Shida nini tena jamani? Nani hao wasio na nia njema na taifa hili?
Tabia zetu za kutofuata katiba na sheria, zimetujengea mazoea za kutoheshimu hata mikataba.
Serikali inatakiwa kubadilika, ijenge utaratibu wa kuheshimu katiba, sheria, kanuni na mikataba. Serikali na taasisi zake na viongozi, wamezoea kutofuata katiba, kuvunja sheria, kanuni, taratibu na kutoheshimu mikataba. Wanafanya hayo yote kwa jeuri ya dola, hawajui kuwa ujeuri huo hauvuki mipaka ya nchi.
Inatupasa wananchi tukemee tabia za ujeuri wa viongozi wa Serikali ili Serikali ibadilike, iendane na Dunia ya watu wastaarabu kuliko kuendelea kulea hizi tabia za guchiro republic.
Unafikiri kama yale mambo ya hovyo ya kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, kesi ya kumbambikia Mbowe ya ugaidi au kumtwanga risasi zaidi ya 30 Lisu, au kumpoteza Kanguye, Azory Gwanda na Sanane, kama wangekuwa watu wa mataifa mengine, fidia yake ingekuwa bilioni ngapi?
Japo Serikali imezoea kudhulumu haki mbalimbali kutokana na mazoea ya miaka mingi, sasa ibadilike, iheshimu mikataba, ndiyo tabia ya watu wastaarabu.