"Ndani ya mwaka mmoja ailetea Tanzania zaidi ya trillion 43"
Ikiwa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kushika atamu, kumekuwepo na mijadara inayozungumzia juu ya mwenendo wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kusafiri ng'ambo tofauti za nje ya nchi ikilinganishwa na ziara afanyazo ndani ya nchi ikiwa ni tofauti na mtangulizi wake hayati Magufuli. Mijadara mingi sana imekuwa ikiendeshwa katika mitaa na mitandao ya kijamii kuhusu safari hizi afanyazo Mhe Rais.
4 July 2022 akiwa katika utiaji saini wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) Katika hotuba yake alisema kuwa;
"Wenye akili za kawaida ni rahisi kulaumu, Rais anasafiri tu hakai. Badala ya kutembelea mikoa anatembelea tu nje, lakini matokeo yake ndiyo haya. Nikienda mkoani tunajenga siasa ya ndani, hakuna maendeleo. Nikienda nje nakwenda kutafuta fedha kwa ajili ya maendeleo"-Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.
Ukweli ni kwamba usio lijua ni sawa na usiku wa giza, wengi wao wamekuwa wakikosoa ziara hizo pasipo kujua ni matunda gani kama taifa tunafaidika kutokana na ziara hizo, pengine ni kutokuwa na ufatiliaji wa kutosha au lah!
Sasa nikujuze ni hii ambayo itakushangaza sana, unajua ziara hizo afanyazo Mhe raisi zimeitengezea nchi ya Tanzania zaidi ya trillioni 40? Haya yamesemwa na Katibu Mkuu Uwekezaji
" Katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa ya awamu ya sita, Economic Diplomacy imeweza kuingiza katika mfumo wetu wa uchumi dola bilioni 19, hizo huwezi kuzipata popote katika mfumo mwingine'- Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Prof. Godius Kahyarara.
Ikiwa ni Uwekezaji wa ndani dola bilioni 9 ambazo ni sawa na trillioni 20, pamoja na mauzo ya nje ni dola bilioni 10 ambazo ni sawa na trillioni 23.
Hayo ndiyo matunda ya ziara afanyazo Mhe Rais Samia Suluhu Hassan!