Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

KWANZA ONDOA UPUMBAVU WAKO WA TANGZAZO LAKO LA KIINGEREZA HAPA .SISI TUMEONA NA KUSIKIA KUTOKA KWENYE VYOMBO VYAO WENYEWE VYA HABARI KUHUSU NDEGE ZA TANZANIA KUTORUHUSIWA KUTUA KENYA. PILI, WEWE PEKE YAKO UNAWEZA UKAJUA HIYO LUGHA LAKINI USIDHANI WATANZANIA WENGINE WOTE WALIOBAKI NI WAJINGA,WANAWEZA KUYATAZAMA MAMBO NA KUSOMA KATIKATI YA MISTARI.
MASUALA YENYE MITIZAMO YA KIUCHUMI MARA KWA MARA HUWA NI MAGUMU KUYAELEWA NA HASA KWA WAJINGA WACHACHE AMBAO WANADHANI KUONGEA KIINGEREZA PEKE YAKE NDIYO UNAWEZA UKAENDELEA.HUU NI UJINGA WA KASUMBA TULIORITHISHWA NA WAKOLONI WETU AMBAO HATA BAADA YA KUONDOKA KWA ZAIDI YA MIAKA 50 ILIYOPITA BADO TUNAABUDU LUGHA YAO.
MWISHO, TUNAIMANI KUBWA KABISA KWAMBA JAMBO HILI LITATATULIWA NA NCHI HUSIKA KWA MAELEWANO NA KWA KUHESHIMIANA.

Halafu na wewe uondoe "upumbavu" wako wa kuandika insha ndefu kwa herufi kubwa zote from A to Z...

Sijui shuleni ulienda kusomea upumbavu?
 
Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC

Hii Serikali ya Magufuli inafikiri watu wote ni wapuuzi kama alivo Jiwe na
Wakenya sio wapuuzi kama Watz!!!

Kila siku tunasikia kwenye Matangazo ya media zetu( TV, Radio na Magazeti):kwamba CORONA IPO NA INAUA WATZ WACHUKUE TAHADHARI! Lakini hapohapo Jiwe akisimama majukwaani anasema Tanzania Corona imekwisha!!!HII NU KUWAFANYA WATU HAWANA AKILI.

Kuna Maagizo toka juu yanaelekeza RMOs na Hospitali zote kutotoa taarifa ya wagonjwa wa Covid-19 na RMO yeyote ajijichanganya tu HANA KAZI......!!
Mpaka Sasa hakyna taarifa zozote za Covid-19 Tanzania na mtu akifa na Covid-19 wanataja ugonjwa mwingine wowote...!!!Huku Ni kujidanganya na kudanganyika!!
Wakenya wameshtuka!
 
Halafu na wewe uondoe "upumbavu" wako wa kuandika insha ndefu kwa herufi kubwa zote from A to Z...

Sijui shuleni ulienda kusomea upumbavu?
Nimeondoa 'Upumvbavu wako' mkuu.Samahani sana.
 
Back
Top Bottom