Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Wanaanza kwa kukujaza upepo mpaka unajiona umenona, wewe ndio wewe, Mfalme. Wanakulainisha na kukulegeza mpaka miguu inakosa nguvu, huwezi kusimama. Wakianza kuingiza huna cha kuzuia, umekwisha. Kwani michezo yao si tunaijua?! Kila siku tunaisikia na kuicheza, lakini ikifika muda wa kuchambua chali, hakuna tunachoopoa.
“Mimi sio kama wale hakyanani nakwambia, tena wao na mimi hatujuani kabisa. Ninyi ndio wenzangu, uchungu wenu ndio wangu toka niko tumboni mwa mama yangu”. Hivi ni nani aliwaambia hili giza linalotuziba mbele na nyuma sisi tunalependa?! Nani aliwaambia ni sifa kujinadi kuoga kwenye bwawa letu lenye maji ya shubiri?! Ah! Nilisahau, tukiwaona wao wanafanana na sisi tunaamini kabisa kunguru tunaweza kumfuga, vifaranga vyetu vitakua bila wasi wasi, njaa tutaisikia kwa jirani.
Eti ulishawahi kuona wapi mpishi anatayarisha viungo vyake, anapika, kupakua na kukaribisha watu kula lakini hajui kapika nini?! Tena anaungana na sisi kwenye mshangao na kuuliza kwa herufi kubwa “IMEKUAJE PILAU HILI LIMEFIKA MEZANI?” Wala hawatuulizi kama tuna njaa, hawaangalii kama chakula kitakua salama au matumbo yetu yatasalimu amri na kubwaga manyanga.
Mchezo wameshausoma wanatujua nje ndani, wametuweka kiganjani. Wanajua kutubananisha hata tufanye nini wakishalenga hatupindishi. Wanajua tutapiga kelele tu, tukichoka tunavuta shuka maisha yasonga. Tumeshawekwa chapa, vyura, NDIO ZETU!