Ndege ya ATCL number TC 106 Bomberdier, tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa

Naomba picha ya ndege za wenzetu
 
Huuu ndo ubunifu wa kupongezwa. Hii ndege ndio inatakiwa iwe inatua JF Kennedy International Airport, NY. Ili kuwaonyesha kuwa na sisi tunaweza
 
Sio kama umekosea ni sahihi kabisa kumbukumbu zako. Tena Emirates walisitisha order ya ndege nyingine type hiyohiyo ya Airbus. Hiyo ilikuwa rangi imebanduka na wanajua haina madhara kufanya usitishe safari za ndege na wataalam walipopima mwanzoni walisema haina madhara. Ila Emirates hawakuwa na uhakika kama hakuna kasoro kwenye body mfano mfumo wa kuzuia radi.

Sasa huyu mchumiatumbo yupo analazimisha tuamini tairi lililolika ni salama eti kwa kutumia procedures sijui specifications. Anabishana na Goodyear ambao ndio one of the best katika utengenezaji wa matairi [emoji116]

... When inspecting aircraft tires, the first thing to check (after checking the tire pressure) is the amount of remaining tread to avoid excessive wear and possible unsafe conditions. According to Larry Rapsard, product support manager for The Goodyear Tire & Rubber Company (NYSE: GT), "Aircraft tires should be removed when the tread is worn to the base of any groove at any spot, or to the minimum depth stated by the aircraft manufacturer."

Au hivi [emoji116]
 
Usingeweka picha nisingeamini maana kati ya usafiri unaohitaji umakini basi ni ndege, ila kwa hapo niseme tuu kazi iendelee
 
@infopaedi

Infopaedia hongera kwa uzalendo wako,wahusika waone aibu,iko siku hizi ndege zitaua ndugu zetu kwa uzembe!!

Enzi za Magufuli ungekua rupango,zama za Mama kiguu na njia watakaa kimya tu!!!
 
Huu sasa ndio uzalendo. Hongera sana na pongezi nyingi zikufikie huko ulipo.
Hapa umetenda jambo la kijasiri sana la mpuliza filimbi kabla maafa hayajatokea.
Mungu akubariki sana.
Wahusika wachukuliwe hatua,maana unaweza kukuta hapo pesa za tairi mpya zilishapigwa siku nyingi.
 
Wakulungwa,huu ni uchochezi!!tafadhari ripoti Kituo chochote Cha polisi.
 
watakuja hapa wenyewe watachukuwa hatua.
 
Stori kama stori uwe ndani uone tairi hili ajabu jingine la dunia hongera kupanda nawe kunguru
Mkuu kuna ajabu gani?, kumbuka kwa aina hii ya ndege tairi za nyuma haziko kwenye belly, bali ziko attached kwenye wings. So, the moment matairi yanashushwa huwa yanaonekana vizuri sana.
 
Duh hii noma kweli, hivi ATCL wanaelewa madhara ya ndege kuwa na tairi kipara kweli?
Wanaelewa u seriosness wa jambo kama hili au wao ni bora liende tu..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…