Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

Angemuomba Mungu amsamehe kwa damu za watu wasio na hatia zilizomwagika kwa makusudio yake na watendaji wa wizara yake Arusha, Moro, Iringa, na bla kujali akawapandisha wauaji cheo.
Damu za wstu hao zitamtesa yeye na kizazi chake chote milele amen.

Kwa nini hawaombi aliowakosea wamsamehe?
 
Tosabiso abangise mopepe santu nalikolo naipele
botema nangae nono ya Yezu mwana nzambe
CHISTMASE mobili mobimba naitese didii
moningate na losambo ya nkolo nzambe nalobi ya
bon a'nnee'. Motema nayaya tete nangai. Izamote
na mwana Nzambe ya 2014

Mkuu tafsiri basi kwa kiswahili
 
Dunia ina maajabu sana aisee binadamu hawa aminiki hawa watakupenda ukiwa na cheo tu......

Sio kweli. Nchimbi kaleta zahma nyingi sana akiwa kama Wazir wa mambo ya ndani na kupelekea serikali kulalamikiwa sana. Huyu kaaminiwa na rais na wananchi lakini he discouraged his supporters. Si kwamba uwezo hana bali kuna kitu nyuma ya pazia. "Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo".
 
Mungu yupi anayemwabudu NCHIMBI ? Maana ametenda karibu yote yaliyokatazwa na mungu .
 
sio kweli. Nchimbi kaleta zahma nyingi sana akiwa kama wazir wa mambo ya ndani na kupelekea serikali kulalamikiwa sana. Huyu kaaminiwa na rais na wananchi lakini he discouraged his supporters. Si kwamba uwezo hana bali kuna kitu nyuma ya pazia. "tanzania ni zaidi ya tuijuavyo".

hana uwezo full stop , hayo mengine unapaka rangi tu .
 
un-thankful baboon.
So He doesn't thank JK for all the authority He gave him despite his grave in-competencies??
 
Mwenyezi Mungu atajua adhabu ya kumpa Nchimbi kwa damu za watu ambao amewaua
 
Sasa nchimbi na wenzake wameondolewa, operation uhai mbona haiendelei? Hii kweli si changa la uso kuwanusuru majangili kuendelea na hujuma yao!
 
SIKU chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kuvuliwa wadhifa wake kwa tuhuma za kushindwa kusimamia wizara yake, kiongozi huyo ametaka apewe moyo wa upendo na kusamehe.

Nchimbi ambaye ni mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya CCM, alisema hayo juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook, wakati akisherehekea kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa.

“Kama Mwenyezi Mungu angeniuliza ni kitu gani anipatie kwa muda huu, ningemuomba anipatie moyo wa upendo na kusamehe,” aliandika.

Mawaziri wengine waliovuliwa nyadhifa zao pamoja na Nchimbi, ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

“Sasa nina miaka 42, namshukuru Mungu kwa kunibariki na kunisaidia kwa kipindi cha mwaka mzima, nawashukuru wazazi wangu, kaka, dada na marafiki zangu, pia ninawashukuru waajiri wangu watu wa Jimbo la Songea na Watanzania wote.

“Ninaukubali upendo wenu na kuniunga mkono…Kama Mungu ataniuliza leo kitu gani anipatie jibu langu litakuwa rahisi, nitamwambia Mungu wangu naomba moyo wa upendo kwa kila mmoja, moyo wa kumsamehe kila mmoja pasipo kujali nini nitarudishiwa, anipe moyo wa kuwatumikia watu kwa saa 24 kwa siku,” alisema Dk. Nchimbi.

Dk. Nchimbi na wenzake wanne walienguliwa madarakani baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao mara baada ya kupewa taarifa za wabunge kuwashinikiza mawaziri hao wajiuzulu kwa sababu ya yaliyojitokeza katika Operesheni Tokomeza Ujangili.

Kuondolewa kwa mawaziri hao kulitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, kuwasilisha taarifa ya kamati yake iliyobainisha unyama mkubwa waliotendewa wananchi katika operesheni hiyo.

Operesheni hiyo ilikuwa ikizihusisha wizara za mawaziri hao waliong’olewa ambapo inadaiwa watendaji waliokuwa wakiiendesha waliua watu, kujeruhi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo mifugo.

Matukio mengine yaliyobainika kwenye operesheni hiyo ni wanawake kubakwa na wengine wakilazimishwa kufanya mapenzi na mama, wakwe au watoto wao.

Source : Tanzania Daima – Nchimbi: Mungu nipe moyo wa kusamehe

My Take
Bado nafikiria ni kwanini Nchimbi anaomba apewea Moyo wa Kusamehe , tena kwenye siku yake ya kuzaliwa, ina Maana amekosewa sana huyu Bwana !!!!
Hili jamaa jinga kweli badala ya kuomba msamaha linataka kusamehe!! Amina Chifupa anakuangalia wewe hasidi!!
 
Wakuu, hii anamaanisha kuwa uwapo madarakani (serikalini) moyo wa kusamehe unakuwa hauna wa huna nafasi (huruhusiwi) ya kumuomba Mungu akupe huo moyo wa kusemehe? Labda ndio maana babu Seya hatoki!
 
Tosabiso abangise mopepe santu nalikolo naipele
botema nangae nono ya Yezu mwana nzambe
CHISTMASE mobili mobimba naitese didii
moningate na losambo ya nkolo nzambe nalobi ya
bon a'nnee'. Motema nayaya tete nangai. Izamote
na mwana Nzambe ya 2014
Tata Nzambe yoka losambo.
 
Tosabiso abangise mopepe santu nalikolo naipele
botema nangae nono ya Yezu mwana nzambe
CHISTMASE mobili mobimba naitese didii
moningate na losambo ya nkolo nzambe nalobi ya
bon a'nnee'. Motema nayaya tete nangai. Izamote
na mwana Nzambe ya 2014

mkuu umeniacha mwandiga kigoma,hebu tafsir mkuu.
 
Sio kweli. Nchimbi kaleta zahma nyingi sana akiwa kama Wazir wa mambo ya ndani na kupelekea serikali kulalamikiwa sana. Huyu kaaminiwa na rais na wananchi lakini he discouraged his supporters. Si kwamba uwezo hana bali kuna kitu nyuma ya pazia. "Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo".

CHAMVIGA
Inasemekana pia makashfa ya unga yanayoikumba nchi huyu jamaa ni mhusika mkuu........
 
Last edited by a moderator:
machozi ya binti aliyebakwa na KAPUYA hayataenda bure, ipo siku nawewe binti yako, mkeo au mama ako mzazi atabakwa ndo ujue uchungu wa kubakwa na kushindwa kumchukulia hatua huyo bazazi
 
Back
Top Bottom