Ndege tatu za Marekani zatunguliwa kimakosa na Kuwait

Ndege tatu za Marekani zatunguliwa kimakosa na Kuwait

Siyo kweli! Ukweli ni kwamba hizo ndege ziliingia kwenue Anga la Iran na zikashambuliwa na Iran. Zikiwa zimejeruhiwa zikaamua kugeuza na kuingia Anna la Kuwait na mara zikadondoka. Kwa bahati zilifanikiwa kuingia Anna la Kuwait vinginevyo zingedondokea Iran@
Wewe uko humu JF harafu bado una akili mgando kiasi hicho huna maana yoyote bora usiwe unachangia maana unatia aibu kwa UHARO huu Uliouandika!!
 
Kwa kipande cha karatasi hicho ndiyo unataka kutuaminisha ndege-vita hizo zilidunguliwa kwenye Dog fighting? Ndege za kirusi haliwezii kutamba kwenye ndege-vita za kimarekani kwenye dog fighting hawana uzoefu huo!!
Umeelewa hata ni kauli ya nani hiyo?
 
Umeelewa hata ni kauli ya nani hiyo?
Hata iwe kauli ya Nani Marubani wa ndege-vita wa Israel au Marekani hawawezi kupigana Dog fighting na marubani wa Iran na wairan wakashinda. Labda tu wewe huyajui Mapigano ya Dog fighting!!!
 
Kamandi la Jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema Machi 2, 2026 kuwa mfumo wa ulinzi wa anga wa Kuwait kwa bahati mbaya ulitungua ndege tatu za kivita za Marekani ikiwa vita dhidi ya Iran na Israel na Marekani ikiendelea.

Kwenye taarifa yao, CENTCOM imesema: "Saa 5:03 usiku Machi 1, 2026 ndege tatu aina ya F-15E zilizokuwa kwenye operesheni zilianguka nchini Kuwait kutokana na kushambuliwa kimakosa na washirika. Wakati wa mapigano makali yaliyohusisha makombora na drones za Iran, ndege hizo za Marekani zilitunguliwa kimakosa na ulinzi wa anga wa Kuwait."

Sasa ukweli wote upo wazi! Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imethibitisha kwamba zile ndege zao tatu hazikuanguka tu kama ilivyodaiwa mwanzo, bali zilitunguliwa kimakosa na ulinzi wa anga wa Kuwait. Hili limetokea wakati kukiwa na mapigano mazito—Marekani na Israel wakifanya mashambulizi mazito nchini Iran kwa lengo la kuiangusha serikali ya Tehran, huku Iran nayo ikijibu mapigo kwa kurusha makombora na drones kwenye kambi za Marekani na nchi za Ghuba.

Habari njema ni kwamba marubani wote sita waliweza kujiokoa na wapo salama. Hii ndio picha halisi ya machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati kwa sasa!​

================ For English Audience ================
​
U.S. Central Command said Monday that Kuwait mistakenly shot down three American fighter jets, as war rages in the Middle East.

"At 11:03 p.m. ET, March 1, three U.S. F-15E Strike Eagles flying in support of Operation Epic Fury went down over Kuwait due to an apparent friendly fire incident," Central Command said in a statement.

"During active combat—that included attacks from Iranian aircraft, ballistic missiles, and drones — the U.S. Air Force fighter jets were mistakenly shot down by Kuwaiti air defenses," it added.

The U.S. and Israel have been conducting strikes against targets in Iran since Saturday morning, to topple Tehran's clerical regime. Iran has fired back, with retaliatory assaults featuring missiles and drones targeting several Gulf countries and American bases in the Middle East.

"All six aircrew ejected safely, have been safely recovered, and are in stable condition. Kuwait has acknowledged this incident, and we are grateful for the efforts of the Kuwaiti defense forces and their support in this ongoing operation," Central Command said.

"The cause of the incident is under investigation. Additional information will be released as it becomes available," it added.

SOURCE: POLITICO
Kumbe?
 
Tukiacha mihemko na mahaba niue ,tukajadili kimantiki, Israel hawezi kuucheza mziki wa Iran akiwa man Solo yaani akiwa peke yake pasipo backup ya mmarekani... Hili lipo wazi kabisa..
Israel pale iran ni kama mkoa tu
 
Surface vessels za Iran kwenye Persian gulf zimepigwa kasoro midget submarines na speed boats ambavyo vyote hivyo havibebi AD radars kufanya engagement ya AA missiles.

AA missile ya Iran ambayo ni surface launched ili ipige ndege ikiwa anga la Kuwait au iwe inakaribia inabidi iwe kuanzia higher medium range hadi long range, level kama Khordad 3 ambayo ikitumia interceptor ya Taer-3 yenye possible maximum range ya 200km kwa kuipendelea sana. Taer-3 ina warhead yenye about 80kg, maana medium range interceptors za Iran zenye range ya 75km zina warhead ya 45-50kg.

Sasa F-15E unaona ni ndege ya kupigwa na 80kg warhead alafu ikaendelea kupaa ili idondoke anga rafiki? MANPAD tu yenye 4kg warhead haiipaishi mbali, hiyo sio A-10 au Su-25 ambazo ni reinforced. Kama ingekuwa ni Iranian missiles hizo F-15E zingedondoka baharini.
kinachowapa shida wakristo wa TZ,Venezuela,North Korea,Russia,China,South Africa , baadhi hazina dini zingine zina wakrsisto wengi zipo pamoja na Iran,halafu kuna wao wazee wa mungu wa Israel Kila kinachofanywa na nchi yenye waislam wengi wanakiponda😁🙃😅🤣,
 
kinachowapa shida wakristo wa TZ,Venezuela,North Korea,Russia,China,South Africa , baadhi hazina dini zingine zina wakrsisto wengi zipo pamoja na Iran,halafu kuna wao wazee wa mungu wa Israel Kila kinachofanywa na nchi yenye waislam wengi wanakiponda😁🙃😅🤣,
Mtanyooka tu kipondo kiko palepale tu!!
 
kinachowapa shida wakristo wa TZ,Venezuela,North Korea,Russia,China,South Africa , baadhi hazina dini zingine zina wakrsisto wengi zipo pamoja na Iran,halafu kuna wao wazee wa mungu wa Israel Kila kinachofanywa na nchi yenye waislam wengi wanakiponda😁🙃😅🤣,
Nenda na hao Wakristo wenzio mkasali. Hapa nimeongea technicalities za silaha, kama huwezi changia kwa muktadha huo kasali rozali na novena.

Zinapozungumziwa mbinu za vita usilete kusujudu wala kuabudu.
 
Back
Top Bottom