Ndoa humuongezea mtu heshima na kuaminika katika jamii yeyote

Ndoa humuongezea mtu heshima na kuaminika katika jamii yeyote

ndoa zina matatizo yake. ila uzuri unaofanya nisapoti ndoa ni kama familia ya mzee baba Casemiro. watoto wanamwona baba huyu hapa wanamwona mama huyu hapa. sio mtoto anamskia baba kwenye simu tu, kuonana mpaka weekend au skukuu.

HAINOGI.
20230224_025437.jpg
 
Hakika ndoa inaleta heshima kwa familia zote mbili. Ila kwa jamii ya sasa mtazamo huo ndo unaosababisha kuongezeka kwa ukatili,,mauaji ya mpenzi nk. Utakuta familia inamlazimisha binti aolewe na mtu ambaye hata hajampenda kisa tu yupo tayari kutoa mahari akishaolewa ndoa haifiki mwaka imevunjika,,wengine wanawake wenyewe wakiona umri umeenda wanajitosa kwa yeyote aliyeko mbele yale ili tu aolewe apate heshima. Akishaingia kwenye ndoa honeymoon ikiisha ameshamchoka mumewe,,,ndo vurugu zinaanza.
Ifike hatua jamii tubadilike. Tuangalie thamani ya maisha yetu kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muasisi wa ndoa kwa binadamu ni Mungu.

Alipowaunganisha Adam na Hawa katiba bustani ya edeni.

Familia ni msingi wa Taifa lolote kwani kukiwa na familia imara ni rahisi kuwa na jamii imara,dini imara na taifa imara.

Familia ni taasisi nyeti na muhimu mno.

Kwakua taasisi hii nyeti ni muhimu sana kwa msingi wa jamii,dini na taifa hivyo viongozi wake ambao ni wazazi huwa na umuhimu huo pia.

Ni rahisi sana kwa baba au mama kuaminika katika jamii yake au dini yake kwakua ana jukumu tayari ambalo ni msingi wa taasisi nyingine.

Ni rahisi kwa aliyeoa au kuolewa kupewa nafasi ya uongozi popote au kupewa jukumu zito popote kuliko yule asiyekuwa na ndoa.

Maamuzi ya mwenye ndoa na asiyekuwa na ndoa kuhusiana na maswala kadhaa ya kidini na kijamii ni tofauti sana.

Mwenye ndoa anakua amepevuka zaidi kifikra na kimtazamo katika maswala ya kijamii kuliko yule asiyekuwa na ndoa.

Kwakua maamuzi ya mwenye ndoa yanakuwa yaliyopevuka zaidi ya yule asiyekuwa na ndoa basi mhusika hupewa zaidi kipaumbele.

Ndoa ni mpango wa Mungu kwa wanadamu ila ni jambo la kusikitisha mno kuona namna shetani anavyotaka kuuuharibu kwa kuwahamasisha vijana wasioe.

Kijana ukitaka kuaminika na kupata heshima unayostahili.

OA.

Usipooa hakuna mtu mwenye akili timamu atayekupa jukumu lolote kubwa.
Ndugu yangu jaribu kutoka nje ya Bongo utagundua maisha siyo uniform.
 
Tafuta Tembo Mkuu..

Tembo kama Tembo huleta status ya Dunia.
 
Sasa heshima ndiyo nini, mimi uniheshimu au usiniheshimu sijali, sababu haunilishi, haunivishi wala haunisaidii chochote.

Waheshimiwa wa mchongo wapo huko bungeni na Waheshimiwa halisi wapo huko mahakamani.
 
Sasa heshima ndiyo nini, mimi uniheshimu au usiniheshimu sijali, sababu haunilishi, haunivishi wala haunisaidii chochote.

Waheshimiwa wa mchongo wapo huko bungeni na Waheshimiwa halisi wapo huko mahakamani.
The purpose of marriage is not to make women happy, or to make men happy.

The purpose of marriage is to ensure that every child is born into a situation where they will have easy access to their mother and a father.
 
The purpose of marriage is not to make women happy, or to make men happy.

The purpose of marriage is to ensure that every child is born into a situation where they will have easy access to their mother and a father.
And how to those in marriage while un-able to bear kid/s?

Your view please....
 
Back
Top Bottom