Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Mkuu ndege huwa inakuwa designed,kuruka kwa engine moja au bila engine na rubani anafundishwa kurusha ndege kwa engine moja na bil engine.As long as engine moja imezima na hakuna physical damage yoyote uwezekano wa ndege kutua salama ni mkubwa kuliko gari kutokupata ajali likipata pancha ya tairi moja wakati likiwa na spidi sawa na ya ndege.
Ndege haiwezi kupaa bila engine ,
 
Sisi engine zote zilizima na Rubani akasema tuanze kusali..lkn cha ajabu tulitua salama JKIA
Acheni kutuletea hadithi za Abunuwasi!
Tumeshambiwa na watu wa ndege kuwa Engine zikisima ndege huweza kwenda umbali mfupi sana (10,000ft) sawa na viwanja vitatu vya mpira, namaanisha hata kama unakiona kiwanja cha kutua mbele haitaweza kukifikia.....
 
Acheni kutuletea hadithi za Abunuwasi!
Tumeshambiwa na watu wa ndege kuwa Engine zikisima ndege huweza kwenda umbali mfupi sana (10,000ft) sawa na viwanja vitatu vya mpira, namaanisha hata kama unakiona kiwanja cha kutua mbele haitaweza kukifikia.....
Flight 009 ya British airways!!
Hawa jamaa walizimikiwa na engine zote nne wakiwa huko juu 39000 feets,
Pilots alifanya gliding kwa karibia dakika 30 ndipo wakafanikiwa kuwasha engine 3 , with engine off waliweza kutembea urefu wa km 120
It is said boeing 747 inaweza kupata gliding ratio ya hadi 15.1,
Maana yake ni kuwa kila kilometer inayoshuka inawezekana kupata km 15 za kuelekea mbele , 39000 feets ni sawa na km 11 , 11x15 ni sawa na 165, maana yake at 39000 feets pilot anaweza kufanya gliding na kupata hadi km 165 za umbali
 
Mkuu ndege huwa inakuwa designed,kuruka kwa engine moja au bila engine na rubani anafundishwa kurusha ndege kwa engine moja na bil engine.As long as engine moja imezima na hakuna physical damage yoyote uwezekano wa ndege kutua salama ni mkubwa kuliko gari kutokupata ajali likipata pancha ya tairi moja wakati likiwa na spidi sawa na ya ndege.
ok fine but ile kusikia ndege imepata itilafu mkiwa juu usiombe yakukute, kuna siku tulichelewa kuland pale KIA, Aiseee asikwambie mtu bila hata kuambiwa nn shida tayari taharuki ilianza kwa abiria ndio iwe mambo ya engine kutokufanya kazi ?
 
Relax wakuu, ndege hizi Zina engine mbili na engine moja ina uwezo wa kuifikisha ndege salama means to land safely, na hata engine zote zikizima pilot ana uwezo wa to land ndege as far as electronics ziwe zinafanya kazi(elewa kuna back up batteries zake).

Kudos kwa pilot wetu inajionyesha ni jinsi gani upo byeee na kwa abiria na wafanyakazi wote ambao mlitulia vema ndani ya ndege, ni MUHIMU mno kusikiliza yale maagizo yanayotolewa kabla ya safari kuhusu emergency.

Wengi wetu huwa we don't pay any attention kwa kufikiria it will not happen to us! Usafiri wa ndege ndio salama kuliko wote duniani.
Ni salama zaidi kuliko usafiri wa gari moshi (train)?
 
Ni salama zaidi kuliko usafiri wa gari moshi (train)?
Unapenda mabishano kweli mkuu,gari moshi lipi hilo?Dar to Kigoma ni salama zaidi kwa gari moshi kuliko ATC flight?,common sense mkuu muda mwingine
 
Ndiyo raha ya kuzoea hayo madude, nadhani alikuwa upande wa dirishani, dogo 'sijui alikuwa anacheza game kwenye simu' kashtuka mmh, mbona engine kama imezima, hakuzoea hiyo hali, mara paap kelele ahahahaaaa...

Angekuwa kijana wa moshono au nyakato aliyezoea Kilimanjaro, BM au Kitendaguro aah hapo ndo selfie mtindo mmoja!.
 
Naomba reference ya hiyo British airway kwani hizi information zipo unrealistic
unaweza kupost hiyowebsite uliyosoma nasi tujisomee
 

Attachments

  • Screenshot_20220731-182854_Chrome.jpg
    Screenshot_20220731-182854_Chrome.jpg
    79.1 KB · Views: 14
Gliding nikama kuelea yaani fikiria ndege imejaa hewa ndani na inakimbia km 890 kwa saa, na ipo juu sana kwenye ft 39,000 halafu uzime engine; itaendelea kwenda kwa kasi huku mwendo ukipungua taratibu ikiwa ni pamoja na kushuka chini taratibu...hapo hakuna ufundi wa ajabu kwani inaelea yenyewe (gliding)
 
Ndo mana mimi kabla ya kupanda ndege huwa nakunywa zangu pombe kidogo ili akili ikae sawa, hata nikiwa ndani ya ndege wale wahudumu wakianza kugawa vinywaji, mimi huwa naagiza bia tu ili akili ivurugike kidogo, mambo kama hayo yakitokea unabaki unawachora tu wala hupaniki sana, pombe bwana
 
Most planes can fly with one engine.
All, not most 2,3,4 or more engined planes are by design able to fly if one engine got a problem, and pilots are trained very well to handle those kind of emergencies
 
View attachment 2306678
Abiria ndani ya ndege ya Kampuni ya Precision, jana waliingiwa na hofu ya usalama wao baada ya injini moja kuzima ikiwa angani.

Ndege hiyo yenye namba PW 467 ikitokea Kahama, ikielekea Dar es Salaam kupitia Mwanza, ilizima injini baada ya dakika 51 kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza.

Hofu ilianza kutokea baada ya abiria mmoja, kijana wa kizungu, kuanza kupiga kelele, akiwaeleza wenzake waliokuwa wameketi jirani, kwamba injini imezima.

Baadaye abiria wengine waliingiwa hofu, huku baadhi wakisali, wakilia na wengine kuonekana wamejiinamia, huku wamefunika nyuso zao.

Baada ya abiria kuonekana 'wakipaniki' ndipo rubani wa ndege hiyo alitangaza kuwepo kwa hitilafu hiyo huku akieleza kwamba hali siyo ya kutisha sana.

"Abiria wetu wapenzi, ndege yetu imepata tatizo la kiufundi, injini moja imezima, lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani, tunapanga kutua katika kiwanja jirani na hapa tulipo," alisema rubani huyo.

Hata hivyo, tulizo la mwana anga huyo halikuleta afueni ya wasiwasi kwa abiria wengi, waliendelea na hofu yao, huku wengine waliokuwa hawajatambua kinachoendelea wakiungana na wengine kusononeka.

Rubani alirejea tena kwa tangazo; "Abiria wetu wapendwa, tunasikitika kwa kilichotokea, nawaomba kuwa watulivu wakati sasa tunajiandaa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Tutatua ndani ya dakika 20."

Baada ya muda huo, ndege hiyo ilitua salama katika uwanja huo na abiria walishangilia. Wengine walipiga kofi, wengine wakipiga kelele za shangwe na wengine wakimshukuru Mungu.

Mmoja wa abiria aliyekuwamo ndani ya ndege hiyo, Simon Mkina, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter na taarifa hiyo kusambaa dunia nzima, huku akipongezwa kwa kutoa taarifa hiyo mapema.
Hivi wabongo Ni elimu hatuna au imagine mtu hajui hata engine ikizima inakuaje anaona propela limeacha zunguka sijui Ni anajua AC imezimwa daaa Yani hadi mzungu apige kelele😁 tutawaliwe hadi kiama
 
Back
Top Bottom