Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Hivi kweli hanuna hata ufa mmoja tunaoeeza kuwafinya ili tuheshimiane,hawa jamaa wanatudharau sana, na Magu aliposema suala la chakula kwenda kwao kipindi kile, waziri wao wa kilimo na chakula alisema wakenya watanunua chakula toka mataifa mengine,sio lazima wanunue Tanzania. Wajinga sana.
Ni kweli watanunua Mexico, Uganda, Zambia na Mozambique.
 
Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC
China ndiko maambukizi yameanza....na imeruhusiwa
 
Mi Hata nashangaa a kwa nini tunahangaikaga na wakenya yaani the way tunavyo behave utafikiri wakenya ni waume zetu wa ndoa halafu anataka kutuacha sasa kwa kuwa wewe mke bado unampenda mme basi unatafuta kila sababu au kosa ili uonekane tu.
Yaani sisi tumebarikiwa majirani wazuri na wengi tu lakini wakenya ndio wanatukosesha usingizi tujipange kufanya biashara na kuwa na strategies ya kupata soko kusini Mwa Afrika na eastern Congo w
 
Hakuna Shaka. Kila mmoja acheze mechi zake. Nasi tutapiga marufuku Ndge yoyote iliyokanyaga ardhi ya Kenya isitue kwetu. Mtalii/Msafiri yeyote anayetamani kufika kwetu asipitie Kenya.
 
Partiner airlines zinakuja hapa! KQ na hizo wanagawiana wasafiri! Ikija BA, kwanini asiwakaie tiketi?
KQ wametangaza kuanza safari za nje, na moja ya nchi wanakokwenda ni Tanzania, yaani Kilimanjaro, Dar, Zanzibar; pamoja na kwamba Waziri Macharia hakuihusisha Tanzania katika nchi zinazoruhusiwa.
How does that still make sense?
 
mkuu samahani hii mambo ya kusema kenya ndugu zetu inanikera kweli, hawa ni jirani tu ambao wanaweza kuwa adui zetu vilevile kama ambavyo imewahi kutokea kwa uganda.
Msemakweli ni Mpenzi wa Mungu.

Watu wanatumia maneno bila ya kuwazia matumizi yake sahihi.
 
Ndiyo maana sijaona faida ya EAC.wivu was kike utawaua hawa.ngoja corona iwachakaze
Hebu tueleze kidogo kwa nini corona inawachakaza wao lakini sisi imepoa!

Au ni kwa sababu ya yale maombi kama tulivyohimizwa?

Hili ni swali makini, usilipuuze mkuu 'ZALENDA'.
 
Ilikua ni suala la mda tu
20200731_214945.jpg
 
Sisi hatuna tatizo kenya ni ndugu zetu wana hasira zikitulia watatambua ukweli na hatuna mpango wa kuwazuia!
Eti ndugu zenu! Damn, you are DISGUSTING!

Hakuna undugu hapo, changamka!

Mmelala lala tu ati ndugu zetu! Hiiiiiiiiiii.....

Biashara za kikanda zenye hujuma zinajibiwa kwa retaliation. Sio kulala tu na kutia tia huruma!
 
Hata wakoma wakati wa kale walikuwa wanjitenga wenyewe tena ukiwakaribia na hujawaona walikuwa wankupigia kelele wakisema sisi ni Najisi

Kwahiyo Kenya iko sahihi kupiga kelele za Unajisi
 
Je, unapata Kila siku taarufa za ukimwi, home ya ini, malaria na kadhalika? Why only Corona?! Na hizo takwimu zikitolewa zitapunguza hiyo Corona?!
 
Hta wale 500 tuliosema wanumwa bado hatujasema kama wamepona .Haaaaaaa
 
Kwahiyo wao ndio wanakaribishwa? Ni kujisahau tu na mambo ya wanasiasa. We either fall apart or grow together. Ngoja tuone nani atakayepoteza
Nasikia tumeishajibu. Kuanzia kesho, Ndege kutoka Kenya marufuku kukanyaga KIA, JNIA wala Zanzibar. Na kama tumewajibu kweli namna hii akili zitawakaa wakenya. Hata hivyo, sifurahii mgogoro na nchi jirani, lakini jirani kama hajielewi hakuna namna ni kumsurubu tu kwa namna tunayoweza.
===
Chakusikitisha mleta mada kaona ni kosa letu Watanzania kwa uamuzi uliofanywa na serikali ya Kenya.
 
Back
Top Bottom