Ndoa ilimpa kilema cha maisha binti

Ndoa ilimpa kilema cha maisha binti

6
Nilifanikiwa kuingia Dar salama ilikuwa ucku sana ikabidi nilale stendi za Dar lux pale shekilango,,, asbh palivyokucha nikaanza kutembea mdogo mdogo huku nikijiuliza wapi naenda, nikapata wazo la kwenda bunju maeneo ya shangazi maana kule nimepazoea angalau, bc nikatafuta usafiri hadi huko, nilifika stendi pale nikasema ngoja nielekee upande huu wa pili yaan shangazi kwake upande wa kushoto mie nikaelekea kulia,, nikakutana na madalali nikawaomba wanitafutie chumba mda huo huo kisizidi elfu 50,, bc nilizunguka na madalali hadi nikapata chumba kizuri cha elfu 50, nikaripia mwaka mzima kwa laki sita, nikatoa 50 ya dalalli, nikaingia kwa chumba nikafanya usafi vzr, nyumba ilikuwa nzuri madirisha ya vioo na wapangaji watatu tu,, nikatoka nikaelekea madukani nikanunua godoro 5/6 , feni, jiko dogo la gesi na sufuria nne, ndoo tatu za maji yaan vitu vidogo vidogo vyote,, nikarudi geto nikapanga vitu vyangu vzr, nikasema sasa ngoja ninunue mchele, unga, sukari, mafuta, na vile vikontena vya kuwekea, yaan ndani palikuwa pazuri, bc nikaingia bafuni nikaoga nikalala ilikuwa jion tu, hapo bado nina hela kama milion moja na laki saba iv, nikatafakari sana nikasema nitafute biashara nifanye cjui nifanye biashara gn? Ilipita kama cku tatu iv Mahamood akanipigia cm, akanilaumu mbona siingii Wthsap? Nikamwambia nimechoka sana, akaniuliza Sasa umefanyaje kuhusu nyumba ya kuishi? Nikamwambia nipo kwa rafiki yangu, akaniambia bc nitoke niende nikafungue akaunti Crdb, mhhhh nilijifikiria nilitaka nisifanye ivo ila roho nyingine ikaniambia acha ujinga, utakufa masikini, kama kukubaka amekubaka tyr, embu fungua akaunti hiyo,, bc nikamwambia sawa, akanielekeza yeye mwenyewe niende mliman cty ndio nikafungulie huko,, bc nikanyanyuka nikaenda kufungua hio akaunti kisha nikamtumia akaunti namba yngu,,, bc nikawa natafakari kuhusu biashara gn nifanye nikapata wazo niuze vipodozi, mm napenda sana urembo, nikimuona mtu ana ngozi nzuri na ananukia vzr huwa napenda sana,, ile pesa yangu nikaweka benki milion moja nikabaki na ile laki saba,,, ilipita kama wiki Mahamood alinipigia cm ameniingizia hela kwenye akaunti yangu milion 4 niliogopa! Akaniambia nitafute nyumba nzima nilipie niishi peke yngu yeye akija Tanzania atakuwa anakuja hapo,, niliogopa mnoo, nikasema hapana cwez kuendelea kubakwa tena na huyu mtu, siendi tafuta nyumba wala nn nitaishi hapa hapa na akija Tanzania bc nitamkimbia,, bc maisha yangu yakaendelea hapo bado cjaanza biashara, naishi tu mwenyewe, ilipita kama wiki tatu iv nikaona nipo mpweke ndani napooza kukaa kimya nikapata wazo nichukue hela nikanunue Tv, bc nikatoa milion moja benki nikanunua Tv flat na kitanda pamoja na Azam,, sasa cku naongea hivo vitu jirani yangu aliona nae ni binti tu ila mm mdogo kwake, akaanza mazoea na mm kila cku anakuja chumbani kwangu mara aniulize shemeji ajambo? Yaan alinizoea gafra tu,, nilianza biashara ya vipodozi naenda kkoo nanunua vipodozi vile vzr na pafyumu nzuri nikawa nazungusha kwenye masaluni ya wadada nauza cash au nakopesha,, mtu akiniagiza kitu chochote naenda kumchukulia namletea, biashara ikaenda vzr nikaanza kupendeza,, Mahamood akawa haachi kunipigia cm Mara kwa Mara ananiahidi vitu vingi sana,, yule jirani akazidi kunizoea yaan kila nikiongea na cm na Mahamood lazima aje asikilize,, cku moja nimetoka nimemuacha chumbani kwangu nilikuwa nje nanunua soda, cm yangu nimeacha ndani haina hata password, naingia ndani tu namkuta yule Dada ameshika peni na karatasi anaandika namba ya Mahamood kutoka kwenye CM yangu alivyoona nimeingia alishtuka sana
 
7

Nilimkuta yule Dada kashika cm yangu yuko na karatasi na pen anaandika namba ya Mahamood,, nikamuuliza vp mbona unachukua namba kwenye cm yangu? Akabaki kimya! Nikamwambia Dada nakuheshimu sana harafu ww ni mkubwa kwangu si vzr nikakuvunjia heshima,, akaniambia nilikuwa nataka kujua huyo Bwana wako anaekuhudumia yupo nchi gn? Ndio maana nikawa nachukua namba ili nijue ni za nchi ipi, nikamwambia aliyekwambia mm nahudumiwa na Bwana nani? Nikamwambia Sasa huyo ni Babu yangu yupo Nje,, akabaki katoa macho nikachukua ile karatasi,, nikamwambia naomba aende nataka kulala mapema kesho naenda kkoo kufata mzigo wa wateja,, bc alinyanyuka akaniambia sawa ucku mwema ila hajafurahia kabisa,,, akiwa anatoka hata mlangoni hajafika Mahamood akapiga cm nikapokea, bc Yule Dada akarudi akakaa kitandani akawa anasikiliza Mahamood akaniuliza vp umelala? Nikamwambia hapana ndio najiandaa, akaniambia ulifanikiwa kupata nyumba kubwa? Nikamwambia sio sana, akaniambia washa data nikupigie WhatsApp,, mhhhh nikaogopa asije akaona chumba kimoja,, nikamwambia sina MB na maduka yamefungwa,, akaniambia sawa ila sitaki uishi kwa mtu, wala sitaki makundi makundi, nimeamua kukuhudumia kwa kila kitu na nitabadilisha maisha yako, utaenda Nchi yeyote utakayo taka ila tu utulie,, nikamwambia sawa akakata cm,, yule Dada akawa ananiangalia kama mtu anayetamani,, nikamwambia naomba nilale bc tutaonana kesho,, akaniambia Jee unalinga sana eeh? Unajiona Queen?? Iv unauzuri gn wa kupata Bwana wa namna hio?? Nikabaki namtizama tu,, akaniambia bc nitakuonyesha akatoka akapigiza mlango
Sikumfatilia sana nikafunga mlango wangu nikalala,, asbh nikaamkia kkoo nilikuwa na oda za watu bc nikawa bize cku hio,, ilifika jion sijarudi kwangu nikapitia salon moja iv ya mteja wangu huwa nampelekea biashara zangu, yule Dada wa salon akawa ananishawishi nitengeneze nywele bc nikakubari nikaanza kufumua nilizosuka ili nioshe, Mara yule Dada wa nyumbani akanipigia cm,, Jee uko wapi? Nikamwambia nipo mahari nimekaa, akaniambia Jee ww huliziki? Yaan una Bwana anakuhudumia kwa kila kitu arafu bado unamsaliti?? Nikamwambia we Dada embu nikome sitaki mazoea ya kijinga na msaliti nani? Unajua nipo wp? Nikakata cm!! Yule Dada wa salon akaniuliza vp unagombana na nani tena? Nikamwambia jirani yangu huyu anapenda kunifatilia sana,, akaniambia ana wivu huyo achana nae,,, bc niliosha nywele nikamaliza nikarudi kwangu, nafika tu nikamkuta yupo mlangoni kwake sijamsalimia wala nn, nikaingia ndani nikavua nguo nikaenda kuoga nikafunga mlango wangu na funguo nikaingia nazo chooni,, natoka bafuni nikamkuta yupo mlangoni kwangu eti Jee mbona umefunga mlango?? Nikamwambia nimechoka sana sijisikii kuongea nataka kulala,, akaniambia unalinga eeh! ,, Kuna mpangaji mwengine pale yeye ni mke wa mtu, akamwambia yule Dada mbona unamuonea Jee?? C amekwambia amechoka ataki kuongea na mtu? Embu muache mwenzio akapumzike, alikuwa ameshika kitasa changu akakiachia nikaingia ndani nikafunga mlango wangu,,, nilikuwa nimebeba chips zangu nikawa nakula huku nachezea cm,, akanitumia msg unajifanya Queen kumbe sura mbaya!! Sijamjibu wala nn,, ila nikawa namtafakari huyu Dada nimemkosea nn? Au anamtaka Mahamood?? Angejua mwenzie maisha yangu ninayopitia bora angeniacha nipumzike tu,, mm Mahamood wala simtaki nimepokea pesa zake sababu ya umasikini wangu tu namchukia Mahamood na mjomba sana kwa kuniharibia usichana wangu ningekuwa na uwezo ningewashitaki wote,, bc nililia hadi usingizi ulinipitia nikalala
Asbh palivyokucha nikaamka nikamshukuru Mungu nikaenda zangu mjini, nilienda kufata mashuka kwenye mnada Tandika ya mitumba, nikachagua mashuka mazuri nikayakunja vzr nikaenda kuyazungusha kwa wateja wangu,, yaan Mungu ni mwema yakaisha yote na nikapata oda nyingine,, nilivyoona biashara ya mashuka inaenda vzr na vipodozi navyo vinaenda vzr nikapata wazo la kwenda kufata mashuka Kampala
Nikasema nisikurupuke kwanza ngoja nifanye utafiti
Bc maisha yangu yakaendelea hapo vita vinazidi mm na yule Dada tumuite Edina
 
8
Niliendelea kuwa bize na biashara zangu nikitoka nyumbani asbh bc kurudi ucku hata muda wa kupika sikuwa nao,, nilikuwa nasema ngoja nijichoshe kutafuta hela kwa bidii ili nisinyanyasike tena,, ilipita kama wiki iv niko bize balaa hata Edina nilikuwa sionani nae nikirudi ucku nazama chumbani kwangu,, kuna cku moja nimerudi ucku kama saa tatu iv nikaingia ndani kwangu nikajifungia, mara mlango ukagongwa nikafungua alikuwa Edina, nikamuuliza vp mbona ucku? Mm nimechoka nataka kulala, akaniambia nimekuja nataka uniazime hela nina shida Mama yangu amelazwa kisha nadaiwa kodi,, nikamwambia mm sina hela, hela zangu zote zipo kwa watu, akaniambia bc mpigie Bwana ako mwambie akutumie, nikamwambia sina Bwana na kama unaona rahisi ivo bc na ww mpigie Bwana ako akupe,, hee c akanisukuma nikadondoka chini akaniambia una linga sana? Unazarau sana? Unanijua mm ww? Nikamwambia naomba utoke ndani kwangu Edina,, akaniambia ctoki, akachukua cm yangu akawa anataka kuifungua ila akakuta nimeweka password, akaniambia toa password nichukue namba ya huyo Bwana ako, arafu tuone kama atakutaka tena mshamba ww,, nikamwambia Edina toka ndani kwangu please!! Aisee nikasema kuonewa sasa kumezidi huyu Dada ananitafutia kesi,, hasira zilinijaa za kikurya nilimshika Edina nikamkaba kwa nguvu hadi aliishiwa nguvu,, mara mlango wangu ukafunguliwa alikuwa yule Dada mwingine mpangaji mwenzetu yupo na mume wake wakanishika wakanitoa,, Yule Dada akaanza kukwambia Edina ww mkorofi umemfata mwenzio ndani kwake kwa nn? Nimekusikia muda mrefu unamuanza Jee?? Acha wivu Edina,, kwan mtoto wa watu kakukosea nn?? Edina kimyaa,, nikaanza kulia kwa nguvu na hasira kali nikakumbuka mapito yangu yote, nikajiona na mikosi tuu,, Mara cm yangu ikaita hapo watu wote wapo ndani kwangu ila yule mume wa yule Dada alitoka, nikapokea CM huku nalia alikuwa Mahamood,, vp mbona unalia una shida gani? Nikamwambia kuna jirani yangu hapa ananichukia bila sababu eti anataka namba yako ya cm ili akujue ww nani unaye nisaidia mm? Amenisukuma hadi chini , Mahamood akaniambia huyo mtu yupo hapo? Nikamwambia ndio, akasema embu weka sauti kubwa kwanza, nikaweka hapo Edina anaona aibu yule Dada mwingine anamuangalia,, Mahamood akasema anataka namba yangu ya nn? Kwanza ww Jee c nimekwambia sitaki uishi uswahilini?? Ctaki uzoeane na watu wa ajabu ajabu?? Kwan ile hela haijatosha kuishi masaki?? Nikamwambia naishi bunju napo ni pazuri,, akasema pangekuwa pazuri huyo kahaba asinge weza kuishi nakwambia iv Tafuta dalali akutafutie nyumba Masaki natuma kesho pesa,, harafu wee kahaba acha kumsumbua mke wangu Mm sichukui mwanamke ilimradi nina vigezo vyangu,, ukijiona mzuri bc jipike ujitafune sawa daah Muarabu ana maneno hadi nilishangaa,, bc akaniambia akikusumbua zaidi mripoti polisi, akakata cm
Edina lilimshuka htr, yule Dada akamwambia Edina unatia aibu doh? Unalazimisha bahati ya mwenzio?? Hadi unafikia hatua kutaka kumpiga kisa wivu?? Edina akanyanyuka akaenda zake,, Yule Dada akaniambia lala kesho tutaongea,, bc nikafunga mlango wangu hata kuoga sikuoga nikalala
Asbh palivyokucha Mahamood alinipigia kujua kiliendelea nn nikamwambia safi tu, akaniambia nikatafute dalali nikamwambia leo sipo sawa nitaenda kesho kutwa akasema sawa,, nikaamka zangu nikaoga nikasepa zangu,, nilikuwa naenda posta kwenye maofisi nilikuwa na wateja zangu nawapelekea mashuka,, bc nina mteja wangu mmoja yeye yupo serikalini ni mfanyakazi, alinizoea sana nikamwambia wazo langu la kufanya biashara ya mashuka na mapazia kutoa Kampala kuleta Dar,, akaniuliza ni biashara nzuri yeye ana mtu anaifahamu biashara hio vzr kwahyo ataniunganisha nae,, bc tulikubaliana vzr ,, nikarudi home kwangu nyumba ipo kimya nikazama ndani kwangu huku nimebeba chips zangu,, nimekaa zangu nakula Mara mlango wangu ukagongwa nikafungua ni Edina tena daah huyu Dada jmn!!!
Itaendelea

9
Nilivyofungua mlango nikamkuta Edina, nikamuuliza vp? Akaniambia jee naomba tuongee, nikamwambia sawa ila sio ndani kwangu tukae hapo nje, akasema sawa, tukakaa akaanza kuniambia nisamehe sana kwa yote niliokufanyia, cjui nimekutwa na nn nazani nimechanganyikiwa tu maisha magumu,, nikamwambia ucjal yameisha,, akaendelea kuniambia Jee please naomba na mm nitafute Danga kama lako maana mm pia biashara yangu ni kuuza mwili wangu ila kwa sasa kila kitu hakiendi? Akaendelea, nilikuwa na Bwana Mzungu alikuwa ananisaidia sana ila nilikuwa nampa nyuma Sasa kaondoka kwao na kurudi cjui atarudi lini,, mhhh nikasema tobaa, mbona Dunia iko iv jmn?? Jee mie nitaweza ya Mahamood kweli?? Nikamwambia Edina mie sina Bwana, yule ananitaka kweli ila mm hapana,, eti bc Jee niunganishe mm nikasema bc ngoja niongee nae kwanza muhusika,, bc alifurahi Edina akaanza kuniambia ohh mie nimefanya sana umalaya ila sijapata Bwana wa kunionga nikaripia, nimeenda Zanzibar sana kutafuta wazungu na waarabu ila naambulia laki, laki mbili ikizidi tano, ila ww una bahati Jee bc nikamwambia mie naingia kulala kesho niingie mzigoni
Nilimtafakari sana Edina, nikasema iv akimpata Mahamood huyu c nitamwagwa mazima mie? Vp kuhusu maisha yangu yataenda vzr? Nikamkumbuka Shangazi yangu alivyonipiga kama Mbwa mumewe alivonibaka, nikakumbuka kipigo cha Baba mdogo hadi kuzimia, nikasema nikimpoteza Mahamood kwa sasa nimekwisha,, hapo benki nina kama milion 4 iv, nikasema hapa lzm niwe mjanja, mm ni yatima sina yeyote kila mtu hanitaki nisipo jisimamia mwenyewe haya maisha bc nitaendelea kuwa mtumwa,
Sio kwamba nilikuwa ctaki kuipanga nyumba kama Mahamood alivyokuwa anataka ila nilikuwa naogopa akija Tanzania c atafikia hapo? C atakuwa ananiingilia nyuma kila cku
Zilipita km cku tatu nawasiliana na Mahamood vzr ila swala la nyumba akawa halizungumzii coz nilimwambia nitamjulisha nikiwa vzr,, bc Edina hakuacha kuniulizia km ombi lake nimemfikishia kwa muhusika namwambia bado
Cku moja nimerudi zangu mihangaikoni nilikuwa nina hamu ya ugali, bc nikawa nasonga ili nile nilale, Mahamood akanipigia cm, akaniambia Jee nakupenda sana, unajua kwa nn nimekupenda? Nikamwambia hapana akasema ww una Nyota kali mnoo,, nilivyokuona mara ya kwanza tu nikaona unawaka kama jua,, nilikupita na gari lkn nikageuza kukufata,, Jee ww hujui tu ww ni Tajiri ,, nikabaki nashangaa, utajiri upi anao uzungumzia Mahamood?? Aliongea mengi sana, akaniambia yeye ana wake wawili mke mkubwa yupo Dubai, na mdogo yupo Uengereza,, na hapa Tanzania ana hard kubwa sana anauza magari hapa Dar na Zanzibar, akaniambia kama nitakuwa tyr nitakuwa mke wake wa tatu na nitaishi hapa Tanzania,, mhh Jee mie jmn nilipenda maongezi yake ila kifiro tu mhhh bc tuliagana
Kumbe Edina alikuwa ananisikiliza yote yale, nashangaa asbh ananiambia namdanganya tuu nimeshindwa kumuunganisha na huyo Bwana, nikamwambia hapana nilieongea nae sio huyo
Bc ilipita kama cku tatu, Edina aliniita akanipa chakula, akaniambia Jee leo usipike kula hiki chakula, nilishakataaga maana haijawahi kunipa chakula hata cku moja tangu nimehamia pale,, ila nikakipokea na kumshukuru nikaingia ndani

10
Vipenzi mnisamehe tu kwa kuichelewesha hii story, ila niliwaambia kabla jmn nipo bize mnoo, niliamua kuileta huku coz nilijua mtaweza kuvumilia hamna midomo michafu kama magrupu mengine maana ningekuwa grupu lingine bc ningejuta story yangu mwenyewe lkn ingenitoa kisirani,, mnivumilie tu!!
Nikapokea chakula nilichopewa na Edina nikaingia ndani,, nikakiweka kile chakula chini wala sikukila wala nn na wala sikufikilia kama kuna ubaya wowote ila nilikuwa nimeshiba zangu chips, napenda sana chips mwenzenu na zimenitoa kitambi ila siachi , asbh naamka najiandaa kutoka kama kawaida , Edina anagonga,, vp Jee kwema? Nikamwambia kwema tu cjui ww,, ulikula kile chakula?? Naomba sahani nioshe, nikamwambia wala sijala nilichoka sana jana mwenzio,, bc Edina akaniambia kwa hasira naomba sahani yangu na hiko chakula mhhhh nikajiuliza kwan kulikoni? Chakula hiki hiki au kuna mengine?? Nikachukua chakula chake nikampa,, akasonya bonge la sonyo, mhhhh nikasema hapa ipo namna sio bure,,, bc kuanzia siku hio ndio bifu langu na Edina likaanza rasmi,, nikitoka vijembe, nikirudi vijembe, akaanza kunichafua mtaaani kuwa mm mchawi naroga wanaume ili wanihudumie,, nilivyoona hali ya pale inazidi kuwa mbaya na mm ugomvi siuwezi nikaamua nilikubari wazo la Mahamood la kupanga nyumba nzima,, nikaongea na Mahamood kuwa anitumie hio hela nipange nyumba, ila ni kule kule bunju siwezi kukaa sehemu nyingine tofauti na kule bc alikubali bila kipingamizi
Nilitafuta dalali nikamwambia aina ya nyumba ninayo itaka akanitafutia nikaiona ni nzuri tu ipo kwenye geti ipo peke yake,, nikamwambia Mahamood akasema nipige picha nimtumie, nikafanya hivo bc akanitumia hela ya kulipia ya mwaka mzima,, nilimshukuru Mahamood ila nikifikiria kifiro naishiwa nguvu,,, bc nikajiandaa kuhama pale, nikaongea na yule Dada mwingine akaniambia nitafute mtu anirudishie garama zangu, nikamwambia sawa ila mm naondoka akipata mtu wa kuhamia pale bc atanitumia hio hela,, nilisubiri Edina katoka nikaleta gari nikabeba vitu vyangu nikasepa
Maisha nikaanza upya kwenye nyumba mpya huku naishi mwenyewe nyumba nzima,, nilimkumbuka Kaka yangu aliyekuwepo huko Arusha nikatamani nimtafute aje tuishi wote ili tupambane na maisha yetu ila sikuwa na mawasiliano nao na nikitaka namba zao lazima niende kwa shangazi ndio ana namba zao, na mm sikutaka kabisa kukutana na shangazi wala mjomba
Bc zilipita km cku tatu iv Edina akanipigia cm, wala sikupokea ilivyokata nikamblok moja kwa moja, cku zilienda maisha yakaendelea huku nawasiliana na Mahamood vzr ,, nakumbuka hio cku nimeamka zangu kwangu nikafanya usafi ndani na nje maana nyumba kubwa Sasa nikawa nimechoka, nikasema leo sitoki ngoja niende sokoni ninunue ndizi zangu nipike nilimisi sana kupika,, bc nikajiandaa vzr ile nataka kutoka tu cm yangu ikaita kuangalia namba ngeni mhhh, nikajiuliza nani tena? Halow Mamujee mpnz mzima? Mhh nikashangaa huyo anae niita mm mpenzi nani?? Ila sauti yke nikiisikiliza vzr kama Mahamood? Sasa mbona hii namba kama ya Tanzania?? Bc nikamjibu nzuri,, akasema mm Mahamood nipo Tanzania njoo mliman cty sasa iv


Nakuja
 
3

Bc nikaandaa zangu chakula ili Kaka akija tule, Kaka akarudi ila hakuwa na raha kabisa, akaniambia Jee hii Dunia ni ya ajabu sana, cjui watu wapoje? Wanapenda kuwaza Negative kwa kila jambo? Nikamuuliza kivip Kaka? Akaniambia watu wamempigia cm mpenzi wake kuwa yeye amereta mwanamke ndani na kesho anakuja kujua mbivu na mbichi,, akaniambia nisijali ataniombea kwa yule jirani ili nilale nae,, bc nikawa mpole nikakosa cha kusema, asbh Kaka aliongea na yule jirani akakubali mm kukaa kwake,, bc kama kawaida nikafanya usafi ndani nikatoa begi langu kupeleka kwa jirani ili akija mwenyewe asinikute mule, bc tulikaa na yule Dada jirani huku tukipiga story mbali mbali, mara yule mpenzi wa Kaka akaja alikuwa na funguo zake akaingia hadi ndani, mie nilikuwa kimya na yule Dada jirani aliniambia nisiende kule maana yule Dada anajisikia sana asije akanionyesha ovyo,, Kaka akarudi akaja huku kwa jirani akanipa hela ya kula yeye akaenda ndani kwake,, nilikaa pale kwa jirani wa Kaka hadi wiki iliisha sikuingia ndani kwa Kaka ila Kaka alikuwa ananipa hela ya matumizi kama kawaida,, nakumbuka siku moja Kaka arirudi kazini akaja huku kwa jirani, akaniuliza Jee unapajua Kariakoo?? Nikamwambia hapana maana niliona kama mtego ananipa,, akanipa hela elfu 50 akaniambia nenda ununue vitu vyako muhimu kesho kutwa nakuletea ticket ya kwenda nyumbani,, bc yule Dada jirani akaniambia kunisindikiza kkoo,, bc nirifurahi sana kwa wema wa Kaka ila nilipata mawazo sana kuwa narudi Musoma naenda kukaa kwa nani? Nikasema bc kama shangazi yangu wa damu kanifukuza bc acha nirudi nyumbani
Asbh tulijiandaa na Dada jirani kwenda kkoo, tulifika vzr nikanunua chupi na sidiria na losheni tu nikabakisha hela kidogo ili nikifika Musoma niuze hata maandazi, bc tukawa tunarudi njiani tukielekea stendi gafra Dada jirani akapigiwa cm na mpenzi wake, akaniambia Jee ww nenda nyumbani mm nitakuja baadae, akanielekeza vzr na funguo alipo iweka, bc akaondoka na mm nikaenda stendi, nimesimama zangu stendi gafra ikaja gari mbele yangu nashangaa anaanza kuniita, nikawa sijamuelewa ni nani? Niliosimama nao stendi wakaniambia Dada unaitwa ww,, nikaenda yule Baba akaanza kutabasamu akaniambia panda twende nikupeleke hapo utakesha usafiri ni shida,, bc na ushamba wangu hata bila kuuliza unanipeleka wp nikapanda gari, nikamuelekeza ninapo enda akasema sawa,, Mara tukafika sehemu akapaki gari akashuka akaingia ndani, akanifata akaniambia haya njoo mara moja,, alikuwa mbaba mrefu kama muarabu IV, nikashuka akanipeleka hadi chumbani ilikuwa hotel, tukaingia ndani akaenda kuchukua vinywaji akaleta,, alinipa soda ila yeye alikuwa anakunywa pombe, niliogopa nikamwambia naomba niondoke, akasema subiri nitakupeleka, akaniuliza una CM? Nikamwambia hapana, akaniambia yeye kesho anasafiri kwenda Dubai ila anataka niwe mpenzi wake maana ameona Nyota yangu ni kali sana na itamfaa sana kwenye biashara zake kwa hiyo tuwe wapenzi,,, sikumuelewa chochote nilikaa kimya tu, nilienda chooni kukojoa nikaacha soda yangu ikiwa wazi, nilivyorudi akanilazimisha ninywe soda yngu, bc nikainywa mara nikaanza kupata kizungu zungu, na sikujua kinacho endelea, nilikuja kushtuka nipo uchi wa mnyama na nguo zangu zimekunjwa vzr zipo kwenye meza,, nikanyanyuka nikaanza kupata maumivu sehemu ya haja kubwa, nikasogea mezani ili nivae nikakuta vipimo vya ukimwi viwili vimegandamizwa na karatasi yenye maandishi"NIMEKUPENDA SANA MTOTO MZURI, HAYO HAPO NI MAJIBU YA UKIMWI YANGU NA YAKO TUPO VZR KUANZIA SASA MM NA WW NI WAPENZI,, HAPO CHINI YA NGUO ZAKO NIMEKUWEKEA CM PAMOJA NA HELA MILIONI TATU ZITAKUSAIDIA HADI NIRUDI SAFARI,, NIMEKUWEKEA LAIN KWENYE CM PLEASE USIBADILISHE,,,," niliogopa sana nikajikagua nikakuta nimeingiliwa kinyume na maumbile nikavaa nikachukua zile hela kweli zilikuwa milion tatu na CM ya smartphone pamoja na chaji cm ilikuwa mpyaa
Itaendelea
Duuh
 
11
Mhhh ile cm ilinifanya nichoke kabisa, nikarudi chumbani nikaingia chooni maana tumbo la kuharisha lilinibana ghafra, nimetoka tu chooni cm nyingine,, Chukua usafiri uwahi hapa sina mda wa kukaa hapa, mhhhh jmn Mamujee mie, umasikini huu ndio unanifikisha huku? mhh!! Nikasema ngoja niende tu sina jinsi, kweli aliniingilia kinyume ila amenisaidia sana acha niende ,, ikabidi nibadilishe nguo, nikavaa jeans na top nikabeba mkoba wangu nikatoka,, nilikodi bajaji hadi mliman cty,, kweli nilikutana na Mahamood,, kiukweli nilivyomuona Mahamood siku ya kwanza na leo tofauti, nadhani cku ya kwanza sikumuona vzr,, kumbe Mahamood ni mzuri tu mrefu, muarabu mwenyewe ila sio kivilee mhhh Amamu mie!! Bc alinikumbatia huku natetemeka balaa,, akaniambia Mamujee ww mwanamke una akili sana, angekuwa mwanamke mwingine tyr ningekuta kajichubua sura na iv hela nampa?, Nikamwambia mm sijawahi kujichubua, akasema ndio sababu nimekuchagua,, bc tulisalimiana pale akaniagizia chakula nikala huku nikiwa na hofu ila nilijipa moyo,, tulivyomaliza kula akaniambia tuondoke, sikujua tunaenda wp ila tulipanda gari yake hadi hotel moja iv, ilikuwa nzuri sana, akaniambia hapo ndipo amefikia,, tukaingia chumbani akatoa begi kubwa akaniambia Mamujee fungua hizo ni zawad zako, nilifungua lile begi nikakuta mabaibui mazuri mazuri jmn, magauni marefu yanangaa na mitandio yake,, pafyumu nzuri pamoja na udi, kiufupi nguo zilikuwa nyingi na nzuri sana,, akaniambia nikaoge nibadirishe nguo,, bc sikuwa na jinsi nikaenda kuoga nikavaa nguo mojawapo nikajipulizia pafyumu, akaniambia haya tutoke, hapo bado hatujafanya chochote
Bc tulitoka hadi nje akaita gari hao tukapanda lile gari alilokuwa analitumia yeye aliliacha pale pale Hotelini ila akaita gari lingine, hapo cjui tunaenda wp, bc tukafika hadi uwanja wa ndege akaniambia Mamujee ushawahi fika Zanzibar? Nikamwambia hapana,, bc leo tutalala Zanzibar nikakaa kimya tu, kweli tulipanda ndege mara tu tumefika nikasema huyu mwanaume ana hela ila tabia yke ndio mbaya,, tulifika tukaenda hadi hotel tulikula tena kisha akanipeleka hadi kwenye hard yake ya magari,, ni sehemu kubwa ina uzwa magari mazuri,, akanitambulisha kwa wafanyakazi wake kuwa mm ni mke wake wa tatu,, bc walinipokea kwa heshima sana,, alinitembeza kidogo tukarudi hotel,, akaniambia Mamujee nimekumisi sanaa nikaanza kulia akaniuliza vp? Nikamwambia mm sipendi huo mchezo akanikumbatia cjui alinipa nn nikapoteza fahamu tena nilivyoamka nikamkuta amelala tena anakoroma, nilijikagua vzr nikakuta ameniingilia tena nyuma tena sio mara moja nililia hadi akaamka, akaniuliza vp mke wangu? Hata sikuongea, nikaendelea kulia tu, akanibeba kwa nguvu hadi bafuni, akaniogesha, akaniambia nivae nguo, nikavaa huku nalia, tukatoka, ilikuwa tyr ucku umefunga, tukashuka chini hadi kwenye ufukwe wa bahari, tukakaa, ni hapo hapo Hotelini yaan kumetuliaa wamejaa wazungu tu,, akaniambia Mamujee nisamehe sana nakupenda sana, ila cwez kujizuia kufanya ivo ndivyo inanibidi nikufanyie ivo na nikikufanyia ivo ndipo nazidi kupata utajiri nililia sana, akanikumbatia akaniambia sema unataka nn kutoka kwangu nikupe? Chochote nitakupa ukitakacho, sikuongea chochote nikakaa pale akanipeleka sehemu kula vitu vya baharini
Itaendelea/ comment ndio zitanishawishi kurudi



12
Hayaaaaa mjeeeeeee maana lawama ndoo mbili
Bc tulienda kula vitu vya baharini c mnajua tena Zanzibar, pweza cjui ngisi, mm sikutaka hata kula chochote, Mahamood alikula then tukarudi hotel,, tupo zetu hotel naogopa hata kulala nahofia asiniingilie tena,, Mahamood akatoa laptop yake akaanza kunionyesha picha zake na familia yake,, kiukweli alikuwa Tajiri hasa maana ananyumba nzuri kubwa tena ghorofa, yaan kama zile tunazoziona kwenye video , akaniambia Mamujee naomba unizoee, nakuahidi nitakupenda na kukupa chochote utakacho,, nikamwambia hapana mm cwez hivo unavyonifanyia , akasema bc sawa sikufanyii tena, ila niahidi utakuwa wangu peke yngu,, nikamwambia sawa!!! Bc akaniambia nilale tu nisiogope anifanyi kitu tena, bc usingizi ukanipitia kweli, kuja kushtuka asbh nimefunikwa shuka vzr na Mahamood amelala fofofo,, nikaamka nikawa nachezea cm, nikakuta msg kutoka kwa Edina,, Jee mambo? Nimekuja hapa kwako mbona haupo?? Sikumjibu ila nikajiuliza huyu kwangu amapajuaje?? Nikaamua niachane nae,,, bc Mahamood aliamka akanikuta nishaoga kabisa na yeye akaenda kuoga akavaa tukashuka chini kula,, akaniambia sasa tunaondoka turudi dar,, tulifatwa na gari yake tukaenda kwanza kwenye hard yake then tukapanda ndege hadi dar
Tumefika dar moja kwa moja hadi Hotelini alipofikia,, tukala tukawa tunapiga story, kiukweli jmn Mahamood ni muungwana sana ila tabia yke chafu ndio inanifanya nimuone shetani,, bc tuliongea mengi hadi kuhusu familia yangu,, akaniambia Mamujee usijali mke wangu,, mara anishike hapa, mara anibusu bc kero tu!! Nikamwambia nataka niende kwangu,, akaniambia subiri nitakupeleka,, tuliendelea kukaa pale bila kunifanya chochote
Jioni ilipofika akaniambia haya twende huko kwako, tulitoka hadi kwangu, alivyofika tu akaanza kuzunguka nyumba nzima, akaniambia Mamujee hapa ndipo umepapenda? Nikamwambia ndio,, akasema haya bhana, tuliingia ndani, sebleni kwangu hakukua na kitu chochote, tv ilikuwa chumbani na kitanda bc akaniambia mbona huna kochi? Sikumjibu maana kama hela nilikuwa nayo ila bc tu,, akakaa kidogo tu akaniambia mm nasepa,, nikamuuliza unaenda wp? Akaniambia Hotelini, mhhhh, nikamwambia Kwan hulali hapa? Akacheka akasema silali kwenye nyumba ya mwanamke mhhhh nikamwambia sawa ila nikajifanya nimenuna, akaniuliza vp una shida yeyote? Nikamwambia sina, bc akanibusu akasepa zake,, mhhhh nikaanza kuona wivu jmn nikajikuta moyo unauma cjui kwann nikajiuliza kwann Mahamood ameondoka? Au ameenda kwa wanawake wengine?? Nikajikuta nalia hata sikula kitu nikalala
Asbh naamka naangalia cm nakuta missed call kibao za Mahamood, nikakumbuka alivyonifanyia jn nikashikwa na wivu upya nikaoga najiandaa nikanywe supu hapo jirani kuna bar kubwa tu, mara cm yangu ikaita kuangalia Mahamood, akaniambia njoo unifungulie geti, nafika getini naona magari mawili, la kwake na kenta ya mizigo,, nikafunga gari la mizigo likaingia,, jmn jmn kumbe Mahamood alinifanyia shopping ya nyumba nzima tena kutoka GSM sofa seti, tv kubwaaa nch 52, friji kubwa Boss, jiko kubwa la gesi, oven, microwave, masefuria yale mazito meza na viti vya chakula, zuria, na showcase daah cjui niseme nn mie bc akamwambia wale watu waingie wanipangie vzr,, walivyomaliza wakaondoka tukabaki na Mahamood,,. Akaniuliza mbona jana hukupokea cm? Nikamwambia nililala,, nikajikuta namkumbatia na kumbusu mhhh,, akaniambia Mamujee naomba bc maana hilo busu lako,, nikamwambia ctaki nyuma, akasema hata mm sitaki nyuma bc kwa mara ya kwanza aliniingilia mbele ila kwa tabu sana maana tangu nibakwe na mjomba sikuwahi kupagusa tena,, bc alifurahi sana maana alikuta kama bikra tu japokuwa mjomba aliitoa bikra yangu
Tulivyomaliza tukaoga akaniambia anipeleke kwenye hard yake ya magari ili akanitambulisha!!!
Itaendelea


13
Samahanini jmn ile niliyoposti Jana badala ya kuwa namba 12 nikajikuta naandika 11, kwhyo 11 zitakuwa mbili,,, tuendelee
Nikajiandaa vzr nikavaa baibui jipya ila ndani nikavaa jeans, Mahamood alinisifia sana na kuniambia nimependeza,, tulitoka pale safari ya kuelekea huko kwenye biashara yake,, tumetoka tu nje nikamwambia njaa inaniuma tuingie pale bar ili tunywe supu, alinishangaa, akaniambia Mamujee unaenda bar?? Nikamwambia tunywe tu supu, akaniambia sipendi mwanamke anae kwenda bar, ujue bar ni sehemu ambayo inavishawishi sana sasa unanishangaza unavyoniambia mtoto wa kike peke yako kuwa unaingia bar eti kunywa supu?? Mhhh nikasema hii tena kazi, nilikaa kimya sikuendelea kuongea tena,, bc wote tukawa kimya ,. Nikashangaa gari linaingia mliman cty , akashuka yeye akaroki milango nikabaki mwenyewe kwenye gari, hazikupita hata dakika 20 akarudi kabeba take away,, akaniambia haya kula, ctaki tena kusikia umeingia bar mhhhh jmn!! Nilifungua kile chakula nikakuta kuku, egg chop, kachori, sambusa za nyama, yaan vitu vingivingi tu na juice,, huyo kawasha gari tukaendelea na safari kimya kimya eti amenuna mm kuingia bar ,,, bc nikawa nakula zangu nikachukua nyama nikamlisha nilijikuta naanza kumpenda Mahamood jmn bc alikula vzr, Mara tukafika hio sehemu, alishuka akaniambia maliza kula kwanza, nikabaki kwenye gari ila jicho langu lote nje naangalia ile sehemu ni kubwa magari ni mazuri ni mengi hatari, nikaona wafanyakazi wake wanaume na wadada, bc kuna kidada kimoja kizuri kina shepu, alivyomuona Mahamood anaingia akamkonyeza mwenzie nikawaona wanajiweka vzr nguo zao, yule mwenye kishepu akajiangalia tako lake huku anajiweka vzr nawachora tu c mnajua tena kwenye gari vioo vya giza, wa nje haoni ndani ila wa ndani anaona nje bc Mahamood akawasogelea akawapa mikono huku wanatabasamu wenyewe ,, Mahamood alivyokuwa anaingia ndani nikaona wanaongea huku wanamuangalia anavyo ondoka,, nikajiuliza hivi Mahamood hawa wadada ajawafanya nyuma kweli?? Mhhhh!! Nikamaliza kula, mara cm yangu ikaita nikaona namba ile aliyotumia Edina kunitumia msg, nikapokea nikamuuliza nani?? Mie Edina naomba tuonane tuongee,, nikamwambia sipo dar kwa sasa nipo Musoma,, nikakata cm,,, Mara Mahamood akaja huku kaongozana na mbaba mtu mzima iv,, akafungua mlango akanishusha huku amenishika mkono,, akamwambia yule mbaba huyu ni mke wangu mdogo,, nikamsalimia yule Baba, tukaingia humo ndani,, wale wadada wakawa wanaangalia kwa mbali, Mahamood akawa ananizungusha kwenye magari ananielekeza aina za magari huku kanishika mkono, tukaingia hadi ofisini kwake, nikakuta picha yake imebandikwa ukutani,, ofisi nzuri,, bc akawaita wale wafanyakazi wote nikatambulishwa kwao,, nikaona wale wadada wanatizamana cjui walikuwa wanajiuliza huyu bosi huyu Dada kampendea nn maana Mamujee mm mwembamba mrefu mweusi sina hata tako
Mara nikashangaa kumuona msanii mmoja mkubwa sana hapa bongo wa bongo freiva, kaja kuchukua gari yake,, akawa anaongea na Mahamood,, bora bosi leo nimekukuta mwenyewe bwana, hawa watu wako wamegoma kabisa kunipunguzia,, Mahamood akauliza gari gn umelipia? Akaambiwa, akamwambia hio gari ipo juu sana bosi hio bei waliokupa ni sawa kabisa,, bc tulikaa pale ofisini wale wafanyakazi walitoka nikabaki na Mahamood ,, tukawa tunapiga story tu
Tulivyotoka pale tukaenda Hotelini alipofikia, tukala tukaanza kuongea,, ndipo akaniambia vzr cku aliyoniona alikuwa anatoka msimbazi police pale kkoo alikuwa anaenda kuonana na mtu pale sasa wakati anarudi kuelekea Hotelini ndipo akaniona nimesimama zangu stendi , akaniambia Mamujee nimekupenda mnoo,, akaanza kunitania ulivyosimama kishamba shamba pale stendi cjui kama vibaka hawakupanga kukuibia nikampiga kibao, akachukua mto akanipiga nao tukaanza kukimbizana mle ndani tukajikuta tumesex tena njia ya kawaida tu
Alinihahidi vitu vingi sana hasa kufunga ndoa na kunijengea nyumba,, akaniambia akitoka huku Tanzania bc anaenda kwanza Uingereza kwa mke wa pili then atarudi tena Tanzania,, Dubai hatoenda kwa sasa coz alikuwa huko juzi,, akaniambia akitoka Uingereza anakuja kunitafutia eneo ili anijengee nyumba yangu kwanza ndipo tufunge ndoa,, kweli nilijikuta napata faraja namuona kama Malaika aliyeshushwa kuniokoa,, akaniambia kuanzia Sasa hio biashara zangu niache nitafute fremu maeneo ya kkoo niuze mabaibui na magauni, yeye atakuwa ananiagizia mzigo kutoka Dubai,, ila akaniambia ole wako unisaliti nakuua Mamujee mhhhh, bc tulilala pale hadi asbh hata kwangu sikurudi
Asbh yake yeye alikuwa anaenda kazini kwake na mm nikamuomba niende kwangu, bc tulikubaliana akaniitia gari likanipeleka hadi kwangu,, nilivyofika kwangu nikaanza kuvikagua vile vitu nikashukuru Mungu
Nikakumbuka mapito yangu yote jinsi nilivyokuwa nafanyishwa kazi kwa shangazi kama mtumwa, naamka saa kumi napiga kazi, mara nipo kwa kuku, maana shangazi alikuwa anafuga kuku, ngombe, bc hadi kukamua mazoea ilikuwa ni mm na hakunilipa hata mia mbovu, shukurani yake kunifukuza kama mbwa wakati mumewe kanibaka nilijikuta nalia, nikafungua begi langu nikatoa namba za cm za Kaka aliyenisaidia pale ubungo ucku, nilikosa matumaini, sijui pakwenda, ila Kaka alinisitiri hata hakuofia usalama wake ila aliangalia usalama wangu
Nikapiga cm iliita sana bila kupokelewa, ckukata tamaa nilizidi kupiga tu ndipo ilipokelewa na sauti ya mwanamke, nikaomba niongee na Kaka Denis,, akaniuliza ww nani?? Nikamwambia mie mdogo wake Mamujee, ukimwambia hivo ataelewa,, bc yule mtu alitulia kimya kwanza kisha akaniambia Denis amefariki ana wiki mbili sasa mwenzenu nina mkosi gn Mamujee mm nilitegemea nimepata ndugu yangu,, kumbe haikuwa ivo Kaka Denis amefariki?? Nilipiga kelele moja nikapoteza fahamu nipo peke yngu ndani
Itaendelea

Nimerudiiiiiiiiiiiii, hayaaa mjeeeeeee tumalize,, likes za kutosha na comment ndio nitashusha fasta fasta, tag mwenzio aje

14
Tusameheane bize kupambana na life....
Bc nilivyopokea zile taarifa za kifo cha kaka Denis nikajikuta naishiwa nguvu na kulala hapo hapo , nilikuja kushtuka baadae sana nimechoka kichwa kizito, nikatafakari sana maisha yangu nikasema hapa nijikomboe tu mwenyewe maana sina yeyote wa kumkimbilia, nilikuwa na namba ya yule Dada jirani ya Kaka Denis, nikampiga lkn haikupatikana, nikajinyanyua zangu pale nikaingia bafuni kuoga, nimekaa zangu huku nina mawazo lukuki, Mahamood akanipigia cm akaniambia atakuja kulala, bc nilimuuliza niandae chakula gn?, akaniambia chakula atakuja nacho yeye, bc niliandaa chumba vzr nikapuliza udi, Mahamood aliniletea huo udi kutoka Dubai,, nikakaa zangu sebleni nimevaa kinguo cha kulalia namsubiri Mahamood,, kiukweli nilianza kumzoea na kumuona mtu wangu wa karibu,,,,
Mahamood alifika tukakumbatiana nilianza kumpenda na kumuona wa kawaida tu,, akaniambia Mamujee ngoja nikaoge kwanza nimechoka sana,, aliingia bafuni nikawa naandaa chakula ili tule,,, CM ya Mahamood ikawa inaita sn,, wala sikujihusisha nayo, alivyotoka mwenyewe ndio akaichukua, alikuwa mke wake mdogo wa Uingereza, wakaanza kuongea kiarabu wenyewe huku wanachanganya na kingereza,, yaan kama vile Mahamood alikuwa anajitetea flani iv,, waliongea mda mrefu sana,,, mm nipo kimya naangalia tv tu,, cm ilivyokata ndio akaanza kuniambia, huyu mke wangu wa pili mkorofi sana, yaan anataka kila wakati niwe nae tu? Ukiwa nae mbali hata miezi miwili tu anaanza kelele? Kila kitu anacho na yeye anasimamia kampuni yetu kubwa huko ila mkorofi tu, mwenzake mke mkubwa hana shida ata ukikaa miezi sita hujamuona wala hajali,,, nikasema mhhhh sasa hapa nitapaweza kweli mkurya mie bc nikazidi kuwa mpole,, tulikula chakula vzr huku tukipiga story tofauti tofauti,, akazidi kunisisitiza kuwa anataka kunioa na nimzalie watoto wawili tu,, bc tulilala na tukafanya mchezo ila kwa njia ya kawaida,, asbh tuliamka akajiandaa ili aende kazini kwake
Tulikaa na Mahamood pale hakwenda Hotelini tena alikuwa anakaa kwangu,, kweli nilimzoea nikimuona kama ndugu, rafiki, yaan nilimuona kila kitu,, safari yake ya kuondoka ilikaribia akaniambia hataki tena nifanye biashara zangu za kuzunguka zunguka, akaniahidi akirudi atakuja kunifungulia biashara,, bc aliniingizia hela ya kutosha kwenye akaunti yangu na kuondoka zake,, kiukweli nilikuwa na hela ya kutosha,, nikaanza maisha yangu huku nikimiss Mahamood,,,
Sikutaka kumsikiliza sanaa Mahamood nikaanza biashara zangu upya, yaan hela ya benki nilikuwa siitoi hata mia natumia hela za biashara zangu tu,, ilipita kama wiki bila ya mawasiliano na Mahamood, ila nikawa mvumilivu coz kama cm bc lzm anipigie yeye,,, niliendelea na mishe zangu huku nakaa mwenyewe nyumba kubwa ila nikazoea
Asbh moja nimeamka nikaanza kujisikia vbya kizunguzungu, hadi nashindwa kutoka kitandani,, nikahisi ni maleria maana sijaumwa mda mrefu,, nilivyopiga mswaki ndio nikatapika haswa yaan njano tupu, nikasema ngoja niende hospital, nikajiandaa kwenda hospital, nikachukua bajaji hadi hospital, ni hospital ya kulipia, nimefika hospital tu naanza kujiandikisha mapokezi nikashangaa mtu amenigusa bega,, kugeuka namuona shangazi huyu hapa nikamsalimia vzr, akaanza kuniambia vp unaumwa? Nikamwambia ndio,, bc akaniambia nenda kwa Dactari then nakusubiri palee,,, mhhhh nikasema sawa,, bc nikaingia zangu kwa doctor nikaandikiwa vipimo vzr, nikaingia kupima,, majibu yalivyotoka mhhhhh
Narudi


15
Bc jmn majibu yalivyotoka mhhhhh eti mjamzito nikamuuliza doctor itakuwa inamda gn, akaniambia kama wiki mbili iv yaan bado changa kabisa , bc akanipa dawa maana nilikutwa na maleria,, nilichanganyikiwa nikasema nitafanyaje kuhusu hii mimba? Hapo inaenda wiki ya pili hatujawasiliana na Mahamood,,,, nikatoka nje nikaenda pale nilipoambiwa na shangazi,, kweli nilimkuta amekaa ananisubiri,, akaniuliza vp una shida gani? Nikamwambia ni maleria tu,, akaanza kuniuliza eti una ishi wp? Maana nilikuwa nimependeza tu ukiniona hata ngozi yangu unajua tu nimebadirika sio Amamu yule,,, nikamwambia naishi kwa rafiki yangu,, akaniambia kwa nn sikwenda kijijini?? Nikamwambia nilikwenda ila baba mdogo alinifukuza , yaan shangazi akajifanya kama sio yeye eti anashangaa kwnn alikufukuza?? Nikasema cjui,, bc aliongea pale kama mtu mwema jmn,,, ila sikumfatilia sana maana nilikuwa na mawazo kuhusu ujauzito wangu,, akawa anaiangalia cm yangu maana niliitoa kwenye pochi nilikuwa naongea na mteja wangu,, akaniuliza unafanya kazi gn? Nikamjibu biashara,, ila alishindwa hata kuuliza huo mtaji umepata wp?? Bc alichukuwa namba yangu ya cm tukaagana maana ckutaka ajue ninapo ishi,, nikachukua bajaji hadi kwangu nimefika kwangu mawazo tele cjui nafanyaje Mamujee mm?? Bc niliendelea na dozi yngu hadi namalizia doz sijapigiwa cm na Mahamood, ila nikimuangalia wtsap pia simuoni,,, bc nikaendele kujiuguza hadi nikapata nguvu nikarudi kwenye biashara zangu,, hapo inakaribia mwezi,, shangazi akawa ananipigia cm Mara kwa Mara kujua naendeleaje,,, cku hio nimetoka zangu kwenye biashara zangu nimefika kwangu tu na cm yangu ikaita kuangalia namba za nnje,, nikapokea alikuwa Mahamood aliniuliza naendeleaje? Nikamwambia vzr tu, akaniomba samahani kwa kuwa kimya mda mrefu eti mke wake mdogo ni mkorofi sana huwa anakagua cm?? Nikamwambia sawa,, ila sikumwambia habari za mimba,, tuliongea akaniuliza kama nina shida yeyote au kama nina uhitaji wa pesa? Nikamwambia hapana,, bc akaniahidi atanipigia tena kesho yke,, tuliagana nikaendelea na Mambo yngu, nilijiuliza sn nafanyaje kuhusu huu ujauzito?? Ila nafsi inaniambia mbona hela unayo benki ya kukutosha tu hata huyo Mahamood asipo kuja?? Bc nikawa najipa moyo tu,, maisha yakaendelea ila mawasiliano na Mahamood yalikuwa ya tabu sana,, niliendelea kupambana hadi mimba yngu ikafika miezi mitatu cjamwambia Mahamood,,
Cku hio nimeshinda nimelala sana hata chakula nilishindwa kula nilishindia juice tu,, nikashangaa cm yangu inaita namba za Mahamood za hapa bongo,, nikapokea akaniambia amefika niende Hotelini,, nikajikuta namjibu tu siwezi kwenda popote cjisikii,, akaniuliza Mamujee unanijibu nn?? Nikamwambia sijisikii kutoka nikakata cm,, nikaanza kulia nikasema ina maana hadi kafika Tanzania hajaniambia ndio ananikurupusha niende Hotelini?? Nikanyanyuka nikaoga nikalala maana ckuwa hata na nguvu,, ucku wa saa tatu iv akanipigia nimfungulie get, kweli nikafungua akaingiza gari ndani, tumefika ndani wala sijamchangamkia ,, akaenda kuoga akaja nilipo kaa, akaniuliza nina shida gn?? Nikamwambia sina shida nipo kawaida,, bc alinibembeleza pale akaniambia nisijali akinioa ndio atakuwa huru kuongea na mm hata mbele ya wake zake,,, tulilala vzr na mechi tukapiga ila ile ya kipole maana naumwa,,, asbh kumekucha kama kawaida yangu lazima nitapike asbh ndio maisha yaendelee akaniona ninavyotapika tena huku machozi yananitoka akaniuliza nn shida? Nikamwambia siko sawa,, akaniuliza tena una mimba?? Nikamwambia ndio,, akaniuliza mbona hujaniambia?? Nikamwambia ningekwambia saa ngp wakati alikuwa hapigi cm?? Akaniambia sawa jiandae twende hospital,,, nilijiandaa hadi Agakhan hospital,, tulifika pale akaongea na doctor nifanyiwe ultrasound ili ajue ujauzito una mda gn,, mda wote huo nipo kimya hata yeye hachangamki sana,,, nikafanyiwa vipimo vzr na majibu yakatoka mimba yangu ina miezi mitatu na wiki tatu,, Mahamood alinitazama usoni,, akaniambia twende,,, hapo sielewi mwenzangu anawaza nn?? Tukatoka hadi nje tukaingia kwenye gari kimya kimya,,, tulienda hadi kwenye hard yake ya magari,, akashuka akaniacha kwenye gari,, alikaa kama nusu saa akaja kunifata nikashuka akanishika mkono tukaelekekea upande wa magari,,, akawaita wafanyakazi wake akawaambia msaidieni mke wangu kuchagua gari zuri lenye thamani yeyote ile nikajikuta machozi yananitoka nikaanza kuchagua gari, huku cjui hata aina ya magari,, wale wadada wakawa wananisaidia, nikachagua Verossa, bc Mahamood akawaambia wale wafanyakazi waandike jina langu kwenye kadi,, tuliondoka hadi Hotelini tukala tulifurahi yaan Mahamood alifurahi sana sana tena ckutegemea kesho yke akanipeleka driving school ili nijifunze kuendesha gari,,, akaniambia Mamujee nakuoa sasa ctaki mtoto azaliwe kabla ya ndoa,,, huku naendelea kujifunza gari nikawa nakaribia kumaliza,,, cku hio kanifata shule tukaingia kwenye gari yake hakuniambia tunaenda wp,, tukafika sehemu akapaki tukashuka huku akiwasiliana na watu,, kumbe alikuwa anaenda kuninunulia kiwanja Salasala jmn jmn Mamujee mie umasikini kwisha tena mhhhhh!!! Bc nikaonyweshwa kiwanja changu kikubwa sana kipo kwenye ramani,, nikamshukuru sana huku nalia,, akaniambia hapana ww ni mke wangu,,, akaniambia hapa nakujengea ghorofa mhhh!!! Bc tulirudi nikawa naweza kuendesha gari sikuchukua mda mrefu sana nikakabiziwa gari yangu na kadi yangu yenye jina langu,, Mahamood alikaa sana kama miezi miwili iv akaniambia anaenda Dubai kumpa taarifa mke mkubwa, ataenda na kwa mdogo, ili tuje kufunga ndoa rasmi,,, hapo kule Salasala ujenzi unaendelea
Nitarudi!!!!
 
Sehemu 1

Naitwa Mamujee, ni mzaliwa wa Musoma. Sijabahatika kusoma sana, niliishia kidato cha pili sababu ya kukosa mtu wa kunisomesha pindi tu nilipofiwa na baba yangu. Mama yangu alifariki kitambo sana tangu nilipokuwa darasa la nne. Baba yangu alipofariki tu, mimi nikachukuliwa na shangazi yangu anayeishi Dar es Salaam, huku kaka yangu akipelekwa kwa shangazi yangu mwingine anayeishi Arusha. Tumezaliwa wawili tu, mimi na kaka yangu.

Nilipofika Dar kwa shangazi, nilipokelewa vizuri. Shangazi yangu alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Pale nyumbani tuliishi na mjomba pamoja na watoto wa shangazi watatu. Kiufupi, pale nilikuwa kama house girl, kazi zote za nyumbani zilikuwa zangu. Watoto wa shangazi walilelewa kama mayai, hawawezi kufanya kazi yoyote. Tuliishi vizuri na shangazi huku nikiendelea kuwa mfanyakazi pale nyumbani, lakini sikujali kwa sababu nilijua mimi ni yatima sina pa kwenda, hivyo nikavumilia.

Ilikuwa imepita kama mwaka tangu nije Dar, nikawa mwenyeji na nikazoea jiji vizuri japo sikuwa mtu wa kujichanganya sana. Siku moja niliamka nyumbani na kuanza kufanya usafi kama kawaida. Shangazi na wanae walikuwa wametoka. Nilikuwa bize sana na kazi zangu, sikujua kama mjomba yupo ndani. Nilipomaliza kazi, nikaingia bafuni kuoga ili nijiandae niende Solomon.

Niliporudi chumbani kwetu nikivaa, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu. Mjomba akaingia chumbani na kunikamata kwa nguvu huku akinifunika mdomo. Mjomba alinibaka! Nililia sana. Sikuwahi kukutana na mwanaume tangu nimezaliwa, na mjomba ndiye alikuwa wa kwanza. Niliumia sana. Baada ya tukio hilo, mjomba alinitishia kuwa nisithubutu kumwambia mtu yeyote, la sivyo angeniua.

Nililala chumbani nikiwa na maumivu makali hadi shangazi aliporudi. Alinikuta nikiwa chumbani bila hata kupika chakula. Akaniuliza, "Mamujee, mbona hujapika chochote na umelala? Kulikoni?" Nikamjibu nalia, "Naumwa." Akaniambia niende nikanunue dawa. Niliposimama kuchukua hela kwa shangazi ili nikanunue dawa, nilitembea kwa shida huku nachechemea. Shangazi aliponiona nashindwa kutembea vizuri, akaanza kuwa na wasiwasi.

Akaniuliza, "Umefanya nini huko chini hadi unashindwa kutembea?" Alinipiga sana akinituhumu kuwa nimeanza umalaya, akidai nimtajie mwanaume aliyenifanya hivyo. Niliomba msamaha huku nikilia na kumwambia mimi si malaya, lakini hakunielewa kabisa. Kipigo kilipozidi, niliamua kumwambia shangazi ukweli kuwa mjomba ndiye aliyenibaka.

Badala ya kunielewa, shangazi aliniita muongo na kusema namsingizia mumewe. Alidai mimi ni malaya tangu utoto na nimerithi umalaya wa mama yangu. Hakutaka kunielewa wala hakutaka kumsubiri mjomba ili amuulize. Aliniambia nitoke nyumbani kwake mara moja. Aliingia chumbani, akabeba begi langu na kuniita nje. Akaniambia niondoke na kunipa shilingi elfu 60 ili nitumie kama nauli ya kunifikisha Musoma.
Santeeeee
 
Back
Top Bottom