Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Mbona hiyo kawaida sana.
Miaka ya 90 ndege ya ATC, wakati huo Fokker Friendship ilizima engine tukitoka Kigoma kuja Tabora, pembeni alikaa mzee mmoja maarufu mwanasiasa, simtaji.

Baadaye ilirekebishwa ile engine pale Tabora baada ya dk 45, tukatoka Tabora kuja Dar.

Engine zote zikawa zikafanya kazi.

ENGINE ya Pili tukiwa hewani nayo ikazima, hapo ndo nikaona mlango wa kuondoka duniani.
Nilipanic.

Maana nikafikiri kama engine ile mbovu ya kwanza ikizima na hatuna parachute, dunia ndo kwaheri.

Lakini tulifika Dar bila matatizo.

Hizo ndege Fokker50 zilisimamishwa baadaye maana zilizeeka sana.
 
Tatizo siyo tu kuzima bali ni nini kimefanya ikazima na ni nini kitafuata. Ni kweli ndege zenye injini mbili zina uwezo kabisa wa kuruka na injini moja bila tatizo lakini unapoona injini imezima inaweza kuwa matokeo ya multiple instruments failure au moto au janga jingine. Hapo ndiko kwenye shida.
 
Hapa bila ndugu barafu kuweka neno lake hapa,sitaandika chochote kuhusiana na uhalisia wa jambo hili.
 
Vipi kama hakuna uwanja karibu? Inaweza kwenda umbali gani bila engine ?

Na si ndege zote zina twin engines.
 
Vipi kama hakuna uwanja karibu? Inaweza kwenda umbali gani bila engine ?

Na si ndege zote zina twin engines.
Viwanja vya ndege vipo vingi mno na marubani kabla ya safari wanakuwa na informations zote na huduma gani ipo kwenye viwanja hivyo, umbali gani inaweza kwenda kuna factors nyingi za kuziangalia mfano ipo umbali gani juu, weather, including upepo na pia ukubwa wa ndege, hivi Vindege vya single engine mkuu hata kwenye viwanja vya mpira inakitua tu,kumbuka yule pilot wa USA aliyetua Ile ndege kwenye mto na akaokoa watu wote (hii ndege ilipoteza engine zote)na kumbuka yule pilot wa Ile ndege ya Ethiopia airways iliyotekwa na akaiweka Ile ndege pwani ya Mauritius baada ya kuishiwa mafuta, aliokoa baadhi ya abiria ila watekaji wote walipelekwa jehanamu
 
Ningekuwepo humo ndegeni ningevaa zangu earphone sauti hadi mwisho kabsa. Ningeweka nyimbo ya rose muhando _Nakaza mwenendo nifike mbinguni.
Ningefanya hivyo kwa sababu hata ningepiga makelele ingebadikisha chochote??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…