Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Watalii wao watauangalia mlima Kilimanjaro kupitia darubini,hatutowaruhusu kuingia kupitia mipaka yetu daima labda waruke moja kwa moja kuingia nchini kwetu
 
Wewe una Corona? Umependekeza solution ya kulimaliza ukakataliwa? Nani anasolution nzuri kuliko sisi ambaye amelimaliza tatizo kuliko sisi? Ni lini umepeleka mgonjwa wako wa Corona Hospitalini akakosa huduma?

Acheni kutoa lawama zinazowashushia hadhi. Tunahitaji hoja za msingi zisizo na hila na zenye tija ya kiuleta ustawi wa taifa na zi vinginevyo.

Kwa suala la Corona Tanzania tuko juu kuliko hao wanaofanya visa vya mbaazi. We are far above their level.

Na ujue kama unasema miujiza ya kijinga kwa reference ya kukataa kwamba Mungu hawezi, unatafuta matatizo kwakko na watu wako. Tubu tena uache kujiona una maarifa kuliko Mungu. Huna,


USA wao wanapambana kumaliza janga, siyo kama sisi tunaoamini katika miujiza ya kijinga!
k
 
Wakenya wanafiki tu hapo wanatufanyia kwa vita ya utalii tu na si lolote, japo hili picha ni la kutisha, nahofu sana huko mbeleni nahisi dunia itatutenga!
Busara ikipunguka huongeza migogoro katika jamii.
 
Wakenya wanafiki tu hapo wanatufanyia kwa vita ya utalii tu na si lolote, japo hili picha ni la kutisha, nahofu sana huko mbeleni nahisi dunia itatutenga!

Kama dunia inaweza kututenga kwa nini unawashutumu wakenya kwa unafiki peke yao?

Haiwezekani kuwa dunia yote ndiyo labda ni wanafiki isipokuwa sisi?
 
Kenya kama nchi si tatizo. Tatizo ni Wakikuyu wanao itawala Kenya. Tanzania tusiposhughulikia hili suala kwa umakini sijui. Hapa wanajaribu kututenga na Waganda na Wanyarwanda ambapo nchi hizi tuliwekeza damu za Wazalendo wa nchi hii. Mkikuyu tusipomchukulia kama tulivyokuwa tunawachukulia makaburu wa SA tutakuwa na wakati mguvu sana kama taifa.

Biashara ya utalii hapa inapigwa vita vya wazi. Sisi tusijiingize kuzuia watalii watakao shukia Kenya kuja Tanzania.

Mpango ule wa kuimarisha usafiri kupitia ziwa Tanganyika umewauma sana hawa watu wa utatu.
 
hizi ndege zimenunuliwa kwa pesa halali ya watanzania iliyoidhinishwa kiharamu, kibabe, kinyume na katiba ya nchi. zinakuwa shari badala ya kuwa heri.
 
Heading ya post yako iko exaggerated na ni chonganishi. Kenya haijapiga marufuku nchi fulani fulani. Ila Kenya itaanza kufungua anga lake tarehe 1 August 2020 kwa kuruhusu nchi 11 kwanza ambazo kwa takwimu zimeonekana kuwa zina maaambukizi kidogo. Sasa kupiga marufuku ndege za Tanzania kuna kuja vipi hapa? Dunia ina nchi kama 200 hivi. Katika hizo Kenya imeruhusu 11 tu kwa vigezo fulani. Sasa kupiga marufuku Tanzania kunaingiaje hapa. Tuache uchonganishi... Katika hali ya sasa, kila nchi ina sovereignty ya kufanya kile inachoona kinalinda afya za watu wake.
 
Hizo ndege unazozizungumzia hapa ni lini ziliruhusiwa kutua Kenya hadi wazikataze sasa?

Nchi hii bado adui ujinga ni mkubwa sana. Unadhani wanazuia ndege kweli?? Umeacha mambo ya msingi unazungumzia ndege. Vipi hilo sharti la kupima covid-19 angala masaa 96 ndani ya safari?? Kama sisi tuliacha kupima wagonjwa, tunaweza kupima wasafiri???
 
Air Tanzania doesn’t fly to Kenya na kama magufuli akiamua to retaliate Kenya ndo wataathirika zaidi maana wao wana 5 flights a day kwa week wana 32 flights and 128 flights a month, 1536 flights a year. Sasa nani atakae athirika zaidi japo na sisi tunategemea to collect revenue from KQ flights zinapokuwa zinapofanya safari za hapa nchini.
 
Mambo mengine ni ya kipumbavu mno, unalazimisha tukuite mjinga?

Dunia ina nchi ngapi we jinga?

Na hata hivyo, Tanzania ni nchi pekee mpaka sasa ambayo vyuo pamoja na shule zooote, wanaendelea na masomo! Kwa Neema ya Mungu, wageni wakiingia kwenye anga la Tz hatakama walikuwa na Corona watapona wawapo nchini mwetu

Mwambieni na huyo ndugu yenu asiji karantini, anajisumbua tu na vikao vya Chama chake atavikosa bule na wajumbe wasije wakamchijilia baharini bule kuhofia Afya yake
 
Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC
Kenya kama ni karata hili ni garasha tu halina impact yoyote.
Wamekuwa wahangaika sana na Tz badala ya kuhangaika na corona iliyowakaba koo.
 
Wamechelewa, tuna world class airport sasa. Hivyo wasafiri wanaweza fanya booking za direct flights. Na mashirika makubwa ya ndege yamesha anza kufanya safari zake kuja Tz baada ya kuona hali ni shwari.. kenya will be in a loosing side hasa wale wageni wanaowadanganya wanashukia kenya bhas kutokea hapo kuingia TZ ndio watakapo nyooshwa. Watalegea tu mbona hao wakurupukaji.
Kwani ukishakuwa na world class airport ndo basi tena wageni wanaweza kuingia kutoka popote pale duniani kama kufumba na kufumbua hata kama hakuna direct route kutoka destination husika?!
 
Nchi hii bado adui ujinga ni mkubwa sana. Unadhani wanazuia ndege kweli?? Umeacha mambo ya msingi unazungumzia ndege. Vipi hilo sharti la kupima covid-19 angala masaa 96 ndani ya safari?? Kama sisi tuliacha kupima wagonjwa, tunaweza kupima wasafiri???

Nani kakwambia watu hawapimwi? Mbona wizara inatoa certificate kwa wasafiri ambao wanatakiwa kuonesha hizo certificate nchi wanazofikia? Kama uko Dar nenda Mabibo pale utakuta msururu wa madereva wa masafa wakipimwa corona.
 
Kwani ukishakuwa na world class airport ndo basi tena wageni wanaweza kuingia kutoka popote pale duniani kama kufumba na kufumbua hata kama hakuna direct route kutoka destination husika?!

Yapo mashirika makubwa tu ya ndege yanayotumia viwanja vyetu. Na Tz ndio hub ya utalii hapa EA, direct flight ni kitu cha kawaida tu na pia sio lazima kupitia kenya. wanaweza kutumia Bole na shirika lao lina operate bongo. Ishu ni je KQ ikipigwa pin itakuwaje?. Ukiweka kwenye mzani utaona ni wapi kuna hasara zaidi.
 
Jibu ni moja tu,ndege zenyewe kwa ujumla hakuna faida zipo kama mapambo tu na moja ya sababu tumekosa kiongozi katika hili.

Note!!
Li-Sun-Likali jana katimba stendi ya Ifakara akwaambia waliokuwa wapiga kura wake:Jamani samahanini sikujua kama hawa jamaa wako hivi,
Raia mmoja akamwambia hukuwa unawajua?Nilikupa pilipiki na laki 7 zikusaidie kwenye kampeni hukunrudishia hata jero leo unakuja kuzingua
Si wampige mawe afe
 
Back
Top Bottom