Ndege ya ATCL number TC 106 Bomberdier, tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa

Ndege ya ATCL number TC 106 Bomberdier, tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa

Jana nimesafiri na ATCL ndege number TC 106 Bomberdier toka Dar kuja Mbeya. Hii ndege tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa. Hii ni hatari sana.

Nilikaa dirishani mkabala na hizi tairi. Jana tulitoka Dar na mvua, na mipira ikiloa si rahisi kuona jinsi mpira ulivyolika. Tunafika, mipira imekauka. Ilivyotoa tairi nikaona jinsi ilivyoisha. Nilikosa amani mpaka ilipo simama.

Hata kama ni tubeless, nadhani kuna kiwango kinacho ruhusiwa cha tairi kulika.

Kwa namna zilivyo hapo, hata uwiano wa kubeba mzigo wakati wa kutua ni tofauti.

Sababu hiyo tairi isiyolika sana ndio inaanza kugusa chini na kubebe mzigo mkubwa.

Hebu fikiria ndege imetua na hiyo tairi inapiga mzinga wakati iko kwenye speed. Au iko kwente speed ya kuruka halafu ndiyo ina piga mzinga. ATCL mtatuuwa kizembe.

View attachment 2197854

View attachment 2197855
Umefanya vyema sana Mkuu. Kuweka habari ikiambatana na Picha.. Unasatahili Pongezi na shukrani kwa hii wake up call kwa Shirika..

Natumaini wahusika wata respond positively na kurekebisha hili tatizo haraka iwezekanavyo kwa Usalama Wa Abiria pamoja na Chombo chetu hiki..

Mapendo.
 
Ni ya kina Nani mkuu
Technicians: Wanawajibika kwenye Dail inspection and weekly Preventive Maintenance .

Safety: Wanawajibika kwenye daily checks and unsafe aircraft's identifications.

Pilots: Anawajibika kwasababu ni jukumu lake kuhakikisha ànafanya Daily prestar checkin
 
Nina picha kama hiyo ya ndege inayofanana na hiyo, tofauti ni kuwa yangu niliipiga mwaka juzi nikitokea bukoba, with stoppover mwanza , by then niliogopa hata kuileta hapa kwa hofu kuu ya the late .
Atcl wapo busy kunenepesha profit books ili waonekane wanajiendesha kwa faida matokeo yake hata basic servise zinachelewa

When you put profit before safety, thats when youll have accidents.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya juzi hakuna cha kunenepesha profit books wala nini, ni mwendo wa hasara tuu kwenda Mbele
 
Tutakukamata tunajua Siti uliyokaa na taarifa zako tunazo, inaleta taharuki kwa watanzania. Asante
Na wewe tutakuloga na kabla wiki haijaisha utakuwa umefukuzwa kazi halafu utakuwa huoni wala kusikia tena...
 
Sio kama umekosea ni sahihi kabisa kumbukumbu zako. Tena Emirates walisitisha order ya ndege nyingine type hiyohiyo ya Boeing. Hiyo ilikuwa rangi imebanduka na wanajua haina madhara kufanya usitishe safari za ndege na wataalam walipopima mwanzoni walisema haina madhara. Ila Emirates hawakuwa na uhakika kama hakuna kasoro kwenye body mfano mfumo wa kuzuia radi.

Sasa huyu mchumiatumbo yupo analazimisha tuamini tairi lililolika ni salama eti kwa kutumia procedures sijui specifications. Anabishana na Goodyear ambao ndio one of the best katika utengenezaji wa matairi [emoji116]

... When inspecting aircraft tires, the first thing to check (after checking the tire pressure) is the amount of remaining tread to avoid excessive wear and possible unsafe conditions. According to Larry Rapsard, product support manager for The Goodyear Tire & Rubber Company (NYSE: GT), "Aircraft tires should be removed when the tread is worn to the base of any groove at any spot, or to the minimum depth stated by the aircraft manufacturer."

Au hivi [emoji116]View attachment 2198749
Asante bwashee kwa elimu nzuri kabisa
Asije mbishi akabisha tena na Hii
 
Wewe utakuwa hujawai kabisa kupanda ndege. Ukiwa kwenye siti za dirishani karibu na mlango wa emergency unaona matairi yote
Unaona hiyo kwenye mbawa.kushoto kulia.
Mbele huoni kitu mpk uwe ground.
Hiyo tairi ni tubeless ni mpira mtupu ajali hapo wanaweza kutembea mwaka mzima wasipate.
Swala ni kwamba wazingatie service km kawa.
Iko siku utakikuta hicho kibajaji kitunda huko kimepitiliza njia badala ya kupaa.
 
Asante bwashee kwa elimu nzuri kabisa
Asije mbishi akabisha tena na Hii
Hilo tairi halina madhara licha ya nyuzi kuchungulia.
Halina upepo ni mpira tu mwanzo mwisho lipasuke vipi?
Halafu hawa watalii wamerudi?🤔
 
Hilo tairi halina madhara licha ya nyuzi kuchungulia.
Halina upepo ni mpira tu mwanzo mwisho lipasuke vipi?
Halafu hawa watalii wamerudi?🤔

MICHELINAirX.jpg


images (2).jpeg


Radial-Tire-Cut-Away-with-Labels.jpg


 
Mkuu kuna vitu unaelezwa lakini hata kama wewe siyo mtaalamu wa hiyo fani, lakini mantiki tu inakataa. Sawa hizo ni tairi zenye matabaka. Tairi moja tabaka limeisha, ina maana tairi moja ni kubwa kuliko la pili. Kwenye kubeba mzigo hapo yanabeba sawa? Moja likizidiwa?
Hata hivyo hebu turudi nyuma. Inakuwaje tairi zilizokaa pamoja vile, moja iishe kwa kiwango kile na ya pili ikiwa nzuri bado walau kashata zinaonekana! Je, kuna mlinganyo hapo?? Kukosekana mlinganyo si tatizo???. Au hiyo tairi ilifungwa ikiwa imeisha hivyo?, kwanini?
Nafahamu kuna swala la tairi ya ndani kuanza kuisha kwenye vyombo vya moto barabarani. Nayo pia hutokea kwenye ndege?. Hata kama hutokea, ndio liachwe kwa kiwango kile cha nyuzi kuonekana???
Za kuambiwa changanya na zako (kama zipo). Lakini siyo habari ya kuambiwa tairi zina matabaka. Sawa zina matabaka....halafu!!!!
Hizo tairi ukiangalia tu ni nzima sana.hizo nyuzi sio issue kabisa
Hiyo bajaj sio km vi harrier vyenu mnanunua china au Japan kwenda navyo Moshi.
Hiyo ni ndege, haichomoki hapo Airport bila kuchekiwa uzito,ujazo na kilakitu.
Mshamba mmoja kapanda picha mpk za matairi anarusha.
Angechukua long haul flight 14 hrs huyu si angekufa kwa presha.
Kuna sehemu huko kati Afghanistan na Iraq mkipita inapigwa swala mnatulia na mnaambiwa mfunge mikanda.
Lolote linaweza kutokea, hapo hata wahudumu wanajifungia huko.
We si utakufa kabisa.
Kuna Gape la Rome- Addiss ushapita?
Matairi hayahusiki hapo, utaweza kuomba sala zote unazozijua hapo kati
 
Hilo tairi halina madhara licha ya nyuzi kuchungulia.
Halina upepo ni mpira tu mwanzo mwisho lipasuke vipi?
Halafu hawa watalii wamerudi?🤔
Babu acha kupotosha
Air craft tires are pressurized!!!
Kama unakumbua ajali ya concord mwaka 2000 ilitokea baada ya concord kikanyaga chuma kilichoachwa na ndege iliyotangulia dc10, chuma hicho kilienda kupasua tenki la mafuta na blowout ya tari ndo ilasababisha moto
Nachotaka kusema ni kuwa matairi ya ndege yanakuwa inflated with air pressure tofauti ni kuwa kule wanatumia nitrogen air ili kupunguza expansion and contraction pressuer during landing and take off.
 
Hizi tairi ninazo size yake mtumba zipo fresha hazijatumika sana huko kwa wenyewe. ATCL wanitafute tuongee biashara hapa
 
Jamaa ana ulalamishi wa ki bwege. Tairi tu kuwa hivyo unaanzisha uzi? Umefunua bonet? Ungeona kule kuna spares mpaka za vits zimefungwa. Mafuta wanaweka ya kidumu, wiring yake nyaya zipo uchi tu nje nje... Hayo mambo siyo ya kuzungumzia. Achani mambo madogo. Hiyo tairi haijapasuka bado inafaa... Mpaka ipasuke ndo itakuwa useless
 
Ndio hivyo! Atashtakiwa kwa kuzusha taharuki kwa watu wanaotegemea kuitumia ATCL.

Hivyo atakuwa ni mhujumu Uchumi.
Airline industry is a safety regulated bussiness, cha kwanza kabisa ni usalama na hauwezi kuwa compromised na chochote kile , at 39000 feets above sea level hakuna msaada wowote mtakaopata kama ndege itazingua
Huyu jamaa ni whistleblower , maana bila yeye huenda tungepata tukio siku moja kwa uzembe wa watu fulani wachache
 
Back
Top Bottom