Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Jumatano ya 24th July 2024, ndege vita 4 zinazojulikana kama nuclear bombers za China na Russia ziliingia kufanya "strategic patrol" au "doria ya kimkakati" eneo la Alaska Air Defense Identification Zone (AADIZ) katika bahari ya Bering karibu na pwani ya Alaska Marekani.
Ndege 2 za China ziitwazo Xian H-6 strategic bombers na nyingine 2 za Russia TU-95MS strategic missile carriers zilionekana pwani ya Alaska. China na Russia wanasema walikuwa wanafanya 8th joint aerial strategic patrol.

China-Russia 8th joint aerial strategic patrol nuclear bombers
Russia imekuwa ikifanya patrol katika eneo la bahari ya Bering, lakini safari hii kwa mara ya kwanza ilishirikiana na China kufanya doria (patrol) katika eneo hilo la Arctic.
Kitengo cha ushirikiano wa Marekani na Canada katika ulinzi wa anga US-Canadian North American Aerospace Defense Command (NORAD) kilituma ndege zao ili kuzizuia. Hata hivyo NORAD inasema ndege hizo hazikuwa tishio kwa usalama zilikuwa eneo la anga la kimataifa.
Beijing imesema doria hiyo haina uhusiano wowote na hali ya sasa ya kimataifa na kikanda (Geopolitical)
Kremlin imesema ushirikiano wa China na Russia katika eneo la Arctic ni wa amani na utulivu.
Ikumbukwe mapema mwezi huu China na Russia walifanya 4th joint naval patrol eneo la kaskazini na mashariki mwa Bahari ya Pacific. Maeneo ya karibu na washirika wa Marekani ambao ni mataifa ya Japan, South Korea na visiwa vya Philippines.

China-Russia 4th joint naval patrol
China na Russia zimeendeleza uhusiano wa karibu tangu Moscow ilipowekewa vikwazo na nchi za Magharibi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine mnamo Februari 2022. Ushirikiano wa kina kati ya mataifa hayo mawili unatazamwa kwa wasiwasi na Marekani na nchi za Ulaya.
Nchi za NATO zilitoa tamko la pamoja mwishoni mwa mkutano wa hivi majuzi uliofanyika huko Washington na kuishutumu China kuwa "mwezeshaji madhubuti" (decisive enabler) wa vita vya Russia nchini Ukraine na kuitaka ikomeshe kuiunga mkono Russia kwa vifaa vya kutengeneza silaha na kisiasa.

Tamko la NATO la kuishutumu China kwa kuisadia Russia katika vita vya Ukraine
Katika ripoti kuhusu usalama wa Arctic iliyochapishwa Jumatatu, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilionyesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili, na kutabiri kuwa ushirikiano wao wa kijeshi utaendelea kuongezeka.

"Kitendo hiki cha China na Russia ni cha kichokozi, uchochezi ambao haujawahi kufanywa na wapinzani wetu."
Lisa Murkowski (Senator wa Alaska)
Lisa Murkowski (Senator wa Alaska)
Marekani ni kwenda naye kibabe tu kama China na Russia wanavyofanya. Mbona Marekani hufanya joint drills na patrol akishirikiana na washirika wake katika eneo la Bahari ya Kusini na ya Mashariki ya China, kwani kuna ubaya China na Russia wakienda eneo la karibu na Marekani kufanya patrol?