Ndege ya ATCL number TC 106 Bomberdier, tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa

Ndege ya ATCL number TC 106 Bomberdier, tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa

Nauli Ni shingapi dar to mbeya
Nauli za ndege hupanda na kushuka kutegemea msimu na tarehe ya booking.
Mfano ukiwa unasafiri mwezi wa 5 ukifanya booking leo bei yake ni nafuu ukilinganisha na anayesafiri j3 ijayo akibook sasa hivi
Screenshot_20220423-211309_Chrome.jpg
 
Da
Ajabu gani? Kutegemea na ulipokaa, mbona tairi unaziona kabisa kabla hazijakunjwa baada ya ndege kupaa; au matairi yakikunjuliwa wakatii ndege inakaribia kutua. Zaidi ya hayo, mtoa mada amekupa na picha ya hizo tairi. Sasa ubishi wa nini?
Dah!! Yaani mkuu kuna vitu unaweza usiamini mpaka uone. Huyo jamaa anabisha wakati pixha inaonyesha imepigwa tokea ndani. Ila mi sishangai sana, kuna baadhi ya nyuzi nimeshaona watu nana-comment bila kusoma uzi. Il huyu jamaa yako kazidi 🤣🤣🤣
 
Hii ni Atari kuliko wanavyodhani. Hapo Engineer aliekagua na kujaza log book ahojiwe. Rubani pia anatakiwa kuhojiwa kwanini aruhusu kuruka na tairi kama Hilo.
Nafikiri Matindi na Tim yake wajichunguze
Rubani ni lzm atakuwa mswahili wale wengine ufuata standard wapo radhi kuacha Kazi kuliko kuendesha kitu chakavu
 
Jana nimesafiri na ATCL ndege number TC 106 Bomberdier toka Dar kuja Mbeya. Hii ndege tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa. Hii ni hatari sana.
Nilikaa dirishani mkabala na hizi tairi. Jana tulitoka Dar na mvua, na mipira ikiloa si rahisi kuona jinsi mpira ulivyolika. Tunafika, mipira imekauka. Ilivyotoa tairi nikaona jinsi ilivyoisha. Nilikosa amani mpaka ilipo simama.
Hata kama ni tubeless, nadhani kuna kiwango kinacho ruhusiwa cha tairi kulika. Kwa namna zilivyo hapo, hata uwiano wa kubeba mzigo wakati wa kutua ni tofauti. Sababu hiyo tairi isiyolika sana ndio inaanza kugusa chini na kubebe mzigo mkubwa. Hebu fikiria ndege imetua na hiyo tairi inapiga mzinga wakati iko kwenye speed. Au iko kwente speed ya kuruka halafu ndiyo ina piga mzinga. ATCL mtatuuwa kizembe.
View attachment 2197854

View attachment 2197855
Mkuu mbona hili lilishatolewa ufafanuzi na wataalam mara nyingi kuwa ni tairi zenye tabaka (layered tyre) na sio kuisha kama unavyotaka kuamini. Rubani gani ataondoa ndege huku akijua wakati wa kutua ni kifo? Kuna kitu kinaitwa wallk around kwa rubani. Hii ni pale anapotembea kuzunguka ndege ili kubaini kama kuna hitirafu yoyote inayoonekana kwa macho kabla ya kuwasha na kuruka. Mambo mengine tuwaulize wataalam tuache mihemuko.
 
Rubani ni lzm atakuwa mswahili wale wengine ufuata standard wapo radhi kuacha Kazi kuliko kuendesha kitu chakavu
Hakuna rubani wa aina hiyo. Are anaona!!!tuache uswahili. Ndege sio bajaji kuwa kila mtu anauelewa wake
 
Mkuu mbona hili lilishatolewa ufafanuzi na wataalam mara nyingi kuwa ni tairi zenye tabaka (layered tyre) na sio kuisha kama unavyotaka kuamini. Rubani gani ataondoa ndege huku akijua wakati wa kutua ni kifo? Kuna kitu kinaitwa wallk around kwa rubani. Hii ni pale anapotembea kuzunguka ndege ili kubaini kama kuna hitirafu yoyote inayoonekana kwa macho kabla ya kuwasha na kuruka. Mambo mengine tuwaulize wataalam tuache mihemuko.
Mkuu kuna vitu unaelezwa lakini hata kama wewe siyo mtaalamu wa hiyo fani, lakini mantiki tu inakataa. Sawa hizo ni tairi zenye matabaka. Tairi moja tabaka limeisha, ina maana tairi moja ni kubwa kuliko la pili. Kwenye kubeba mzigo hapo yanabeba sawa? Moja likizidiwa?
Hata hivyo hebu turudi nyuma. Inakuwaje tairi zilizokaa pamoja vile, moja iishe kwa kiwango kile na ya pili ikiwa nzuri bado walau kashata zinaonekana! Je, kuna mlinganyo hapo?? Kukosekana mlinganyo si tatizo???. Au hiyo tairi ilifungwa ikiwa imeisha hivyo?, kwanini?
Nafahamu kuna swala la tairi ya ndani kuanza kuisha kwenye vyombo vya moto barabarani. Nayo pia hutokea kwenye ndege?. Hata kama hutokea, ndio liachwe kwa kiwango kile cha nyuzi kuonekana???
Za kuambiwa changanya na zako (kama zipo). Lakini siyo habari ya kuambiwa tairi zina matabaka. Sawa zina matabaka....halafu!!!!
 
Hizi ndo zile tairi zinaitwa mitano tena au? nunueni hata mchina bhanaa........
 
Back
Top Bottom