Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Sijafahamu hizi chuki za baadhi ya watanzania kwa nchi yao zinawasaidia nini hasa?!
 
I have more than 15yrs in tourism industry and hospitality, what do you have in this sector?

kenya kwenye utalii haiwezi kusimama yenyewe wala kuwa na sauti bila kuitaja TZ. na pia KQ ndio iliwabeba sana maana inashirikiana na mashirika makubwa hivyo watalii wanapitia kenya sababu hiyo.

I know nothing in this industry, you would rather stay quite, since you are an empty set on this Industry.
 
Watalii wengi wa TZ wanakuja na mashirika ya KLM, Ethiopian Airline, Emerate, Dubai Air etc ambayo yana direct flights to KIA Airport na yote hayo yalishaanzisha safari kuja TZ. Sasa hawa Kunyaland wanatutisha nini wakati walishajaribu kuzuia Shuttle Bus zetu kwenda kuchukua watalii pale JKIA lakini hawakufaulu baada ya kuona KLM imeanzisha direct flights from Amsterdam to KIA then DAR and Back to Amsterdam hapo awali ilikuwa inateremka Nairobi then KIA. Kwa taarifa yako hawatubabaishi kabisa na kuhakikishia tukifunga mipaka na Kenya tutapata watalii wengi zaidi kwa kuwa hata hao wanaanzia Kenya lakini destinations zao nyingi zinakuwa TZ kupanda Mt. Kilimanjaro, kuona pia Ngorongoro, Serengeti na Zanzibar pia. Tulipowabana kwenye madini ya Tanzanite na Dhahabu sasa wanapumulia mipira!!

Hebu weka pato la Tanzania na Kenya kwenye utalii, kisha tuendelee na huu mjadala wako. Hapa suala sio wingi wa vivutio vya utalii, bali ni jinsi gani umejipanga kwenye sekta hiyo. Nasubiri kwa hamu uweke mapato baina na nchi hizi mbili. Tena ukiweza weka miaka hii mitano ili uwe na nafasi nzuri ya kutetea usemacho.
 
Inajulikana wazi kuwa kingozi wetu wa zamani amekufa kifo kinachoashiria COVID 19. Sasa acheni Kenya wajilinde. Sisi hatupimi na hatufuatilii wagonjwa.

Mtu mkubwa kafa with unknown clinical observations and case definition. Unategemea nini. Nkurunzinza ameondoka hapo Burundi ilikuwa hivyo hivyo, baadae sisi. Na ndio maana msibani hawakufika wanajua kinachoendelea hapa kwetu.
Ulisikia taarifa ya familia lakini kuhusu sababu ya kifo cha mkuu,au wewe ni mke mdogo wa marehemu una taarifa yako?
 
Ndugu yako akiwa na mapungufu, wa kwanza kumsitiri ni nani kati ya watu wa mbali au wewe ndugu yake!?

Wakenya hawakupaswa kuitangazia dunia jambo kama hili! Walipaswa kudeal na sisi kindugu yaan kaka yako anaumwa UKIMWI na kweli alifanya umalaya kwa makusudi lakini ni lazima umuuguze!
wakenya si ndugu zetu wala wenzetu fahamu hilo, hawa jamaa walituon sisi ni wajinga na hatuna maendeleo hivyo wanaweza kufanya wanavyotaka sasa mambo yanaenda yanabadilika inawasumbua sana na kuzuia hawawezi.
 
sasa wao siwameamua kukumbatia ugonjwa kwa ajili ya misaada shauri yo bwana

Kwa sababu kila mtu ana yake sidhani kama tunayo haki yoyote ya kuwasemea wala kujinasibu na sababu za kwa nini wao, kwa nini vile.

Wamesema wao kuwa wamekumbatia ugonjwa ili wapate misaada au ni ufukunyunyu wetu tu?

Kama sisi hatujaukumbatia ili tusipate misaada hilo ni letu tuhangaike nalo.

Haieleweki kwa nini tunakwazika na maamuzi yao.

Kama wao Corona ni ugonjwa na sisi Corona si ugonjwa sidhani kama inawahusu.

Kinachotuhusu ni je Corona ni ugonjwa? An internal issue. Usisahau pana waliopoteza wapendwa. Pole pole mkuu.
 
I know nothing in this industry, you would rather stay quite, since you are an empty set on this Industry.

Wewe ndio unatakiwa ukae kimya. Na kama kitu unahitaji ujifunze uwe mpole utapata shule nzuri tu mkuu. Haya mambo hayaitaji mihemko wala hisia kuyazungumzia. Yanahitaji facts, sio maneno.
 
Nchi zote mbili zinategemeana na nitakupa mfano. Kenya wanaitegemea Tanzania kwa abiria wake kusafiri na KQ kutokea JKNIA hadi Nairobi na hatimaye kuunganisha kwenda wanakotaka pia Tanzania inaitegemea Kenya kwa kukuza mapato pale ambapo ndege zake zinapotua katika viwanja vyake.

Ila kwa ishu ya Corona ilivyochukuliwa Tanzania sitashangaa kuona tunapigwa ban zaidi na kuathirika pakubwa. Nadhani ulisoma pia tangazo la nchi ya Dubai kuhusu watanzania wanaotaka kuingia huko kuanzia kesho. Kenya ingetaka kufanya usanii kama sisi wala wasingeshindwa ila walijiangalia hasa kwenye mambo ya usafiri wao wa anga na utalii ikabidi wawe wazi ili hata itakapoanza kupungua Corona then takwimu ziwe za wazi pia.

Sisi ni kama tulichekesha tena kichekesho cha kitoto pale ambapo usiku mmoja tulikuwa na cases zaidi ya 500 na vifo 16 halafu ghafla hakuna tena kitu au tangazo lenye data zilizothibitishwa kutoka wizarani! Hicho ni kichekesho tena cha aina yake mkuu.
hapo ulipo kuna taarifa yoyote ya mgonjwa au kifo kwa ajili ya corona?
 
Cha ajabu wanaoteseka na marufuku wa Kenya ni Wachaga, na Wachaga hapo hao ndiyo waliojazana hapa kushangilia, Wachaga wamejazana Kenya huko wanauza mboga na mitumba, watakula wapi?

Low IQ!
 
Kwa sababu kila mtu ana yake sidhani kama tunayo haki yoyote ya kuwasemea wala kujinasibu na sababu za kwa nini wao, kwa nini vile.

Wamesema wao kuwa wamekumbatia ugonjwa ili wapate misaada au ni ufukunyunyu wetu tu?

Kama sisi hatujaukumbatia ili tusipate misaada hilo ni letu tuhangaike nalo.

Haieleweki kwa nini tunakwazika na maamuzi yao.

Kama wao Corona ni ugonjwa na sisi Corona si ugonjwa sidhani kama inawahusu.

Kinachotuhusu ni je Corona ni ugonjwa? An internal issue. Usisahau pana waliopoteza wapendwa. Pole pole mkuu.
hakuna wakati sisi ka tanzania tumesema corona si ugonjwa, tulisema ni ugonjwa na upo na takwimu zilikuw zinatolewa na wizara husika na watu waliumwa na wapo waliopoteza maisha, shule na vyuo vilifungwa lakini kwa sasa hatuna ugonjwa huo ndo maana tumefungua shule na mambo mengine yanaendelea, kama wewe hutaki kusikia kenya wanakumbatia ugonjwa kwa sababu ndo masharti ya misaada waliyopokea basi.
 
Hebu weka pato la Tanzania na Kenya kwenye utalii, kisha tuendelee na huu mjadala wako. Hapa suala sio wingi wa vivutio vya utalii, bali ni jinsi gani umejipanga kwenye sekta hiyo. Nasubiri kwa hamu uweke mapato baina na nchi hizi mbili. Tena ukiweza weka miaka hii mitano ili uwe na nafasi nzuri ya kutetea usemacho.

Wewe jamaa kweli ni mweupe kwenye sekta ya utalii. Kwa mapato ya utalii kenya haijawahi kuifikia Tanzania hata mara moja. Hilo liko wazi mkuu.
 
hakuna wakati sisi ka tanzania tumesema corona si ugonjwa, tulisema ni ugonjwa na upo na takwimu zilikuw zinatolewa na wizara husika na watu waliumwa na wapo waliopoteza maisha, shule na vyuo vilifungwa lakini kwa sasa hatuna ugonjwa huo ndo maana tumefungua shule na mambo mengine yanaendelea, kama wewe hutaki kusikia kenya wanakumbatia ugonjwa kwa sababu ndo masharti ya misaada waliyopokea basi.

Corona free country.

Ndiyo maana wanatunyanyapaa. Hata huko mipakani Tunduma, holili, Namanga, sirali, mutukula, kabanga, rusumo nk nchi zinazowakuta madereva wetu na huu ugonjwa ni kutuonea gere tu. Sisi ulikwisha zamani sana.

Tuwashitakie kwa Mungu.
 
Wewe ndio unatakiwa ukae kimya. Na kama kitu unahitaji ujifunze uwe mpole utapata shule nzuri tu mkuu. Haya mambo hayaitaji mihemko wala hisia kuyazungumzia. Yanahitaji facts, sio maneno.

Kaa kaa kutulia tafadhali usije ukaishia kuchekesha walionuna.
 
Kenya sio pahala salama kwa ndege zetu kutua huwenda abiria wakaambukizwa ama kuhamisha Covid-19/kutoka Kenya kupeleka kwengine.
 
Back
Top Bottom