Ndege tatu za Marekani zatunguliwa kimakosa na Kuwait

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Kamandi la Jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema Machi 2, 2026 kuwa mfumo wa ulinzi wa anga wa Kuwait kwa bahati mbaya ulitungua ndege tatu za kivita za Marekani ikiwa vita dhidi ya Iran na Israel na Marekani ikiendelea.

Kwenye taarifa yao, CENTCOM imesema: "Saa 5:03 usiku Machi 1, 2026 ndege tatu aina ya F-15E zilizokuwa kwenye operesheni zilianguka nchini Kuwait kutokana na kushambuliwa kimakosa na washirika. Wakati wa mapigano makali yaliyohusisha makombora na drones za Iran, ndege hizo za Marekani zilitunguliwa kimakosa na ulinzi wa anga wa Kuwait."

Sasa ukweli wote upo wazi! Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imethibitisha kwamba zile ndege zao tatu hazikuanguka tu kama ilivyodaiwa mwanzo, bali zilitunguliwa kimakosa na ulinzi wa anga wa Kuwait. Hili limetokea wakati kukiwa na mapigano mazito—Marekani na Israel wakifanya mashambulizi mazito nchini Iran kwa lengo la kuiangusha serikali ya Tehran, huku Iran nayo ikijibu mapigo kwa kurusha makombora na drones kwenye kambi za Marekani na nchi za Ghuba.

Habari njema ni kwamba marubani wote sita waliweza kujiokoa na wapo salama. Hii ndio picha halisi ya machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati kwa sasa!​

================ For English Audience ================
​
U.S. Central Command said Monday that Kuwait mistakenly shot down three American fighter jets, as war rages in the Middle East.

"At 11:03 p.m. ET, March 1, three U.S. F-15E Strike Eagles flying in support of Operation Epic Fury went down over Kuwait due to an apparent friendly fire incident," Central Command said in a statement.

"During active combat—that included attacks from Iranian aircraft, ballistic missiles, and drones — the U.S. Air Force fighter jets were mistakenly shot down by Kuwaiti air defenses," it added.

The U.S. and Israel have been conducting strikes against targets in Iran since Saturday morning, to topple Tehran's clerical regime. Iran has fired back, with retaliatory assaults featuring missiles and drones targeting several Gulf countries and American bases in the Middle East.

"All six aircrew ejected safely, have been safely recovered, and are in stable condition. Kuwait has acknowledged this incident, and we are grateful for the efforts of the Kuwaiti defense forces and their support in this ongoing operation," Central Command said.

"The cause of the incident is under investigation. Additional information will be released as it becomes available," it added.

SOURCE: POLITICO
 
marubani wote sita waliweza kujiokoa na wapo salama.
KWenye F-15E, inakuwa na seat mbili, moja rubani na moja anakaa WSO(weapon system officer) kazi zake ni kucheza na radar, sensor pamoja na silaha ikiwemo kulenga target.

Kama ni ndege tatu ina maana ni rubani watatu na WSOs watatu...

Je ndege hizo hazikuwa na IFF(kifaa cha kujitambulisha kwenye radar)? ndege zote tatu ?.. ikiruka hiko kifaa kinaiambia radar ni ndege friendly.

Ndege zote tatu wakati tofauti ?

Hao centcom wanaficha, ukweli utajulikana.
 
IFF inafanya kazi hasa kwa ndege za Air force husika au za NATO pekee. Kuwait haipo NATO ambao ndege zao zote zinatumia Link 16 command na sasa Link 22 inayokuja.

Kila jeshi duniani mkiwa high intensity kuna friendly fires zipo. Kwenye vita ya Kagera JWTZ walidungua ndege zao wenyewe mbili, kwenye vita ya Iraq Marekani vifaru vyake vya Abrams vilishambuliana, kwenye vita ya Ukraine jeshi la anga la Urusi (VKS) limeangusha ndege zake kadhaa ikiwemo Sukhoi Su-34.
Ndio maana Urusi kutokana na changamoto ya IFF waliunganisha jeshi la ulinzi wa anga (lililokuwa na air defence systems) na jeshi la anga (lilikuwa na ndege vita) mwaka 2015. Maana commands tofauti ni vyepesi kushambuliana wakiwa kwenye panick au high intensity.

Ni jambo la kawaida mno, ndio maana NATO huwa wanatumia muda mwingi kupangilia data links zao pamoja na kupeana taarifa wakiwa wanashambulia kwa pamoja, na mara nyingi linaenda jeshi moja moja kwanza. Sio hapo hapo ndege za Marekani na za UK ziko hewani.
Hata Marekani na Israel kwenye vita hii ya Iran utaona kuwa hawaendi kwa pamoja muda uleule. Ni kuepuka friendly fire.
 
Tambua kuwa umbali wa karibu zaidi wa wa kutoka Iran hadi Kuwait ni kilomita 500, yaani tuseme ncha za karibu kabisa za hizo nchi mbili. Sasa fighter jet ishambuliwe na air defense missile alafu isafiri kilomita 500? Imekuwa B-52 bomber hiyo kwamba ina injini nane hata zikizima tatu kwa pamoja bado inaenda.
 
Wameingia kichaka cha wahuni zaid yao wataimba kila wimbo shubamit zao,
 
Waongo hao hawataki kukiri Iran ndio kazipiga
 
Kuwait wanaamini Irani atarusha ndege badala ya kombora? au hajui US na IDF ndio watumiaji pekee wa ndege kwenye huu mgogoro wa karibuni.
Ndege na kombora vyote kwa pamoja ni air targets. MIM-104 Patriot inaweza dungua missile au jet, na radars zake zinaweza ona drone, missile au jet.

Umeona UAE wamesema wamedungua drones na makombora mangapi, kati ya vyote hamna jet yoyote ya Iran. Iran hana uwezo wa kurusha jet kwenda nchi yoyote na hiyo haimaanishi basi AD systems zifungwe hazina kazi.
 
Unaelewa Kuwait na Iran zinatenganishwa na persian gulf?, unaelewa kisiwa cha Iran kinaitwa Kharg?, unaelewa ni kilomita kama 200 hadi Kuwait.. unaelewa maeneo hayo ya persian gulf kuna jeshi la maji la Iran kitu kinachopelekea Iran kuwa karibu zaidi na Kuwait chini ya kilomita 200?

Possibility ipo kubwa tu ya Iran kulenga hizo ndege, ndege yenyewe ni F-15E, unachopinga haiwezi kupigwa ni kitu gani haswa?
 
Iran amesema amedungua hizo ndege.
Unaona hilo haliwezekani? Iran kudungua F-15E?
 
Iran kabutua hizo
 

Attachments

  • Screenshot_2026-03-02-21-47-44-275.jpg
    158.8 KB · Views: 27
Hizo zimebondwa na Iran
 

Attachments

  • Screenshot_2026-03-02-21-47-44-275.jpg
    158.8 KB · Views: 29
Surface vessels za Iran kwenye Persian gulf zimepigwa kasoro midget submarines na speed boats ambavyo vyote hivyo havibebi AD radars kufanya engagement ya AA missiles.

AA missile ya Iran ambayo ni surface launched ili ipige ndege ikiwa anga la Kuwait au iwe inakaribia inabidi iwe kuanzia higher medium range hadi long range, level kama Khordad 3 ambayo ikitumia interceptor ya Taer-3 yenye possible maximum range ya 200km kwa kuipendelea sana. Taer-3 ina warhead yenye about 80kg, maana medium range interceptors za Iran zenye range ya 75km zina warhead ya 45-50kg.

Sasa F-15E unaona ni ndege ya kupigwa na 80kg warhead alafu ikaendelea kupaa ili idondoke anga rafiki? MANPAD tu yenye 4kg warhead haiipaishi mbali, hiyo sio A-10 au Su-25 ambazo ni reinforced. Kama ingekuwa ni Iranian missiles hizo F-15E zingedondoka baharini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…