Ndoa ambazo mke anampenda sana mume hazidumu. Kwasababu.......

Ndoa ambazo mke anampenda sana mume hazidumu. Kwasababu.......

Kusema ukweli hakuna mwanamke anayevutia kama yule ambaye ukimwambia jambo la masilahi na tija au faida, hata kama hakulielewa ila anachagua kukusikiliza bila chembe ya kubishana au kwenda kinyume na wewe.

Unajikuta ukimuona ni kama umeona female version yako. Unamuona ni upande wako wa pili ambao ulikuwa unautafuta sasa umeupata. Na hapo unajikuta kuna mambo akikwambia hata kama haujalielewa au kulipa umuhimu unajikuta unalifanyia kazi kwa moyo wote bila ubishani au kumvimbia.

Sasa hawa tunakutana nao wapo kinyume kabisa na mafunzo ya mahusiano. Wao wanayaview mahusiano kama aina ya sehemu ya mashindano na kufanya vile wanajitakia hata kama haipo sawa.

Imagine unamwambia mwanamke mimi sipendi wale marafiki zao unao hang nao wanaonekana hawajielewi kwanza hawana mahusiano serious watakupotosha na kikupoteza, yeye anakujibu kwahiyo unanichagulia marafiki na hautaki niwe na marafiki, mbona wewe sikuchagulii marafiki?!

Una amua kukaa kimya tu ili kuepusha mazungumzo yakukaraisha. Fast-forward miezi michache unakuja gundua alitongozwa na mojawapo ya wanaume wanaohang na hao marafiki zake mademu wadangaji, na marafiki zake wanapambana kumuungisha kuwa akubali kuwa mpango wa kando kwa siri na wewe hautagundua.

Unafuma hizo, unamhoji kuwa si nilishakujuza kuhusu hawa rafiki zako kuwa sio watu wazuri, anakutazama yale macho ya "eeeeh basi jamani si umeshanibamba nisamehe tuishi kwa amani".

Hapo ndipo wanaume wanaona ni ufala kuheshimu hisia za mwanamke au kuishi nae pekee yake bila kumchanganyia mahusiano ya michepuko.
 
hehehe, na ubaya ni kwamba mnalinganisha maandiko na maisha ya sasa na wakati hata hao wanawake Wenyewe hawana hofu ya Mungu
 
Vice versa is true,sisi tupo field kabsa mwanamke akikupenda utaishi kwa furaha sana maisha yako yote ya ndoa!
Nadhani wewe haujaelewa lugha ya kisaikolojia aliyotumia mleta mada. Ni ngumu kuwa mwanamke anapenda the very same way mwanaume anapenda hilo haliwezekani.

Mwanaume ndie anapenda mwanamke anamkubali, kumtii na kumeshimu mwanaume anaekuwa nae.

Ukiona mwanamke anakaa na wewe na hauna kitu usiite kupenda ile ni kukuheshimu na kutii maono yako ndio maana anabakia na wewe.

Sisi wanaume ndio tunapenda mwanamke na kusacrifice pesa na mali zetu ili wao wafurahi si kwasababu ya kupata lolote.
 
yeye anakujibu kwahiyo unanichagulia marafiki na hautaki niwe na marafiki, mbona wewe sikuchagulii marafiki?!
Mwanamke huyu hafai. Mwanaume alikosea tangu mwanzoni. Alipaswa kuutafiti na kuupima utii wa mwanamke huyu kabla ya kumuoa.

Mpe kazi ama maagizo ya kukarahisha uone kama atatii na kuyafanyia kazi. Hapo utaubaini utii wa mchumba
 
Utii unatokana na kutimiza majukumu. Tatzo hawa wa sasa nadhani wana list ndefu sana ya majukumu kwa vijana wa leo.

UKISOMA mada za humu inaonekana Wanataka pesa, hela, fedha, chapaa, umpende, umdekeze na usiwe na maumbile madogo ndo angalau kidogo labda utamfaa.
 
UKISOMA mada za humu inaonekana Wanataka pesa, hela, fedha, chapaa, umpende, umdekeze na usiwe na maumbile madogo ndo angalau kidogo labda utamfaa.
Mara zote Haiwezekani mtu akawa amejaaliwa vyote.
Mwenye hela ana kibamia
Mwenye kibamia ana hela
Mwenye 6 packs ni mjinga, mlevi na mgomvi.
Mwenye hofu ya Mungu ana hofu ya maisha kila siku.
 
Ila na nyie hamna msimamo mara mileage inasoma mno. Mnataka nini aiseee
😊😊 Inategemea ntu na ntu, mfano mie kikubwa utelezi tu, sina vigezo vingiii kivile, utelezi upo inatosha mambo ya kuchagua chagua tunawaacha newcomers
 
Vice versa is true,sisi tupo field kabsa mwanamke akikupenda utaishi kwa furaha sana maisha yako yote ya ndoa!
Ila ili ndoa ama mahusiano yadumu ni lazima mwanaume awe anayependa zaidi kuliko mwanamke.

Mwanaume ana uwezo nachorale wa kumfanya mwanamke ambae hamoendi ampende ila mwanamke hana, so kama mwanaume hampendi mwanamke, hakuna namna mwanamke atafanya mwanaume ampende na hivyo hayo mahusiano hayawezi kudumu.

Injini ya mahusiano yoyote ili yaweze kudumu ni lazima mwanaume awe anapenda zaidi ya mwanamke.

Wanawake wengi huishia kulia kwa sababu huingia kwenye mahusiano na wanaume wanaowapenda wao, sio wao kupendwa na hao wanaume, hii ni big mistake.

Kwa mwanamke mwenye akili, date mwanaume anaekupenda.
 
😊😊 Inategemea ntu na ntu, mfano mie kikubwa utelezi tu, sina vigezo vingiii kivile, utelezi upo inatosha mambo ya kuchagua chagua tunawaacha newcomers
Asante studio
Haya sasa baada ya kutoa maoni studio naomba akurudishe ukaketi kidogo😆
 
Mmmm mimi tena sitamani tena kupendwa na mwanamke hawa watu upendo wao ua sio wakudumu kabisa anaweza kukupenda leo kesho kukatokea mwanaume mwingine mwenye sifa kama zako akampenda pia
Kwa ufupi upendo wa mwanamke haunaga msimamo basi
Kila mwanamke ana vitu vyake anavyovipenda kutoka kwa mwanaume kama unavyo technical umeuteka moyo wake
 
Mmmm mimi tena sitamani tena kupendwa na mwanamke hawa watu upendo wao ua sio wakudumu kabisa anaweza kukupenda leo kesho kukatokea mwanaume mwingine mwenye sifa kama zako akampenda pia
Kwa ufupi upendo wa mwanamke haunaga msimamo basi
Ukiona hivyo ujue alifata vitu fulani fulani kwako na si kwamba alikupenda,mwanamke akikupenda kweli hababaishwi kirahisi huko nje.
 
Ukiona hivyo ujue alifata vitu fulani fulani kwako na si kwamba alikupenda,mwanamke akikupenda kweli hababaishwi kirahisi huko nje.
Hii habari ya mke kumpenda mwanaume ndiyo mm mleta mada naikataa. Haipaswi kuwa kigezo cha ndoa.

Ningekuelewa kama ungesema huyo mwanaume hakumpenda na kumheshimu mwanamke
 
Back
Top Bottom