tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Mambo ya leo ni mengi. Alichokifanya bwana Nchimbi kutangaza "kujiuzulu" umakamu wa rais ni zaidi ya uhaini. Nasema haya kwa sababu anuai.
Kwanza, kitendo cha kukubali kuachia nafasi yake baada ya kushinikizwa na wanaCCM mtandao, kinaashiria jinsi alivyo muoga kama kunguru, tofauti na watu wengine wanavyompamba na kumuona kama shujaa. Huyu jamaa sio shukaa bali ni mnafiq na muoga kama walivyo waoga wengine. Kama kweli Nchimbi ni mwanaume rijali, alipaswa kukomaa. Sio kuachia madaraka kirahisi rahisi kama alivyofanya. Kuachia madaraka kirahisi baada ya shinikizo dogo tu kutoka kwa wanamtandao, kutawapa kiki sana Msoga gang & Co. Sasa wataanza kuitafuna nchi kama mchwa na kuna tetesi Ridhiwani Kikwete ndiye anapigiwa chapuo kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Sasa manyang'au wataanza kuitafuna nchi hadi mfupa wa mwisho.
Nchimbi angekuwa jasiri, angepigana vita akiwa humo humo ndani hadi afukuzwe, kama alivyofanya Rigath Gachagua kule Kenya. Lakini, kinyume na matarajio ya wengi, amekubali kuwa kunguru muoga amekimbiza mbawa zake na kuwaachia mafisi waendelee kuitafuna nchi bila uwoga. Afadhali alipokuwa anaunguruma akiwa jikoni, mafisi walikuwa wanaogopa kuchukua minofu yote. Baada ya kuondoka sasa tutarajie mafisi kula hadi mzani. Na tusisahau wazungu wamemnyima misaada Samuya na genge lake. Kuanzia sasa, hicho kidogo kinachopatikana kutokana na vyanzo vya ndani kitakuwa kinapitiwa na mafisi kama upepo.
Pili, kwa mujibu wa katiba, Nchimbi anahesabika kama Makamu wa Rais mstaafu. Kwa maana hiyo, yeye na mwenza wake wataendelea kulipwa 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais aliyepo madarakani. Aidha, serikali itamjengea nyumba, kumpa walinzi, mafuta, madereva, wapishi, nk. Kwa ufupi, ataendelea kuenjoy maisha kama Makamu wa Rais. Na haya yote yanagharamiwa na kodi za wanachi maskini wanaokula mlo mmoja baada ya siku 2. Kwa mukdhata huu, mtu yeyote makini na mwenye akili zilizotimia, hawezi kushangilia kujiuzuru kwa Nchimbi kwani kitendo alichofanya ni mzigo kwa taifa na walipakodi wa nchi hii. Kwa maana nyingine, Nchimbi ameamua kuwa mtumishi hewa kwa kuamua kukaa pembeni huku akiendelea kula bata 80% ya Makamu wa Rais mpya atakayeteuliwa. Huu ni zaidi ya uhaini. Watu wanalia kila siku kuhusu uhaini ambao hauwaumizi wanaacha uhaini wa Nchimbi utakaowachakaza kiuchumi moja kwa moja.
Hii nchi ina wananchi wenye akili za kinyumbu sana. Tazama Tundu Lissu anataabishwa kwa zaidi ya mwaka gerezani kwa uhaini wa mchongo huku wananchi hao hao wakishangilia uhaini wa Nchimbi na kumuona shujaa! Ama kweli ni bora mtu ukose mali upate akili. Watanzania ni nani aliyewaroga?
Tatu, kitendo cha kujiuzulu kwa Nchimbi kitawasahaulisha wananchi mambo muhimu yanayoendelea hapa nchini. Kwa mfano, ghafla bin vuu kesi ya uhaini wa mchongo wa Tundu Lissu sasa imepoteza mashiko. Sasa hivi watu wote wamehamia kwa Nchimbi. Yaani watu tunaacha kufuatilia mambo ya msingi yenye umuhimu wa kitaifa tunafuatulia tamthlia za CCM za "kujiuzuru" kwa Nchimbi. Na sio tu kwamba CCM wametupoteza maboya kwa hii tamthlia bali watatumia mwanya huu kuiba fedha za umma na kuzitorosha nje ya nchi kwa manufaa yao na vizazi vyao. Huu sasa ndio uhaini halisi.
MAONI YANGU
Nitamuona Nchimbi shujaa ikiwa ataendelea na msimamo wake ule ule wa kudai Katiba Mpya. Polepole alipojiuzulu aliendelea na msimamo wake hadi walipomuua. Naye anapaswa kusimamia msimamo wake bila kujali chochote, hata ikibidi auawe kama Polepole alivyouawa. Akifanya hivyo atakuwa shujaa wa taifa na kila mtanzania atamkumbuka kwa ushujaa wake.
Nawasilisha.