Kwa ndoa ya Kikristo kuachana ina kaugumu kake kidogo
Mmezaa watoto 2, its obvious mnaweza kuamua kuachana na mkafanikiwa lakini after 2 years nyote mtakuwa kwenye majuto nikimaanisha Wakwe ambao wamelianzisha, Wewe, Mkeo na Watoto
Ni wazi kwamba tatizo liko kwa Wazazi wa mkeo, na ni wazi vile vile kwamba Mkeo aidha ni mdogo kwa umri au hajapevuka kiakili na yeye ndiye ataejuta zaidi mambo yakishaharibika. Kuisaidia ndoa yako ni jinsi gani unamfanya mkeo anazinduka ktk lindi la tashwishi za Wazazi(hasa Mama)
1. Unaweza fanya kikao na Baba Mkwe tu akiwa na Mzee mwingine ambaye ni Rafiki yake wa karibu umuelezee dukuduku zako na usistize kwamba huna lengo la kumuacha mkeo. Kama Baba nimuelewa wa maisha na hajashikwa na mkewe na yeye ndiye Breadwinner pale nyumbani una nafasi kubwa ya kuiokoa ndoa yako kwa kumtumia yeye. Kaa naye karibu, jinyenyekeze atawiwa kuokoa ndoa yenu, wachaga ni waelewa saana ikiwezekana tafuta hata wazee wa kichaga ukae nao kwanza ili wakapambane na mwenzao
2. Tafuta shangazi yake muelewa, shosti, au Mama mwenye hekima katika Jumuiya(for catholics) au jamii, ampe mwanga wa maisha, amwonyeshe vile jinsi gani anavyopeleka maisha yake shimoni ampe na case studies
3. Viongozi wa Dini nao ni muhimu, kama mtakuwa na vikao ambavyo vinahusisha familia zote mbili. Watanzania bado tunaithamini dini hivyo kuwepo kwa watu wa dini kunaweza rudisha nyuma nia ovu.
4. Tengeni Muda na Mahali
Wakati mwingine mazingira yanaweza kuwa kikwazo hebu tafuta muda muende mbali na mlikozoeaga kwenda. Mnaweza kwenda Magoroto, Zanzibar au Mafia au popote kulingana na uwezo wenu. Lengo ni kuonyesha thamani ya umoja wenu ukilinganisha na hasara ya utengano wenu
5. Acha Kuchepuka
6. Mtafutie shughuli ya kufanya, fuatilia kila mara anaendeleaje. Ni kawaida kwa wamama wa Nyumbani(most of them) kuona pesa huwa zinapatikana kiurahisi hivyo unaposhindwa kutimiza matakwa fulani anajua unafanya makusudi
7. Hamad Kibindoni, Silaha Mkononi
Usikae kiboya, seek legal advice kwa Mwanasheria ikibidi ulipie kabisa sio humu JF, ili silaha za kidiplomasia zikishindikana uwe unajua muelekeo
8. Muombe Mungu kikombe kikuepuke. Nguvu ya kuamka usiku na kuomba Mungu ni kubwa sana, ikiwezekana hata kufunga ufunge, hasa hasa linapokuja suala la watoto