Ndiyo tuseme kwamba mapenzi yana wenyewe ama?

Ndiyo tuseme kwamba mapenzi yana wenyewe ama?

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Wakuu ebu tuwe wawazi, hivi uko mliko serious mnafeel na kuexperience real love? Maana kwa upande wangu mambo ni bila bila, mapenzi ya kweli naishia kuyaona kwenye movies na kuyasikia kwenye lyrics za nyimbo.

Kuna muda nasikiliza nyimbo mpka nawaza kwamba hivi vitu kweli vinatokea na watu wanapendwa kwa kiwango hiki, au ni kwamba natafuta kitu ambacho ni immaginary?

Naandika yote haya ili pengine niweze kujitune niendane hali halisi, kuna muda unakutana na mdada unatia nia, ila baada ya muda unaona kabisa inaektiwa..kifupi unaona kabisa namna unavyotumika kwa ajiri ya maslahi yake ya kiuchumi, wengine wanakuwa wawazi toka mwanzo kwamba "mimi ukinihudumia tu nitakupenda".

Bado nauliza je mapenzi ya kweli yapo, au huwa ni maigizo tu. Je ninachokitafuta naweza kukipata au napoteza muda, kuhusu kuwa na mwanamke nisiyempenda na kuwa na hisia nae nilishajaribu mpka kukaa naye nikiamini nitampenda mambo yakawa kinyume kabisa, kadri siku zilivyoenda nilizidi kumchukia.

Je mapenzi ya kweli yapo? Na kama yapo ni kwamba tukubali kwamba mapenzi yana wenyewe?

Huwezi pata wa kukupenda kiwango unachokitaka kama wewe mwenyewe hujajipenda kiwango hiko...

Wewe unajipenda kiwango gani?
Wanaokutazama wanaona kweli huyu mtu 'anajipenda'..

Ukijichukulia poa kila mtu atakuchukulia poa..
Ukijipa standard ..na watu watakupa standard..
 
Mimi nataka utii na heshima tu. Mapenzi hayanisaidii.

Mkuu unataka mtu ainvest muda wake kwako for nothing in return? Hutaki kuhudumia?

Huduma zinaenhance hisia aiseee....
 
Jipende ww mwenywe. Mtafute anayeonyesha anakupend mchukue ila usiwekeze upendo wote kwake.
 
Mapenzi ya kweli yako mkuu.omba Mungu ukutane na mtakae endana nae na kuchukuliana.
 
Mimi nataka utii na heshima tu. Mapenzi hayanisaidii.

Mkuu unataka mtu ainvest muda wake kwako for nothing in return? Hutaki kuhudumia?

Huduma zinaenhance hisia aiseee....
Kuhudumia sikatai, ila kunapokuja kama exchange ya kupendwa inaleta ukakasi kidogo, kwa mfano huyu aliyeleta hayo masharti ni kweli alikuwa moyoni, ila siku ambayo nilistop kumpa hela ili nione uelekeo na mapenzi yaliishia hapo!
 
Sasa unamjaribu binadamu mwenzio ya nini? Alikuwa na tatizo?

Why f^ck up a good thing?
 
Huwezi pata wa kukupenda kiwango unachokitaka kama wewe mwenyewe hujajipenda kiwango hiko...

Wewe unajipenda kiwango gani?
Wanaokutazama wanaona kweli huyu mtu 'anajipenda'..

Ukijichukulia poa kila mtu atakuchukulia poa..
Ukijipa standard ..na watu watakupa standard..
Umejipa standards na mwenzako akajipa standards kutakua na mapenzi?

Hii theory yako ni ngumu ikija katika real life.
As you will notice standards ni surefire way of dying alone.
 
Back
Top Bottom