Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Suala si kuonekana shujaa.Sasa unashauri nini kifanyike au angepaswa kufanya nini ili aonekane shujaa?
Suala ni kuwa na misingi na kuisimamia.
Wanasiasa wetu hawana peinciple, wanayumbishwa na upepo.
Angeamua akae kwenye lane moja bila logical inconsistency.
Angekubali kuwa fisadi anayekubaliana na wauaji awe chawa wa Samia tu, tungemuelewa yupo upande huo. Tusingekubaliana naye, lakini tungemuelewa. Angalau angekuwa logically consistent. Hawa machawa wapo wengi, wengine wametoka mpaka upinzani kina Kitila. Wamechagua upande, tunawaelewa wamesimamia wapi.
Ama, angechagua kushikilia agenda yake ya katiba mpya na kuwa the sane person in the room, angekataa kujiuzulu, hakuna wa kumlazimisha kujiuzulu bila impeachment process. Na huko kwenye impeachment angemwaga madudu yote.
Tungemuelewa.
Sasa hivi kawa kama mtaka yote hukosa yote.
Kule kwenye mafisadi wauaji kawasaliti, na huku kwenye wanaharakati wanaotaka mageuzi nako kawasaliti.
Imekuwa kama ule wimbo wa Ali Kiba wa Mwana.