Ndege ya Tanzania yakamatwa nje, Taifa ladaiwa bilioni 380 kwa kuvunja mkataba bila utaratibu

Ndege ya Tanzania yakamatwa nje, Taifa ladaiwa bilioni 380 kwa kuvunja mkataba bila utaratibu

Tatizo hizo pesa zinawanufaisha wao zaidi ndio maana sie tuna enjoy tu.!

Enzi za Magu ingetuuma sana maana alitumia hizo pesa kujengea lami kijijin kwetu na kujenga masoko, stend n.k
Ningekuwa mkatili ningekuambia deni husika lilipoanzia. Mimi ni nani wa kumuambia mtoto wa kizungu Santa isn't real.
 
Acha tu ikamatwe ili tutawaliwe vizuri. Wakati wa JPM wengi waliziponda na kumzodoa leo zinakamatwa watu hao wanajifanya kuumia, huu ndo unafiki wenyewe na mie nasema acha tupigwe.

Alafu msiyoyajua ni mengi kuliko yaliyo nyuma ya hili lakini yote kwa yote ukidhani Ikulu ni kupigiwa tu saluti na mizinga unajidanganya. Ikulu ni mahala patakatifu, tunayoyapitia kama nchi kwa sasa hivi kwakweli nchi yetu inaumizwa sana lakini Mungu ndo anajua.

Wawekezaji feki hawataki ushindani, kwanini ili wewe uendelee ufikilie kuua vya eengine kwanza?

Acha wateke soko lote kwa hila. Hivi zinazoruka leo zimebaki ngapi vile maana muda si mrefu zinaisha hizi. Ambaye angeweza kusimamia leo hayupo sasa nani atasimama leo, kwa maoni yangu ni bora hizi ndege ziuzwe zote pesa ifanye mengine.

Tukiziacha ziishe zenyewe tutaambulia vilio vikubwa sana watanzani, ni heri nusu shari kuliko shari zima.

Tunastahili laana.
 
Kweli magazeti siku hizi yana ka-uhuru ka kuandika kitu, ingekuwa enzi zile…wangekiona…
Kwani kipindi cha Magufuli hazikukamatwa na magazeti yakaandika? Sema kwa Magufuli mafisadi yaligonga mwamba, hakuna ndege iliyochuliwa na kesi zao za kubumba zilishindwa, na wewe naona ni uzao wa mafisadi, endelea kulamba asali tu.
 
Bilioni 380 ni pesa ndogo sana kwa nchi hii. Walipe tu deni la watu. Kwani kwenye ule ujinga wao wa Royal Tour walitumia Sh. ngapi kama sio zaidi ya hizo?
 
Acha tu ikamatwe ili tutawaliwe vizuri. Wakati wa JPM wengi waliziponda na kumzodoa leo zinakamatwa watu hao wanajifanya kuumia, huu ndo unafiki wenyewe na mie nasema acha tupigwe.

Alafu msiyoyajua ni mengi kuliko yaliyo nyuma ya hili lakini yote kwa yote ukidhani Ikulu ni kupigiwa tu saluti na mizinga unajidanganya. Ikulu ni mahala patakatifu, tunayoyapitia kama nchi kwa sasa hivi kwakweli nchi yetu inaumizwa sana lakini Mungu ndo anajua.

Wawekezaji feki hawataki ushindani, kwanini ili wewe uendelee ufikilie kuua vya eengine kwanza?

Acha wateke soko lote kwa hila. Hivi zinazoruka leo zimebaki ngapi vile maana muda si mrefu zinaisha hizi. Ambaye angeweza kusimamia leo hayupo sasa nani atasimama leo, kwa maoni yangu ni bora hizi ndege ziuzwe zote pesa ifanye mengine.

Tukiziacha ziishe zenyewe tutaambulia vilio vikubwa sana watanzani, ni heri nusu shari kuliko shari zima.

Tunastahili laana.
Vipi Mwajemi katia guu lake hapo?
 
Shida nini tena jamani? Nani hao wasio na nia njema na taifa hili?
Tabia zetu za kutofuata katiba na sheria, zimetujengea mazoea za kutoheshimu hata mikataba.

Serikali inatakiwa kubadilika, ijenge utaratibu wa kuheshimu katiba, sheria, kanuni na mikataba. Serikali na taasisi zake na viongozi, wamezoea kutofuata katiba, kuvunja sheria, kanuni, taratibu na kutoheshimu mikataba. Wanafanya hayo yote kwa jeuri ya dola, hawajui kuwa ujeuri huo hauvuki mipaka ya nchi.

Inatupasa wananchi tukemee tabia za ujeuri wa viongozi wa Serikali ili Serikali ibadilike, iendane na Dunia ya watu wastaarabu kuliko kuendelea kulea hizi tabia za guchiro republic.

Unafikiri kama yale mambo ya hovyo ya kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, kesi ya kumbambikia Mbowe ya ugaidi au kumtwanga risasi zaidi ya 30 Lisu, au kumpoteza Kanguye, Azory Gwanda na Sanane, kama wangekuwa watu wa mataifa mengine, fidia yake ingekuwa bilioni ngapi?

Japo Serikali imezoea kudhulumu haki mbalimbali kutokana na mazoea ya miaka mingi, sasa ibadilike, iheshimu mikataba, ndiyo tabia ya watu wastaarabu.
 
Vita ya kiuchumi waulizwe ZIMBABWE, N.KOREA, IRAN na Russia. Tanzania inahukumiwa kwa maamuzi yake ya kukurupuka na kutofuata makubaliano.
 
Kuna watu watashangilia. Na kuombea iwe kweli.
Hapa suala siyo kushangilia au kuchukia, bali kujiuliza:

1) Je, madai hayo dhidi ya shirika letu ni halali?

2) Kulitokea nini hata ATCL ikashindwa kuheshimu mkataba?

3) Nani aliyesababisha?

4) Aliyesababisha ataadhibiwa kwa namna gani, sawa na hasara aliyotusababishia?
 
Mashauri yaliyopo katika hatua za usuluhishi ni:
1. Sunlodges v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub.
2. Agro EcoEnergy and others v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
3. Symbion Power and others v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
4. Saab v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
5. Winshear v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
6. Nachingwea and others v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub

Kutokana na hali hii, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria inapaswa kutoa taarifa kwa Watanzania kupitia Bunge ili kueleza hatua mbalimbali za mashauri haya, na sababu za kushitakiwa na pengine kiasi cha fidia ambacho tunaweza kulipa endapo tutashindwa.

Tanzania pays treaty award to avoid aircraft seizure ....​

Global Arbitration Review
https://globalarbitrationreview.com › ...
Tanzania pays treaty award to avoid aircraft seizure

30 Apr 2021 — Tanzania has paid US$22 million to satisfy an UNCITRAL award after the Italian-owned creditors attempted to
 
Hivi comment kama hizi huwa mnatoa bila kufikiri? Beberu gani aje kugombana na nchi omba omba? Yaani hata budget yako unakopeshwa au kupewa tu hlafu u-compete na bebeeru? GDP yako ni ngapi; your trade volume comparison by world standard ni negligible! my foot! kwani google mnaitumiaje; for watching porn!
Nchi za wenzetu zilizoendelea ukigombana na raia mmoja hata kama amevunja sheria ujue umegombana na serikali. Ukimfungia biashara mtu mmoja ni kama umegombana na nchi.

Mugabe aligombana na raia wa uiengereza akachukua mashamba akawapa wenyeji. Mpaka leo Zimbabwe ipo kwenye kibano tena sio na uingereza tu ni pamoja na marafiki zao. Hao ndio mabeberu.
 
Back
Top Bottom