Ndege ya Tanzania yakamatwa nje, Taifa ladaiwa bilioni 380 kwa kuvunja mkataba bila utaratibu

Laiti JPM angekuwa hai leo naamini angeongea jambo kuhusu haya yanayotokea sasa. Haya naombeni hili nalo mkalitizame!
 
Formula ya trab na trat haiwez kuaply hapo tukaikomboa?
 
Unatakiwa useme huo utaratibu ambao aukuzingatia sheria.

Ina maana hatuna sheria unayosema raisi ndio main custodian wa ardhi na ana mamlaka ya kuipangia matumizi.

Kama tuna sheria ya namna hiyo basi raisi akuvunja mkataba kimakosa ana mamlaka hayo, ilo sasa ni jukumu la mwekezaji kujua.

Ata ingetokea shamba tayari lishaendelezwa raisi bado ana mamlaka ya kufuta mkataba only that customary kwenye mkataba wa matumizi ya ardhi hasa kwenye kilimo utalipia fidia ya gharama za mazao yanayotarajiwa kuvunwa as stated in ‘Hutton v Warren (1836).

Na basic rule ya kulipa damages ni kumrudushia mtu hasara iliyowazi kwa kuvunja mkataba, sasa wewe unaweza justify hizo $165 million dollars kwenye mkataba wa kilimo.

Mkataba wenyewe bila hata ya kutumia sheria zozote nimekuwekea vigezo vya implied term awali vinavyoweza vunja mkataba kuna hiyo ‘business efficacy’ (officious bystander test). Hiyo test inatumiwa kumuuliza neutral party kama huo mkataba ni sahihi, zingatia eneo lilikuwa linatumiwa na wakulima na serikali ilikuwa aijawatoa, eneo lipo ndani ya hifadhi na mgogoro ulishafika mpaka bungeni.

Je katika mazingira hayo kutuliza munkari raisi anaweza tumia nguvu yake kubadili matumizi ya ardhi, ata huko ulaya watakwambia sawa especially zama hizi ambazo kampuni zina pressure kubwa huko kwao kwenye sustainable environment na ujirani mwema na locals.

Ni hivi kesi huwa tunashundwa sisi huko kwa mabeberu, halafu tunaishia kuambiwa details za kesi ni siri.
 
Lengo la arbitration ni kutafuta neutral hearing ground and in most cases judges are supposed to have previous expertise on the industry kutokana ugumu wa baadhi ya case.

Lakini ata huko kwenye arbitration details za contract terms zina apply vilevile kama vile kesi Ingesikilizwa nchi husika; sio kwamba kuna legal definition zao.

Kwa ivyo kama kuna contract dispute ya kulima imefanywa ndani ya Tanzania na statute law inasema raisi ndio custodian wa ardhi mwenye uwezo wa kubadili matumizi yake, that will be considered part of the contract term Kwenye arbitration yoyote duniani regarding that particular case.

Je mwekezaji hana haki ya madai ya hasara baada ya raisi kubadili matumizi ya ardhi, yes lakini sio kwa kiwango icho kwa sababu hakuna chochote alichofanya not mention eneo lenyewe lilikuwa na mgogoro tayari enough reason to terminate its usage kuwaridhisha wenyeji.
 


Viongozi wetu watapona? Kuna siku viongozi watatiwe kizuizini huko nje mpk deni lilipwe.
 
Hawachelewi kusema; 'Ni stori za mitandaoni tu, wananchi mzipuuze'.
 
Tati,o arbitration process ilitoa nafasi kwa Tanzania, Tanzania haikufuatilia kwa wakati, mpaka mahakama ikaamua.

Pia, maofisa wa serikali wanasema Tanzania ina asset nyingi, inaweza kulipa. Yani hata hawaoni kuwa hili ni tatizo.
 
Acha waichukue tu hamna Cha maana kwenye Hilo kopo la kibwengo
 
Jitahidi habari iwe kamili maana ipo nusu na haisemi imekamatwa wapi, kwa kosa gani, hilo deni linatokana na nini?
WEW kummbe kingereza Ina kushida mbna mleta mada ameeleza vzr tu acheni kukurupuka jmn someni Uzi vzr kwa kutulia

Kumbee ndio nyie mnataka kufaulishwa laws school [emoji41] bila kusoma pole Sana

Rudia kusoma
 
Mbna majanga jmn
 
Ndege ni mbovu hiyo Wazungu wamestuka hawatauza hiyo ndege watakamata kitu kingine siku za mbeleni labda Tanzania walipe.
 
Tati,o arbitration process ilitoa nafasi kwa Tanzania, Tanzania haikufuatilia kwa wakati, mpaka mahakama ikaamua.

Pia, maofisa wa serikali wanasema Tanzania ina asset nyingi, inaweza kulipa. Yani hata hawaoni kuwa hili ni tatizo.
Hao watu wa serikali akili zao huwa zinawatosha wenyewe.

Bongo wanasheria waliobobea wapo private, serikalini wengi tia maji tia maji.

Binafsi nikitaka clarification ya what the law implies kupata maelezo rahisi ya interpretation huwa naenda Jaba Shadrack blogspot ndio wanadadavua vizuri, but so ante other private law firms.

Huko serikalini lawyers wa kweli wachache.
 
Mwasisi wa haya yote ni Jiwe
Jiwe ndiyo ali sign hiyo mikataba ya Kifisadi!? Au Jiwe ndiyo alikua anajaribu kupambana na hiyo Mikataba yenu ya Kifisadi mliongia Kama vile hakuna kesho tena!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…