Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 25,258
- 48,589
Sehemu 1
Naitwa Mamujee, ni mzaliwa wa Musoma. Sijabahatika kusoma sana, niliishia kidato cha pili sababu ya kukosa mtu wa kunisomesha pindi tu nilipofiwa na baba yangu. Mama yangu alifariki kitambo sana tangu nilipokuwa darasa la nne. Baba yangu alipofariki tu, mimi nikachukuliwa na shangazi yangu anayeishi Dar es Salaam, huku kaka yangu akipelekwa kwa shangazi yangu mwingine anayeishi Arusha. Tumezaliwa wawili tu, mimi na kaka yangu.
Nilipofika Dar kwa shangazi, nilipokelewa vizuri. Shangazi yangu alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Pale nyumbani tuliishi na mjomba pamoja na watoto wa shangazi watatu. Kiufupi, pale nilikuwa kama house girl, kazi zote za nyumbani zilikuwa zangu. Watoto wa shangazi walilelewa kama mayai, hawawezi kufanya kazi yoyote. Tuliishi vizuri na shangazi huku nikiendelea kuwa mfanyakazi pale nyumbani, lakini sikujali kwa sababu nilijua mimi ni yatima sina pa kwenda, hivyo nikavumilia.
Ilikuwa imepita kama mwaka tangu nije Dar, nikawa mwenyeji na nikazoea jiji vizuri japo sikuwa mtu wa kujichanganya sana. Siku moja niliamka nyumbani na kuanza kufanya usafi kama kawaida. Shangazi na wanae walikuwa wametoka. Nilikuwa bize sana na kazi zangu, sikujua kama mjomba yupo ndani. Nilipomaliza kazi, nikaingia bafuni kuoga ili nijiandae niende Solomon.
Niliporudi chumbani kwetu nikivaa, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu. Mjomba akaingia chumbani na kunikamata kwa nguvu huku akinifunika mdomo. Mjomba alinibaka! Nililia sana. Sikuwahi kukutana na mwanaume tangu nimezaliwa, na mjomba ndiye alikuwa wa kwanza. Niliumia sana. Baada ya tukio hilo, mjomba alinitishia kuwa nisithubutu kumwambia mtu yeyote, la sivyo angeniua.
Nililala chumbani nikiwa na maumivu makali hadi shangazi aliporudi. Alinikuta nikiwa chumbani bila hata kupika chakula. Akaniuliza, "Mamujee, mbona hujapika chochote na umelala? Kulikoni?" Nikamjibu nalia, "Naumwa." Akaniambia niende nikanunue dawa. Niliposimama kuchukua hela kwa shangazi ili nikanunue dawa, nilitembea kwa shida huku nachechemea. Shangazi aliponiona nashindwa kutembea vizuri, akaanza kuwa na wasiwasi.
Akaniuliza, "Umefanya nini huko chini hadi unashindwa kutembea?" Alinipiga sana akinituhumu kuwa nimeanza umalaya, akidai nimtajie mwanaume aliyenifanya hivyo. Niliomba msamaha huku nikilia na kumwambia mimi si malaya, lakini hakunielewa kabisa. Kipigo kilipozidi, niliamua kumwambia shangazi ukweli kuwa mjomba ndiye aliyenibaka.
Badala ya kunielewa, shangazi aliniita muongo na kusema namsingizia mumewe. Alidai mimi ni malaya tangu utoto na nimerithi umalaya wa mama yangu. Hakutaka kunielewa wala hakutaka kumsubiri mjomba ili amuulize. Aliniambia nitoke nyumbani kwake mara moja. Aliingia chumbani, akabeba begi langu na kuniita nje. Akaniambia niondoke na kunipa shilingi elfu 60 ili nitumie kama nauli ya kunifikisha Musoma.