Kufunga vipaza sauti kwenye nyumba ya ibada halafu ikifika saa 10-11 alfajiri unawaamsha watu wote (hata wasio husika na imani yako) ili wakaswali; siyo ustaarabu! Hii inageuka kuwa kero/kelele (noise pollution) kwa wale wasio husika.
Kufungua kanisa kwenye makazi ya watu na kuwapigia mzika kwa sauti ya juu mchana na usiku; na yenyewe ni kero/kelele kwa wasio husika na hilo kanisa!
Kufungua bar kwenye makazi ya watu halafu unapiga mziki kwa sauti ya juu mchana na usiku; na yenyewe inasababisha noise pollution.
Magari kupiga hovyo honi zenye sauti ya juu, na yenyewe ni kero!
Bodaboda kukata yale mabomba ya kutolea moshi, au kuweka vyuma ili kutoa mlio usio wa kawaida na yenyewr ni kero isiyo vumilika.
Kanisa kugonga kengele saa 12 (asubuhi na jioni) na saa 6 mchana kwenye makazi yenye mchanganyiko wa watu wenye imani tofauti; na yenye ni kero/kelele!
Matangazo holela ya mtaani/sokoni/maeneo ya biashara kwa kutumia vipaza sauti; na yenyenyewe yadhibitiwe.
Nini cha kufanya?
1. Kuwepo na sheria ya mazingira ya kuzuia hizi kelele! Kama siyo kuzikomesha kabisa.
2. Teknolojia imebadilika. Zitumike saa, simu, au alarm kwa ajili kujulishana/kukumbushana muda wa ibada/sala.
3. Kuwe na sheria ya kufungwa kwa sound proof kwenye nyumba za starehe kama bar pamoja na majengo ya makanisa ya kilokole ili kuzuia sauti kutoka nje wakati wa kuserebuka.
4. Magari kupiga honi hovyo kwenye makazi ya watu, iwe ni marufuku.
5. Bodaboda zote zilikatwa mabomba ya kutolea moshi, zikamatwe na kwenda kuozea kwenye vituo vya polisi.