Ndege ya ATCL number TC 106 Bomberdier, tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa

Umefanya vyema sana Mkuu. Kuweka habari ikiambatana na Picha.. Unasatahili Pongezi na shukrani kwa hii wake up call kwa Shirika..

Natumaini wahusika wata respond positively na kurekebisha hili tatizo haraka iwezekanavyo kwa Usalama Wa Abiria pamoja na Chombo chetu hiki..

Mapendo.
 
Ni ya kina Nani mkuu
Technicians: Wanawajibika kwenye Dail inspection and weekly Preventive Maintenance .

Safety: Wanawajibika kwenye daily checks and unsafe aircraft's identifications.

Pilots: Anawajibika kwasababu ni jukumu lake kuhakikisha ànafanya Daily prestar checkin
 
Kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya juzi hakuna cha kunenepesha profit books wala nini, ni mwendo wa hasara tuu kwenda Mbele
 
Tutakukamata tunajua Siti uliyokaa na taarifa zako tunazo, inaleta taharuki kwa watanzania. Asante
Na wewe tutakuloga na kabla wiki haijaisha utakuwa umefukuzwa kazi halafu utakuwa huoni wala kusikia tena...
 
Asante bwashee kwa elimu nzuri kabisa
Asije mbishi akabisha tena na Hii
 
Poleni sansa, tutachukua hatua baada ya ajali...
 
Wewe utakuwa hujawai kabisa kupanda ndege. Ukiwa kwenye siti za dirishani karibu na mlango wa emergency unaona matairi yote
Unaona hiyo kwenye mbawa.kushoto kulia.
Mbele huoni kitu mpk uwe ground.
Hiyo tairi ni tubeless ni mpira mtupu ajali hapo wanaweza kutembea mwaka mzima wasipate.
Swala ni kwamba wazingatie service km kawa.
Iko siku utakikuta hicho kibajaji kitunda huko kimepitiliza njia badala ya kupaa.
 
Asante bwashee kwa elimu nzuri kabisa
Asije mbishi akabisha tena na Hii
Hilo tairi halina madhara licha ya nyuzi kuchungulia.
Halina upepo ni mpira tu mwanzo mwisho lipasuke vipi?
Halafu hawa watalii wamerudi?🤔
 
Hizo tairi ukiangalia tu ni nzima sana.hizo nyuzi sio issue kabisa
Hiyo bajaj sio km vi harrier vyenu mnanunua china au Japan kwenda navyo Moshi.
Hiyo ni ndege, haichomoki hapo Airport bila kuchekiwa uzito,ujazo na kilakitu.
Mshamba mmoja kapanda picha mpk za matairi anarusha.
Angechukua long haul flight 14 hrs huyu si angekufa kwa presha.
Kuna sehemu huko kati Afghanistan na Iraq mkipita inapigwa swala mnatulia na mnaambiwa mfunge mikanda.
Lolote linaweza kutokea, hapo hata wahudumu wanajifungia huko.
We si utakufa kabisa.
Kuna Gape la Rome- Addiss ushapita?
Matairi hayahusiki hapo, utaweza kuomba sala zote unazozijua hapo kati
 
Hilo tairi halina madhara licha ya nyuzi kuchungulia.
Halina upepo ni mpira tu mwanzo mwisho lipasuke vipi?
Halafu hawa watalii wamerudi?🤔
Babu acha kupotosha
Air craft tires are pressurized!!!
Kama unakumbua ajali ya concord mwaka 2000 ilitokea baada ya concord kikanyaga chuma kilichoachwa na ndege iliyotangulia dc10, chuma hicho kilienda kupasua tenki la mafuta na blowout ya tari ndo ilasababisha moto
Nachotaka kusema ni kuwa matairi ya ndege yanakuwa inflated with air pressure tofauti ni kuwa kule wanatumia nitrogen air ili kupunguza expansion and contraction pressuer during landing and take off.
 
Hizi tairi ninazo size yake mtumba zipo fresha hazijatumika sana huko kwa wenyewe. ATCL wanitafute tuongee biashara hapa
 
Jamaa ana ulalamishi wa ki bwege. Tairi tu kuwa hivyo unaanzisha uzi? Umefunua bonet? Ungeona kule kuna spares mpaka za vits zimefungwa. Mafuta wanaweka ya kidumu, wiring yake nyaya zipo uchi tu nje nje... Hayo mambo siyo ya kuzungumzia. Achani mambo madogo. Hiyo tairi haijapasuka bado inafaa... Mpaka ipasuke ndo itakuwa useless
 
Ndio hivyo! Atashtakiwa kwa kuzusha taharuki kwa watu wanaotegemea kuitumia ATCL.

Hivyo atakuwa ni mhujumu Uchumi.
Airline industry is a safety regulated bussiness, cha kwanza kabisa ni usalama na hauwezi kuwa compromised na chochote kile , at 39000 feets above sea level hakuna msaada wowote mtakaopata kama ndege itazingua
Huyu jamaa ni whistleblower , maana bila yeye huenda tungepata tukio siku moja kwa uzembe wa watu fulani wachache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…