NDEGE YA KWANZA KUUNGANISHWA TANZANIA
View attachment 2782387
Tanzania imeanza safari ya kuzindua ndege yake ya kwanza kabisa kutengenezwa nyumbani.
Kampuni ya "Airplanes Africa Limited" inazindua ndege ya kwanza kabisa Tanzania kuunganishwa nchini katika maenesho ya
TIMEXPO 2023.
Ndege aina ya
Skyleader600 imeundwa kwa ajili ya safari za kibiashara na uwezo wa kumudu gharama ya chini ya uendeshaji.
Poa kampuni ya
AAL inapanga kupanua
Skyleader500 kwaajili ya matumizi ya kilimo.
Kampuni hiyo iliyo
Morogoro, ilionesha ndege ya kwanza kabisa kuunganishwa nchini Tanzania siku ya Jumatano. Tamasha la
Skyleader 600’s lilifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee katika Maonesho ya Kimataifa ya Wazalishaji Tanzania
(TIMEXPO), yaliyofanyika katika jiji kuu la Dar es Salaam.
Ndege hiyo imeundwa kupakia watu wawili akiwemo rubani.
David Grolic, mkurugenzi wa AAL alifichua kuwa shirika lake liliamua kuchukua fursa ya mazingira mazuri ya biashara ya Tanzania, na nia ya kutumia teknolojia mpya, kwa kuanzisha kuunganisha ndege nchini.
Chanzo:
The Morogoro-based aircraft company, Airplanes Africa Limited (AAL), displayed the first-ever assembled aircraft in Tanzania on Wednesday
africa.businessinsider.com