We jamaa tangu April ukionaga story za Corona unashupaza shingo sana. Ulikomaa na lockdown weeeee mpaka ukajiona mjinga. Shule zimefunguliwa tangu July mpaka leo shwari tu. Mmebaki mnaokoteza maneno tu. Last week watu wamejaa uwanja wa Mkapa kumuaga Ila hakuna cha mlipuko wa COVID19 wala nini., Mmejazana airport kumpokea Lissu na hakuna cha COVID19 wala nini. Bado unakomaa na Corona tu????, Huonagi aibu mkuu?.. Tanzania hakuna Corona, kama mnaipenda sana CORONA si muhamie huko KENYA??
Pamoja na kurukia kichwa kichwa (trespassing) hoja bila hodi, Maswali yote yaliyokuwa mule hukuyaona bali kwenda kuandika huo utopolo? Hata aibu kidogo hamna?
Tulikuwapo siyo JKNIA peke yake, bali pia Uhuru na wengine hadi Lupaso achilia mbali waolikwenda Uhuru wasipate nafasi ya kuingia.
Hivyo kwenda JKNIA wala isikupe taabu.
Kote kutatu tuliweza kufika. Wewe unayejidhania kuwa mzalendo sana kuliko wengine uliweza kufika kupi, mburura wee?!
Ungekuwa na hoja ungekuwa umeyajibu maswali yale yaliyokuwa kwenye bandiko ulilorukia. Huna hoja, huna lolote zaidi ya kuwa ni mchumia tumbo, mbinafsi mkubwa usiyekuwa na mbele wala nyuma.
Eti nikajiona mjinga. Nilikwambia hayo au ndiyo ya kujitekenya mwenyewe na kujichekesha mbumbumbu mkubwa wee?!
Nyie ni mzigo na hasara kubwa kwa taifa hili. Haisaidii lolote kuacha kukupeni makavu makavu bila ya kumung'unya maneno.
Hakuna mwenye chembe ya akili mkichwa anayeweza kuthubutu kumtamkia mwingine eti aondoke nchini. Si mburura wewe wala si jiwe.
Haondoki mtu hapa!
Unataka list ya waliokufa kwa corona?
Kupisha magomvi na malalamiko uchwara, list ya wanasheria nguli iliwahi kuwekwa hapa. Ipi unataka, ya vigogo?
Tuokoteze maneno sisi au wewe ndiye mwokotezaji?
Eti hakuna Corona Tanzania - utopolo mtupu.