Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
NDAISABA RUHORO AKICHANGIA HOTUBA YA BAJETI KUU YA SERIKALI YA WIZARA YA KILIMO, BUNGENI JIJINI DODOMA
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro tarehe 21 Mei, 20245 amechangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Wizara ya Kilimo ambapo amempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde juu ya mabadiliko ya bajeti ya Kilimo kutoka Bajeti ya shilingi Bilioni 297 mpaka Bajeti ya shilingi Trilioni 1.2.
Ndaisaba George Ruhoro ameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mabadiliko ya bei ya Kahawa kati ya mwaka 2021 mpaka 2025 kwani limekuwa na mabadiliko makubwa ambayo hayakudhamiliwa kutokea hasa kwa Jimbo la Ngara kutoka 1200 mpaka 6700 kwa Kahawa ya Robosta.
Ndaisaba George Ruhoro ameipongeza Serikali kwa maboresho ya mfumo wa mauzo uliofuta tozo 49 na kubakiza tozo 7 ambazo anatakiwa kulipa mfanyabiashara na siyo Mkulima.
Aidha, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amewasilisha maombi kadhaa kwa Wizara ya Kilimo kupitia michango yake katika uwasilishaji wa bajeti ya Wizara hiyo ambayo ni pamoja na:-
1. NFRA kutimiza ahadi yao ya kuja Ngara na kuanzisha vituo vya ununuzi wa nafaka ikiwemo Mahindi ili kuweka uwiano bora wa manunuzi ya mahindi na nafaka nyingine
2. Wizara ya Kilimo kuanzisha Mfumo wa Ruzuku itakayosaidia Kilimo Cha umwagiliaji kwa mkulima wa Kahawa ambae hukabiliwa na wadudu wanaoadhiri mizizi ya Kahawa msimu wa Kiangazi.
3. Uimarishaji na uboreshaji wa Vitalu vya Kahawa ambapo kati ya mwaka 2025-2030 wananchi wa Ngara watakuwa na uhitaji wa Miche ya kahawa milioni10 na Mbunge RUHORO ameomba Wizara kuanzisha Vitalu vya miche ya Parachichi pembeni mwa kila kitalu Cha miche ya Kahawa.
4. Ujenzi wa Masoko ya Kimkakati likiwemo Soko la Nzaza Kabanga linalosimamiwa na Wizara ya Kilimo Moja kwa moja kuwe na mfumo bora wa uendeshaji wa ujenzi ili kuwasaidia wasimamizi wa ndani ya Halmashauri na Mamlaka za Mkoa na kuharakisha ujenzi huo.