Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Sijafahamu hizi chuki za baadhi ya watanzania kwa nchi yao zinawasaidia nini hasa?!
 

I know nothing in this industry, you would rather stay quite, since you are an empty set on this Industry.
 

Hebu weka pato la Tanzania na Kenya kwenye utalii, kisha tuendelee na huu mjadala wako. Hapa suala sio wingi wa vivutio vya utalii, bali ni jinsi gani umejipanga kwenye sekta hiyo. Nasubiri kwa hamu uweke mapato baina na nchi hizi mbili. Tena ukiweza weka miaka hii mitano ili uwe na nafasi nzuri ya kutetea usemacho.
 
Ulisikia taarifa ya familia lakini kuhusu sababu ya kifo cha mkuu,au wewe ni mke mdogo wa marehemu una taarifa yako?
 
wakenya si ndugu zetu wala wenzetu fahamu hilo, hawa jamaa walituon sisi ni wajinga na hatuna maendeleo hivyo wanaweza kufanya wanavyotaka sasa mambo yanaenda yanabadilika inawasumbua sana na kuzuia hawawezi.
 
sasa wao siwameamua kukumbatia ugonjwa kwa ajili ya misaada shauri yo bwana

Kwa sababu kila mtu ana yake sidhani kama tunayo haki yoyote ya kuwasemea wala kujinasibu na sababu za kwa nini wao, kwa nini vile.

Wamesema wao kuwa wamekumbatia ugonjwa ili wapate misaada au ni ufukunyunyu wetu tu?

Kama sisi hatujaukumbatia ili tusipate misaada hilo ni letu tuhangaike nalo.

Haieleweki kwa nini tunakwazika na maamuzi yao.

Kama wao Corona ni ugonjwa na sisi Corona si ugonjwa sidhani kama inawahusu.

Kinachotuhusu ni je Corona ni ugonjwa? An internal issue. Usisahau pana waliopoteza wapendwa. Pole pole mkuu.
 
I know nothing in this industry, you would rather stay quite, since you are an empty set on this Industry.

Wewe ndio unatakiwa ukae kimya. Na kama kitu unahitaji ujifunze uwe mpole utapata shule nzuri tu mkuu. Haya mambo hayaitaji mihemko wala hisia kuyazungumzia. Yanahitaji facts, sio maneno.
 
hapo ulipo kuna taarifa yoyote ya mgonjwa au kifo kwa ajili ya corona?
 
Cha ajabu wanaoteseka na marufuku wa Kenya ni Wachaga, na Wachaga hapo hao ndiyo waliojazana hapa kushangilia, Wachaga wamejazana Kenya huko wanauza mboga na mitumba, watakula wapi?

Low IQ!
 
hakuna wakati sisi ka tanzania tumesema corona si ugonjwa, tulisema ni ugonjwa na upo na takwimu zilikuw zinatolewa na wizara husika na watu waliumwa na wapo waliopoteza maisha, shule na vyuo vilifungwa lakini kwa sasa hatuna ugonjwa huo ndo maana tumefungua shule na mambo mengine yanaendelea, kama wewe hutaki kusikia kenya wanakumbatia ugonjwa kwa sababu ndo masharti ya misaada waliyopokea basi.
 

Wewe jamaa kweli ni mweupe kwenye sekta ya utalii. Kwa mapato ya utalii kenya haijawahi kuifikia Tanzania hata mara moja. Hilo liko wazi mkuu.
 

Corona free country.

Ndiyo maana wanatunyanyapaa. Hata huko mipakani Tunduma, holili, Namanga, sirali, mutukula, kabanga, rusumo nk nchi zinazowakuta madereva wetu na huu ugonjwa ni kutuonea gere tu. Sisi ulikwisha zamani sana.

Tuwashitakie kwa Mungu.
 
Wewe ndio unatakiwa ukae kimya. Na kama kitu unahitaji ujifunze uwe mpole utapata shule nzuri tu mkuu. Haya mambo hayaitaji mihemko wala hisia kuyazungumzia. Yanahitaji facts, sio maneno.

Kaa kaa kutulia tafadhali usije ukaishia kuchekesha walionuna.
 
Kenya sio pahala salama kwa ndege zetu kutua huwenda abiria wakaambukizwa ama kuhamisha Covid-19/kutoka Kenya kupeleka kwengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…