Ndege ya Tanzania yakamatwa nje, Taifa ladaiwa bilioni 380 kwa kuvunja mkataba bila utaratibu

Nidandie kwenye hoja yako hii, nami niongeze maswali:

Hii ardhi aliyonyang'anywa huyo mwekezaji wa sukari, ni hiyo hiyo aliyopewa Bakresa?

Je, huko kwa Bakresa hapakuwa na wananchi waliokuwa wakilima mashamba yao?

Bomba la mafuta ya Uganda linapata shida kupata pesa, kwa vile wananchi wanadaiwa hawakupewa haki zao stahili, je hawa Waswedi wao maswala ya wananchi hayakuwahusu, au ndiyo 'double standards' zinazotegemewa?

Sasa tumekubali kujisalimisha kwa hawa wakubwa, lakini naona bado haitatosha, tutakamuliwa hadi tone la mwisho la damu.
 
Ndege ya ATCL imezuiwa nchini Uholanzi kwa amri ya mahakama ya ICSID (Hii ni Mahakama inayoshughulikia migogoro ya uwekezaji ya Kimataifa). Ni mahakama iliyopo chini ya Benki ya Dunia.

Amri hiyo ya mahakama ya kuzuia ndege ya ATCL aina ya Airbus 320 ambayo ni mali ya walipakodi wa Tanzania - imetolewa baada ya kampuni ya EcoDevelopment ya Sweden kushinda shauri dhidi ya serikali ya Tanzania, ikidai fidia ya Dola za Kimarekani Milioni 165 (TZS Bilioni 380). Madai hayo yalitokana na kitendo cha Serikali ya Tanzania kufuta hati ya umiliki wa ardhi mjini Bagamoyo ambapo kampuni ya EcoDevelopment iliwekeza kwa miaka 10, mradi wa kuzalisha Sukari, Umeme na Mafuta.
------

Habari ya hii kesi ni nzito, na serikali imekata rufaa lakini bado haijaajiri kampuni ya sheria ya kuitetea. Mwanasheria mkuu Eliezer Feleshi hajato taarifa zote. Lakini hii kesi ni nzito. Kuna mashirika makubwa kama Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrka nk.

Tuendelee kufuatilia.
 
LOoooh, mkuu, nawe hapa umejikunja na kujisikia umejitutumua sana kwa haya uliyoweka hapa?

Hivi wewe huoni utajiri uliopo hapa, ambao watu kama wewe mmelaza akili kabisa kama maiti; na kudhani kwamba wengine wote duniani hawauoni?

Hebu tafakari vizuri andiko lako hili, tena naona kuna misukule wenye akili mbovu na wao wanakuunga mkono hapa!
 
Tatizo ni utaratibu uliotumika kufuta umiliki haukuzingatia mkataba wa mwekezaji na Tanzania. Kumbuka kuwa Magufuli alikuwa na haiba ya kufanya maamuzi ya kibabe. Kwani mwaka 2007/08 alipokamata meli ya uvuvi akiwa Waziri wa uvuvi wewe Mayor Quimby ulikuwa wapi?

Kuna vile vipengere ambavyo Tanzania haiku tekeleza hususan kwenye mazingira, hivyo ikapelekea yeye kutoendeleza hilo shamba.
 
Nikajua ndege mnama hawa njiwa kumbe pipa
 
Wangekamata kimbinyiko na Sai Baba mbona mapema2 tungeandamana! Iyo mbanga wacha2 wakae nayo uko, sisi dola1 kwa cku hatuna ndoto ya kuisogelea hilo dubwana achilia mbali kuipanda
 
Uholanzi kwa kiswahili kwajina jingine inaitwaje?..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…