Ndoa: Baba Mchungaji anawakumbusha vijana wetu wa kike na wa kiume misingi imara kwa mahusiano na ndoa imara

Ndoa: Baba Mchungaji anawakumbusha vijana wetu wa kike na wa kiume misingi imara kwa mahusiano na ndoa imara

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Hii mambo ya vijana kuchukuana na kuanza maisha bila kutushirikisha wazazi imekaaje?

Binti unajiskiaje kuishi na mtu asiyejulikana kwenu?

Kijana wa kiume unapata amani kuishi na binti bila kufuata taratibu? Ni kushindwa kulipa mahari au kushindwa kujua faida za kufuata taratibu?

Wazazi tunalionaje hili? Tunawaongozaje watoto wetu kwenye malezi na maisha ya mahusiano?

Je, vijana kufuata taratibu kunaweza kusaidia kujenga familia bora na kupunguza majanga yanayotokana mahusiano kwa jamii? Au ndio utandawazi watoto hawaulizi wala kuulizwa?

Nimempenda sana huyu kamanda wa police chang'ombe. Mwanamke wa shoka huyu ameongea bila kumungunya maneno wala kupepesa macho😍🇹🇿🙏 Mwenye namba zake anipe tafadhali

#MtotoMleeAkimjuaMungu😍📿📖🕍💒⛪🕌🕋🙏

Cc Extrovert mkorinto Jokajeusi Carlos The Jackal Tate Mkuu Asprin Bujibuji
 
Wanawake wa Leo hawaeleweki kabisa hata ukimuuliza unamtu , umeolewa huku anakuona Una pesa anakujibu ndiyo lakini si kiivo[emoji23][emoji23]

Wanaume nao hawaeleweki ana mademu wanne watano ukimuuliza anasema anasimilizia Kwanza[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]

Haya mambo haya.......
 
Wengine mahari inatushinda tunakomolewa na nyie wazazi na binti kuniacha hawezi anaamua ajisogeze mwenyewe
 
Misingi ikiharibika mwenye haki atafanya nini. ZABURI 11:3

Tunakosea kwingi sana kwenye malezi, Sijui ndio umagharibi umezidi au ni kutokujua majukumu yetu kama wazazi na walezi!? Au kutokuwajibika??

Tumekua watu wa kupambania watoto wetu wanaopata mimba warudi mashuleni, kuliko tunavyowapambania wasipate hizo mimba wakiwa bado mashuleni.

Huwa najiuliza, hivi mimi kama mzazi ninayepambana binti yangu amwache mtoto wake mchanga nyumbani arudi kusoma; kile kichanga kinalelewa na nani?

Je mtoto hahitaji malezi, joto na upendo wa mama yake akiwa mdogo?

Kwanini hatuoni kama tunamtesa asiyeweza kujitetea wala kujipigania kwa kumnyima haki yake hadimu kwa kumuondoa mama yake?
 
Hili tatizo ni kubwa sana, linaanzia mtoto wa kike anapoanza maisha ya chuo na kuondoka chini ya ulinzi wa wazazi. Inawezekana una uwezo wa kumpangishia binti chumba na kumuwekea mahitaji muhimu. Akaja kushawishiwa kuishi na kijana ambae anajiona hana uwezo wa kupanga chumba.

mama D ninafhani mchungaji wako angeanza kuangalia swala la vijana kuolewa bila bikra kwanza, huu ndiyo mzizi wa come and we stay.
 
Mapadre, wachungaji, mashekhe wanatukumbusha kila siku ila kwa asilimia kubwa wazazi na walezi tumeacha kuwajibika.

Tungekua tunawapambania vijana wetu kwenye maadili tukishirikiana na viongozi wa imani kama tunavyowapambania hadi kwa masomo ya ziada (tuition) ili wapate division 1 na GPA nzuri vyuoni tungefaulu kwa kiasi kikubwa

Nimemsikiliza huyu mtumishi kuanzia dakika ya 50 ameongea mengi

Wazazi wapambane kuwaachia watoto wao utajiri na nchi iliyo bora zaidi kuliko walivyoikuta, kinachoitwa maadili ya mapenzi kukiwa hakuna ajira kwa vijana wengi ni utopolo tu.

Hakuna utajiri wa maana na wenye faida bila msingi imara wa maadili.

Na hakuna taifa litakalopata maendeleo bila kuwa na misingi bora ya familia maana huko ndiko kunakotengenzwa taifa la miaka ijayo.
 
Tangu hujazaliwa Ulaya na Marekani ndio wanaongoza kwa talaka na sasa hivi ndio wanaongoza kwa watu wake kuishi bila ndoa na ushoga ambavyo kwako wewe vitu hivyo sio maadili lakini ndio wanaipa nchi yako misaada.
Hakuna utajiri wa maana na wenye faida bila msingi imara wa maadili

Na hakuna taifa litakalopata maendeleo bila kuwa na misingi bora ya familia maana huko ndiko kunakotengenzwa taifa la miaka ijayo
 
Tangu hujazaliwa Ulaya na Marekani ndio wanaongoza kwa talaka na sasa hivi ndio wanaongoza kwa watu wake kuishi bila ndoa na ushoga ambavyo kwako wewe vitu hivyo sio maadili lakini ndio wanaipa nchi yako misaada.

Yaani unasikitisha sana. Wewe hoja yako ya msingi hapo ni kwamba tuanze kampeni za kupeana talaka na tuache kuwa na ndoa ili tuwe kama ulaya na marekani? Au tuanze kuhamisha wanaume wawe mashoga ili tuwe na uwezo mkubwa kama marekani!!??

Unapoamua kushindana na marekani na ulaya kwa talaka na ushoga unatulazimisha kuamini kabisa wewe ni shoga ambae ni matokeo ya talaka. Vipi, na wewe unatoa misaada kwa nchi gani? Au kwa watu gani?

Sio mbaya kama kwenye hoja za maadili ukafikirisha akili yako sawasawa kuliko kuhalalisha haramu eti tuu sababu marekani na ulaya wanafanya hivyo
 
Back
Top Bottom