Ndani ya mwaka mmoja Rais Samia ailetea Tanzania zaidi ya trillion 43

Vigezo na Masharti vizingatiwe Ili kuzuia watu wa namna hii kuanzisha thread.

Ni aibu kuwa na hoja za namna hii jukwaani tena la Intelligence!!!!
 
Hizo 43T kwa ni za bure au mikopo? Hata hivyo ziko wapi mbona hatuzioni? Umeme shida, maji shida, barabara ni mashimo, mfumuko wa bei uko juu, hali ya maisha ya Mtanzania ni magumu halafu mnalete propaganda zenu hapa
 
Awalipe basi wastaafu malimbikizo yao.

Mifuko ya hifadhi ya jamii inapumlia mashine na hawapeleki pesa walichofanya ni kupunguza lumpsum kwa wale wa PSSSF ambao ndiyo wengi.
 
Hakuna njia rahisi ya kuleta maendeleo, vyovyote atakavyofanya lazima kuna upande utalalamika. Afanye anavyoona yeye inafaa nchi kuendeshwa.

..nadhani wasifiaji wange-concentrate kupigia chapuo miradi ya maendeleo ambayo Raisi anaikamilisha.

..kupigia chapuo fedha za mikopo, au ahadi za uwekezaji, sio sahihi kwasababu hakuna uhakika kama matumizi ya mikopo, au uwekezaji unaotarajiwa, utatuletea matokeo mazuri.

..awamu iliyopita walisifia na kuwajaza waTz matumaini makubwa kuhusu miradi ya Sgr na Stieglers gorge. Yale matumaini makubwa kupita kiasi ndiyo yanayowapa serikali wakati mgumu kuelezea changamoto, na hali halisi ktk miradi hiyo.

..Tujenge na utamaduni wa kuelezana UKWELI kuhusu utendaji wa serikali yetu.
 
Asante kwa kutujulisha.Wananchi tunamuunga mkono.
 
2025 kutakua na kazi sana kushawishi raia hiyo mikopo +tozo+ kodi kama maendeleo yaliyofanyia hayatoonekana,,,mana wapinzani wake hawatotumia nguvu kubwa,,,,tumuombee tu ikamilike hiyo miradi aliyopanga kufanyia na hizo hela!!!
 
Machawa mna shida sana dunia hii.. rais kutembeza bakuli wakati nchi yetu imejaa mali za kutisha ni aibu sana.. Kuwa na rais wa kimichongo ndiyo hasara yake maana hana mbinu wala maarifa ya tunatokaje tulipokwamia. Mtu anawazia kutembeza bakuli tu.. 'tutaolewa' muda si mrefu

Mleta hoja ndiye kituko zaidi kwa sababu hizo trln 43 hazioneshi matokeo yoyote.. mlipuko wa bei za bidhaa, gharama za maisha ziko juu sana halafu chawa zinasifia..
 
Kuwa na dhahabu ardhini bila kuwa na Elimu na mtaji na vitendea KAZI, dhahabu hiyo inakuwa kama mawe mengine tu ya kawaida.

Serikali iboreshe ELIMU inayoendana na raslimali zilizopi Hasa Kwa wilaya zenye raslimali hizo.

Ameeen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…