Ndege yatua kwa dharula baada ya mtu mmoja kusema 'Allahu Akbar'

Ndege yatua kwa dharula baada ya mtu mmoja kusema 'Allahu Akbar'

Inaeleweka hiyo ni adhana hakuna mtu atatishika. Lakini ikitokea ndani ya ndege tena iko angani ni lazima italeta taharuki hasa baada ya yale yaliyotokea September 11 mwaka 2001.
September 11 walisema Allah akbar?
 
Abiria wa ndege ya shirika la easyJet waliokuwa wakisafiri kutoka Luton, Uingereza kwenda Glasgow, wamejikuta katika hali ya taharuki baada ya mwanaume mmoja kusimama katikati ya safari na kudai kuwa alikuwa na bomu ndani ya ndege hiyo.

1753702377364.png
Tukio hilo limeibua hofu kubwa miongoni mwa abiria, baada ya mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 41 kupaza sauti kwa kusema, “Simamisha ndege. Tafuteni bomu ndani ya ndege. Kifo kwa Marekani. Kifo kwa Trump.” Pia alisikika akirudia maneno ya Kiarabu ‘Allahu Akbar’ yenye maana ya Mungu ni mkuu.

Video ya tukio hilo, ambayo kwa sasa inachunguzwa na maafisa wa kupambana na ugaidi, inaonesha jinsi abiria walivyomdhibiti mwanaume huyo, ambapo abiria wengine walimpekua kutafuta vitu vyovyote hatarishi huku wakimhoji kuhusu madai yake, na iwapo alikuwa ametumia pombe au dawa za kulevya.

Mwanaume huyo alikamatwa na polisi mara baada ya ndege hiyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Glasgow.
 
Aisee kila nikisoma hii thread nacheka sana!
Imagine jamaa walivyo pink, halafu jamaa from nowhere anapiga yowe, ALLAH AKBAR!
MZUNGU DAMU ITAMJAA USONI MPAKA ATAFANANA KAMA JEZI YA SIMBA!
😅😂🤣
Mbavu zangu!
😅😂🤣😭
 
Back
Top Bottom