ikizihusisha wizara za mawaziri hao waliongolewa ambapo inadaiwa watendaji waliokuwa wakiiendesha waliua watu, kujeruhi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo mifugo.
Matukio mengine yaliyobainika kwenye operesheni hiyo ni wanawake kubakwa na wengine wakilazimishwa kufanya mapenzi na mama, wakwe au watoto wao.
Source : Tanzania Daima Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe
My Take
Bado nafikiria ni kwanini Nchimbi anaomba apewea Moyo wa Kusamehe , tena kwenye siku yake ya kuzaliwa, ina Maana amekosewa sana huyu Bwana !!!!
Kama Nchimbi anaomba moyo wa upendo na kusamehe yafaa angetafakari ya fuatayo:
1.Angefanya nini kama yule mwanamke aliye uawa kama angekuwa ni dada yake au mama yake?
2.Angefanya nini kama wale watoto waliokuwa wakimtegemea mama yao sasa wamebaki wapweke ndiyo angekuwa ni yeye?
3.Angefanya nini kama yule mama aliyeingizwa chupa ya soda ukeni na njia ya haja kubwa kama ange kuwa ni mama yake,shangazi yake au dada yake?
4.Angefanyaje kama yule mheshimiwa aliyeambiwa afanye mapenzi na mti kama angekuwa ni baba yake au kaka yake?
5.Angefanyaje kama wale wanawake waliobakwa kwa zamu kama wangelikuwa ni shangazi zake au mama zake?
Kwa maoni yangu:
Baada ya kupata taarifa zile kama waziri alitakiwa kuwaomba radhi watanzania kupitia vyombo vya habari kutokana na vitendo hivyo vya kinyama vilivyotokea katika wizara iliyochini yake ili watanzania ndiyo waone kama wanaweza kumsamehe au laa kuliko kujiona kama yeye ndiyo kaonewa.[/FONT][/SIZE][/I]