Hata Ayatollah kabla hajauwawa alikuwa anatoa matamko, hata makamanda wote waliouwawa walikuwa wanatoa matamko. Kuongea na kutenda ni vitu tofauti kabisa.
Kwenye vita ya siku 12 hizo F-15 tena sio E versions maana Israel hajazipokea, zile za zamani zilikuwa zinazurula anga la Iran kwa siku 12 zote alna hawakuangusha hata moja. Walidai wamekamata marubani wa kike wa Israel baada ya ndege zao kuzidungua, unajua mwenyewe story ilipoishia. So kama Iran ingekuwa inaweza kudungua jets za Israel au US, ingeonyesha vita ya last year badala yake wakaambulia vidrone viwili vitatu kama Houthi wafanyavyo.
Hizo F-15E ndio ndege zina uwezo mkubwa zaidi wa kubeba mzigo mzito kwa jet fighters, Israel hana bomber na anazitumia hizo kama bomber.
F-15E ni ground attack/strike.. kama inavyoitwa strike eagle, haikubuniwa kwa ajili ya air superiority, si nyepesi ,kwanza ina crew wawili.
Nasema F-15E kwa sababu Israel wali modify F-15E wakapata F-15I Raam, ambayo ndio kama bomber yao, walifunga avionics, radar na systems ili kuendana na mahitaji yao. hivyo naiita ni F-15E tu ile ile. Hivyo Israel hio F-15E unayosema wanayo toka zamani sana tena iliyoboreshwa.
Hivyo Israel F-15I ipo advanced zaidi kuliko hio F-15E ya US.
Hivyo unaposema walitumia ndege za zamani na hawakutumia hizo E sikukuelewa, labda kama ulimaanisha F-15A/C ambapo zina crew mmoja na ni nzuri kwa air superiority na nyepesi japo ni za zamani zaidi.
Elewa kwamba hizo ndege zilikuwa zinafanya stand off strike ,zinabeba cruise missile kama Delilah ambayo inaweza kwenda 250km, kuna missiles wanazo zinakwenda zaidi ya 300km.
Hivyo ni ndege nzuri kwa deep penetration strike, hivyo zinabeba cruise missiles na kusimama umbali ambapo ni safe distance, hivyo inaweza shambulia pasipo kuingia eneo ambapo wanaelewa kuna defenses.
Ndio maana wanapenda kuzitumia hizo ndege, ila mnavyoelezea ni as if kila zinapotaka kushambulia zinapita juu ya target na kushambulia, kitu ambacho si kweli, zinaweza ingia anga la Iran lakini kwa tahadhari, maana hizo ndege ni nzito.
Ndio maana nilikuuliza Iran anashindwa kuipiga F-15E, maana ni ndege za kubeba mizigo mizito, na nzuri kwa stand off strike, hivyo ukiona F-15E 3 zimeangushwa fahamu fika kinachoendelea Iran ni deep penetration/stand off strike. Tofauti na source zauongo kusema ndege zinapiga sarakasi anga la Iran.